Mwenye details nzuri kuhusu Gari Suzuki Kei naomba upite hapa

chamng'asi

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
211
385
Niko mbioni kununua hii gari kwaajili ya familia... Nimependa muonekano wake na pia injini ni ndogo cc 650 nitaimudu. Hofu yangu sijui chchte kuhusu hii gari. Msaada tafadhali kwa wajuvi wa mambo...
 
Umesema uko mbioni kununua hilo gari kwa ajili ya familia?

Kubeba familia na engine ya cc650? Haina nguvu ya kutosha. Kuwa na gari isiyo na nguvu ya kutosha kwa matumizi unayohitaji sio salama mkuu.

Pia kama unabeba familia manake engine itakuwa inafanya kazi kwa nguvu kubwa (high rpm) muda mrefu hivyo kuichosha haraka.

Nafasi ndani ni ndogo kwa matumizi ya familia. Udogo wa gari unamaanisha itokeapo ajali kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kupata majeraha.

Maana ya Kei car kwa wajapani ni city car. Inafaa kwa safari za mjini kwenye foleni kubwa na limited parking space.
 
Nunua gari yenye kuanzia cc 1200 mpaka 1,500 ulaji unafanana umesema unataka Family Car hako kagari kakibeba watu wanne walioshiba kupanda mlima shida.

Sister anayo hio gari anapokaa kuna milima kikiwa kinawatu wanne walioshiba mpaka washuke ndo kipande mlima. Ila nunua mkuu roho ya paka hiyo gari.
 
Sio nzuri kwa familia...aidha wewe na mwanao mmoja.

Cc 650.
 
Nimewahi kulimiliki. Matumizi ya mafuta ni madogo sana. Tatizo haliwezi kupanda milima hususani kwenye njia za vumbi. Pia njia zenye mbavu za mbwa inarukaruka balaa
 
Ni nzuri kwa ulaji wa mafuta ila kinahitaji service mara kwa mara kwa familia hapana hakifai ni gari ya mizunguko midogo kwa hapa Town mimi ninayo ipo ktk hali nzuri kama unahitaji nicheki nikuhuzie
 
Mkuu nashukuru sana
 
Nunua gari yenye kuanzia cc 1200 mpaka 1,500 ulaji unafanana umesema unataka Family Car hako kagari kakibeba watu wanne walioshiba kupanda mlima shida.

Sister anayo hio gari anapokaa kuna milima kikiwa kinawatu wanne walioshiba mpaka washuke ndo kipande mlima. Ila nunua mkuu roho ya paka hiyo gari.
Oooh sawa ndg shukurani kwa elimu
 
Umesema uko mbioni kununua hilo gari kwa ajili ya familia?

Kubeba familia na engine ya cc650? Haina nguvu ya kutosha. Kuwa na gari isiyo na nguvu ya kutosha kwa matumizi unayohitaji sio salama mkuu.

Pia kama unabeba familia manake engine itakuwa inafanya kazi kwa nguvu kubwa (high rpm) muda mrefu hivyo kuichosha haraka.

Nafasi ndani ni ndogo kwa matumizi ya familia. Udogo wa gari unamaanisha itokeapo ajali kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kupata majeraha.

Maana ya Kei car kwa wajapani ni city car. Inafaa kwa safari za mjini kwenye foleni kubwa na limited parking space.
Mkuu asante mno.... Sina swali tena umemaliza
 
Yani baba, mama na watoto mnajazana kwenye suzuki kei.. Si mtakua mnapumuliana sana.. Labda ukifanye cha kuwapeleka watoto shule
 
Back
Top Bottom