Mwenye hatimiliki ya nchi yetu ni nani? Mwananchi mwenyewe?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Mungu alipomuumba mwanadamu, baada ya kukiuka miiko ya kuishi katika bustani ya Eden akamtupa duniani na akamwambia aitawale dunia pamoja na vilivyomo(Mazingira yake)!
Kwa upande mwingine kabla ya ukoloni jamii zetu hasa za kiafrika ziliishi katika koo mbali mbali na kujiundia dola ili ziweze kujitawala, kulikua na viongozi wa koo au dola/himaya hizo! Kilikua na taratibu ambazo zilijiwekea na maisha yalienda barabara kabisa.Walizaliana,wakakua na wakapanuka na wengine walikufa.


Baada ya kuingia ukoloni jamii hizi zilifunzwa maisha mapya, zilifunzwa ustaarabu na utaratibu mzuri zaidi wa kuishi! Na kweli kabisa baada ya wakoloni kuona ndugu zao hawa wameshabadilika ndipo wakaondoka na kuwaachia maeneo yao wajitawale kwa utaratibu uliobora kabisa kuliko ule wa kijima.


Hapa kwetu Tanzania baada ya wakoloni kuona sasa tumeelewa na werevu wamepatikana wakaamua kutuachia himaya yetu chini ya Uongozi wa hayati baba wa Taifa Mwl JK Nyerere alikaa pamoja na wenzake wakitumia chama cha TANU kama taasisi ya kisiasa iliyowaweka pamoja wakapanga ni vipi namna namna ya kuliendesha taifa moja bila kujali rangi, kabila wala dini ya mtu! Waliandika katiba ambayo ilimpa kila mtu kua na Uhuru wa kutawala pasipo kujali ni wapi anatoka au ni wa dini gani! Hakuna kipengele hata kimoja ndani ya katiba hiyo kinasema kua ukoo flani utatawala milele taifa lenye makabila tofauti na lake.


Haikutosha hapo kwa uungwana wao na kutumbua uwezo wa kila Mtanzania kutoka katika sehemu mbali mbali(pengine lilikua ni shinikizo la wakubwa zetu) basi mwaka 1992 wakamua kuwepo na kitu kinachoitwa "Mfumo wa vyama vingi", mfumo huu likua na maana ya kwamba wewe ukiwa kama mtawala Mawazo yako lazima yawe na mbadala kupitia chama kingine, lazima ukosolewe kupitia Chama kingine,utambue kua kuna siku nawe utakua mpinzani wa huyo mpinzani siku akiwa mtawala! hakuna mahali wewe utatawala milele, ni lazima na mwenzako naye ipo siku atatawala kwa sababu watangulizi wetu walituunganisha sote kutokea maeneo mbali mbali kwa hiyo kila moja ana haki sawa na mwezake.


Hiki kiburi cha kusema flani hawezi kutawala labda kwa mtutu wa bunduki kimetoka wapi? Kitendo cha kusema kanda flani haiwezi kuongoza taifa kimetokea wapi? Kwanini hatujiulizi kua kabla ya ukoloni tulikua tukiishi katika matabaka yaliyokua yakijitawala yenyewe? Ndio tunakotaka kurudi? Ni vipi tunaenzi ustaarabu ulionzishwa na watangulizi wetu?


Kuamka usingizini na kuwaambia watanzania ambao walikwishaunganishwa pamoja tena kwa lugha moja kua kuangalia live vikao vya bunge kwa utashi wako binafsi si matusi ni nini? Kwani wao walikuambia kua hawahitaji kuangalia kwakua wako makazini? Huu utashi wa kutaka kujimilikisha Mali ya watanzania wote na kuifanya yako unataka kuwaambia nini?Hujui chombo kinachoitwa cha Taifa ni cha watanzania wote kwa wenye vyama wasio na vyama?


Wenye hatimiliki ya nchi yetu ni sisi wananchi wala sio taasisi flani au kikundi flani cha watu, huo mkataba wa kumilikishwa nchi kwa kikundi haupo na haujawahi kuwepo! Taifa ni la watu wote Kwahiyo mtawala anaweza kua yeyote pasipokujali anatokea Chama gani au kabilia gani ama dini gani.



Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Back
Top Bottom