Mwenye contact za Mh. Dkt. Jakaya Kikwete

kayanda01

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
1,142
971
WanaJF wote heshima kwenu...

Mimi ni kijana mtanzania, aged below 29 years, jinsi yangu: Me.

Wakuu, nahitaji sana kuonana au kuwasiliana na Rais mstaafu ndg. Dkt Jakaya Kikwete.

Nina shida sana ya mtaji ili kuinua kibiashara changu kidogo. Nina shida ya Tsh Million 5. Nataka kumuomba mh. Jakaya anisaidie hata kwa kunikopesha, nitairejesha ndani ya miezi kumi.

Huko kwenye mabenki na taasisi za kifedha sikopesheki maana nashindwa kutimiza msharti ya dhamana. Hivyo, ndipo fikra zangu zikanielekeza kwa mh. Jakaya. Binafsi huwa nina imani kubwa sana kwa huyu baba, ana moyo wa kiungwana sana.

Aidha, Lengo Kuu la kufanya biashara ni kukusanya pesa ili niweze kujisomesha chuo (bachelor degree) kuanzia mwaka huu au mwaka kesho. Nimefanya Admission application mwaka huu lakini sina kabisa tumaini kama nitapata mkopo wa HESLB maana sera za bodi ya mikopo zimebadilika. Mimi ni mtoto wa mkulima, so nimeanza tu kujiandaa kisaikolojia mapema na kujipanga. Napambana ili nijikwamue kimaisha na kulijenga Taifa pia. Failing to PLAN is planning to FAIL!

JF ni jukwaa kubwa with high esteem na lenye watu wa status mbali mbali. Hivyo basi, kwa yeyote humu mwenye contacts na mh. Dkt Jakaya Kikwete, naomba sana anitumie Private Message. Nafahamu yaweza kuwa sio rahisi kupata contacts zake, basi ama mtu yeyote anisaidie kumfikishia ombi langu hili.

WanaJF, my sincere appreciations in advance to you all, for any kind support that you may render to me in that regard.

Stay blessed.

Email: kayandac@yahoo.com
 
Mkuu kama una mpango wa kusoma tafuta namba za Prof. Ndalichako ila kama ni mtaji nazani JK au wale nduguze waweza saidika

pia usiwe mgumu kukabiliana na maswahibu kwani kuna njia zaid ya elfu za kutatua tatizo lako, jaribu kuitazama njia iliyokaribu yako zaidi.
 
Nenda ofisi za CCM, Lumumba Dar. Wacha barua yako pale administration na ataipata, amma atakupangia miadi ya kuonana nae amma atakupatia mtu wa kukupatia ufumbuzi tatizo lako.

Pia Lumumba unaweza kuomba miadi ya kuonana nae na watachukuwa namba za simu zako na watakupangia muda na siku ya kuonana nae.

Jaribu kufupisha maelezo na usifanye kama ulivyoyaleta hapa.
 
Back
Top Bottom