Mwenye gari namba T 696 BUC anitafute haraka

Habari zenu wakuu?
Bila shaka mko salama!

Kuna taarifa fupi tu ningependa kuwapatia.

Kuna gari imepaki sehemu fulani hapa Dar es salaam kwa takribani miezi minne sasa bila taarifa yoyote.

Mwenye gari hajulikani wala haijawahi kuja kuuliziwa.

Mpaka sasa tunashangaa hii gari alieipaki kapatwa na shida gani mpaka kashindwa kuirejea?

Au ina majanga gani hapa jijini?

Gari namba ni T 696 BUC, RANGI YA BLUE BAHARI. Gari ni ndogo tu ya watu 4-5.

Haina tatizo lolote kama kuondolewa vioo, tyre wala nini. INALINDWA MPAKA MWENYEWE AJE na atoe maelezo.

Kama una taarifa zake njoo PM

(picha sitaweka hapa kwa sababu maalum)
Nenda Polisi, watafuatiliwa TRA na atapatikana
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom