Mwenye duka ndie anaejua faida ya duka

Princemwalejr

JF-Expert Member
Nov 9, 2017
496
488
Mwenye duka ndie anaejua nani wa kumuuzia bidhaa zake na auze bidhaa kiasi gani na wakati gani aziuze. Mwenye duka ndie mwenye hiari ya kumkopesha mtu bidhaa, ndie anaepanga bei za bidhaa zake. Mwenye duka anajua nini afanye kukwepa kodi au kuficha faida yake kwa wanaomdai.

Nazungumzia dili la madini. Ni kweli mafanikio yaliyopatikana ni makubwa lakini kazi bado ipo sana. Acacia wanaweza kukopesha dhahabu au kuziuza kwa bei ya kutupa kwa kampuni yao ya jina jingine. Hapo Tanzania itaendelea kuambulia patupu kwenye mgao wa 50/50. Isipoangalia inaweza kupata hata deni.

Waarabu wanapopanga bei za mafuta, wanapodhibiti kiwango cha uzalishaji wa mafuta ni kwa sababu wanamiliki visima vya mafuta yao. Na ndio maana matajiri wa kutupwa wako Arabuni.

Ni lini Afrika itamiliki utajiri wake? Tusijidanganye utajiri wa Afrika ya kusini bado unamilikiwa na wazungu. Na kwingine kote Afrika umiliki wa utajiri wa maliasili mambo ni shaghala baghala. Umiliki wa asilimia 16 kwa dhahabu za nchini kwako si jambo la kujivunia hata kidogo.
 
Back
Top Bottom