Mwenge wa Olympic Tanzania

Mwazange

JF-Expert Member
Nov 16, 2007
1,056
81
Wandugu kama tuonavyo jinsi mwenge wa Olympic unavyoleta zengwe duniani kote. Kasheshe la London, Paris, leo huko San Fransisco, Je na sisi tumejiandaa vipi na mapokezi yake? au FFU ndo watakaoukimbiza mwenge, maana wajamaa wale wana kale katabia ka kukong'ota kwanza maswali baadae. Haya kwa wale wenye mapafu ya kupambana nao kwa jina la haki za binadamu za Tibet, Taiwan, Darfur, na kwengineko. Nafikiri utatua bongo tarehe 13 mwezi huu ukitokea Bueno Aires, Argentina. Maoni, tuandamane vipi?
 
We wacha tu maana huwezi kujenga kwa mwenzako wakati nyumbani kwako kunateketea halafu wakubwa wa michezo hiyo wamepinga suala la michezo kuchanganywa na siasa wanasema mnawaharibia ulaji .
 
Maoni, tuandamane vipi?

dqlp55.jpg
 
ni kweli si busara hata kidogo kuchanga siasa na michezo haingii akilini.


nnategemea watanzania si watu wa kufata mkombo. tunaelewa kuwa wenye kuchochea maandamano wana ajenda zao nyengine chini ya zulia


ila serikali ya tanzania imehakikisha kuwa hatua zote imechukua kuhakikisha yaliotokea hulo hayatokei tanzania
 
Tanzania imepewa heshima kubwa ya kukimbizwa mwenge barani Africa,halafu tuandamane? kwa lipi?Si mantiki ya kuandama zaidi kuwa malumbukeni!
 
Tanzania imepewa heshima kubwa ya kukimbizwa mwenge barani Africa,halafu tuandamane? kwa lipi?

Na hiyo heshima ndo itakayowaonyesha hao waandamanaji ni kipi kilichomfanya panzi kutohudhuria mikutano ya kunguru(kurabi) 'watatafunwa'. Nani aandamane? Athubutu??
 
Tuandamane ili iwaje?, mimi nadhani tungeanza kwa kuandamana kuhusu pressing needs zetu kwanza then ayo mengine next!, tunaenda zima moto kwa jirani inhali nyumba yetu ina teketea pia?
Wanaondamana huko i guess pia wana ajenda zao za siri na sio inshu ya Tibet tuu!, i think pace of development ambayo China ina achieve so far ni threat kwa wao!, Even Bush has admitted that WE CANT MIX SPORTS AND POLITICS!
 
Back
Top Bottom