Mwenye jibu la wizi wa mitandao ya simu ni huyu hapa

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,451
486
Nimeona watu wakilalamika sana kuhusiana na suala zima la kuibiwa muda wa maongezi au transaction wanazozifanya kupitia mitandao mbalimbali hapa nchini, na pindi wanapotafuta mtu wa kuweza kuwatatulia tatizo hili wanaishia kupigwa danadana .
Sasa kama ulikuwa hujui mtu mwenye uwezo wa kushughulikia suala hili, basi ni TCRA kwani hawa ndio wanaowajibika kwa suala zima linalohusiana na mfumo mzima wa mawasiliano na wapo pale kwa ajiri yetu.
 

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,359
2,329
TCRA hawana ubavu wa kuzikemea wala kuziadhibu kampuni za simu pindi zinapoenda tenge kwani mlo wao wa kujiendesha unatoka hapo,jiulize masuala ya usajili yameishia wapi,central registry for imei nk.
Wenzao Kenya na Rwanda at least wanaregulate na kuspervise ipasvyo,mfano ni simu fake zilivyoondolewa mtandaoni Kenya na kule Rwanda kampuni ikitoa huduma dhaifu inapigwa fine kwa masaa yote ilipokuwa imewasumbua wateja.
Mfumo uliounda mamlaka hii na Ewura haufai kwani unamsimamia mtu unaetegemea kula yako kutoka kwake
 

mbota

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
929
414
asante sana ila TCRA ndio waowapa award za kutoa huduma bora kwa hao wanaoongoza kwa kutuibia ......... watch out and you can realize what i say///
 

Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,854
1,129
Nimeona watu wakilalamika
sana kuhusiana na suala zima la kuibiwa muda wa maongezi au
transaction wanazozifanya kupitia
mitandao mbalimbali hapa nchini, na pindi wanapotafuta mtu wa kuweza
kuwatatulia tatizo hili wanaishia kupigwa danadana .
Sasa kama ulikuwa hujui mtu mwenye uwezo wa kushughulikia suala hili,
basi ni TCRA kwani hawa ndio wanaowajibika kwa suala zima
linalohusiana na mfumo mzima wa mawasiliano na wapo pale kwa ajiri
yetu.

Wee! vipi? kwani hatuwajui hao wezi?
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,530
Tatizo si TCRA bali kuwa na viongozi wafanya biashara kiasi cha kuwa na hisa kwenye hayo makampuni jambazi ya simu. Nadhani Tanzania inaongoza kwa kutoa huduma mbovu na kutoza viwango vya juu vya simu na umeme katika Afrika.
 

gastone

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
329
113
Alafu ukitaka ujue ccm lao wote moja mwangalie january makamba, toka aingie hapo kimya kama hajui kinachoendelea! Msambaa huyu mnafiki kweli kweli amebaki kudanganya wanabumbuli tu kwa sababu na wenyewe pia wanaishi kimazoea!!
 

mtotowamjini

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
4,527
1,163
hivi mnajua hii mitandao ya simu inawaibia hela sana wateja wao na wala hawana habari...wewe fikiria kila mtu akiibiwa shs 50 kwenye simu yake atajua? ukiiba sh 50 kila siku kwa watu 100000 hiyo ni million 50 so kuna watu wanaweza wakawa wanapata million 50 kila siku kwa uwizi...ndio ujiulize kwa nini ma boss wa hii mitandao wanapata bonus million 200 na zaidi...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom