Mwenendo wa Uhamaji wa Waafrika katika nchi zao unaelezwa kuongezeka siku hadi siku

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,800
4,460
Mwenendo wa Uhamaji wa Waafrika unaelezwa kuongezeka siku hadi siku

African Migration Trends to Watch in 2022 – Africa Center for Strategic Studies wanaeleza kuwa Idadi ya Uhamaji wa Waafrika ndani na Nje ya Afrika inaelezwa kuongezea karibu mara mbili zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2010, na inatazamiwa kuendelea kupanuka zaidi kwa miongo miwili ijayo. Tazama data zifuatazo kutoka UN DESA zikionesha hali ya uhamiaji tangu mwaka 1990 mpaka 2020.

1647146664426.png

Picha: data za UN DESA zikionesha hali ya uhamiaji tangu mwaka 1990 mpaka 2020
Suala la uhamiaji barani Afrika limekuwa linachochewa na sababu mbalimbali kulingana na eneo husika. Kuna Waafrika wanaohama kutokana na kuvutiwa na mambo fulani yanayopatikana eneo husika na wengine wanalazimika kuyahama makazi yao bila kupenda.

Miongoni mwa sababu zinazowasukuma baadhi ya Waafrika kuyahama makazi yao ni pamoja na kuwapo kwa migogoro katika nchi zao. Inaelezwa kuwa takribani nchi 15 za kiafrika wakazi wake wanahama kutokana na kuwapo kwa migogoro.

Inaelezwa kuwa nchi za Afrika ya Kaskazini ndio zinaongoza kuzalisha wahamiaji wengi wanaokwenda barani Ulaya zikiongozwa na nchi ya Moroko, Algeria, na Tunisia. Takwimu zinaeleza kuwa kati ya wahamiaji Milioni 11 wanaotoka Afrika kwenda Ulaya milioni 5 wanatokea Afrika Kaskazini.

Tafiti zinabinisha kuwa Wahamiaji wa Kiafrika waliopo Ulaya walipelekwa kwa sababu za ajira au masomo. Watunisia waliokimbia shinikizo la kiuchumi, kwa mfano, walijumuisha zaidi ya robo ya wahamiaji wasio wa kawaida waliozuiliwa kuvuka bahari ya Mediterania kwenda Italia mnamo 2021. Tazama vielelezo vifuatavyo kuona muenendo wa uhamaji wa Waafrika ndani na nje ya bara.


1647146862573.png

Picha: Ramani ya Afrika iliyoandaliwa na UN DESA ikionesha mielekeo ya Wahamiaji wa Kiafrika ndani na nje ya bara

1647146926781.png

Picha: Data za UN DESA zikionesha idadi ya Wahamiaji katika nchi za Afrika Tangu mwaka 1990 mpaka 2020
Idadi kubwa ya Wahamiaji wa Kiafrika hawavuki bara la Afrika
Inaelezwa kuwa uhamiaji wa Afrika kwa kiasi kikubwa unahusisha kutoka nchi moja kwenda nyingine ndani ya bara la Afrika. Takriban Waafrika milioni 21 waliohama sehemu moja kwenda nyingine wanaishi ndani ya Afrika.

Takwimu zinaonesha Waafrika wengi wanahamia Maeneo ya mijini katika nchi ya Nigeria, Afrika Kusini na Misri kutokana na ukuaji wa uchumi na mzunguko wa biashara katika maeneo haya.

Aidha, kwa upande wa Waafrika waliohama nje ya bara hilo milioni 11 wanaishi bara la Ulaya, milioni 5 wanaishi Mashariki ya Kati na zaidi ya Milioni 3 wanaisi Amerika ya Kaskazini.

1647147124296.png

Picha: Data zikionesha mataifa ambayo wakimbizi wengi wa Afrika wanaenda
Majanga ya Asili na Mabadiliko ya hali ya hewa yanatazamiwa kwenda kuongeza kasi ya uhamiaji Afrika
Inaelezwa kuwa Bara la Afrika linakabiliwa na na maafa mengi ya asili kuliko mataifa mengi duniani How Global Warming Threatens Human Security in Africa – Africa Center for Strategic Studies. Matukio hayo ni kama ukame, mafuriko, vimbunga na magonjwa ya mlipuko pamoja na kukosekana kwa utulivu.

Benki ya Dunia inakadiria kuwa Afrika kutakuwa na wahamiaji milioni 86 Groundswell Part 2 : Acting on Internal Climate Migration watakaochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika ifikapo mwaka 2050.


Credit: African Center for Strategic studies
 
Back
Top Bottom