Mwenendo wa siasa Tanzania

huko kwenu vipi

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
1,519
1,462
Habari wanajamvi......

Nimekaa na kutafakari kwa muda mrefu bado sijapata mwafaka wa ninachokitafakari hivi siasa za Tanzania ni sehemu za kupiga dili?

Siasa za Tanzania ni kwa ajili ya "conflict of interest"kwann WANASIASA wa Tanzania hawasimamii wanachokiamini??

Kwann wanasiasa wa Tanzania wanayumbishwa na Vyama vyao badala ya kusimamia wanachokiamini??

Hivi ni nani katuloga?

Umekuwa CCM tangu anaingia kwenye siasa takriban miaka 50 upo ccm Leo hii unatoka CCM unaenda chama kingine mfano unahamia CHADEMA,CUF,NCCR-MAGEUZI halafu unakuwa mkosoaji no one wa serikali ambayo ulikuwa huko takriban miaka 5O kwann hukukosoa ulipokuwa huko??

Je umekihama CCM kwa maslahi binafsi?????

Sheria zote za mikataba umezipitisha wewe kwa kukaa kimya bila kupinga chochote Leo hii unaona ile sheria uliyopisha wewe imekuwa ya hovyo kwann hukupinga wakati mnaipitisha???

Wanasiasa tuwe na desturi ya kuchambua vitu na pengine kupinga hadharani kama unaona/unahisi mambo yanaenda mrama bila kujali vyama vyetu

Sheria nying za Mikataba mbalimbali zimepitishwa pengine zimepitishwa kwa ushabiki wa vyama vyetu Leo tunalaumu je wakulaumiwa ni nan?????????

Kuna baadhi ya viongozi/wasiasa wamekihama vyama vyao na kuhamia CCM kisa tu MH RAIS MAGUFULI anafanya mambo mazuri yanayowagusa pengine ndo wameyasubiria kwa muda Mrefu

Swali ni huyu MAGUFULI atatawala milele???

Je akija Rais mwingine akaboronga aliyoyafanya Magufuli je watakikimbia chama na kwnda vyama vingine????

Je watu/wanasiasa kama hawa wanachokisimamia hasa ni kipi?????

Je watu kama hawa wanafaa kupewa Nchi na pengine kupewa uongozi katika sehemu mbalimbali?????

Wanasiasa kama hawa si wako kimaslahi zaid???

Je wanafaa kuwa viongozi??????

Ifike sehemu kiongozi asimamie anachokiamini,kukatwa kwenye chama isiwe kigezo cha mtu kukihama chama,

Kuna viongozi tuliwategemea wakijenge Tanzania mpya lakini wao ndo no moja kukiharibu sasa wananchi wa kawaida/maskini watafanya nn kuipeleka Tanzania mbele?????????

Wananchi pamoja na umasikin wao hawajawahi kukihama chama,Sasa hawa viongozi tunaowaamini wanarandaranda Mara Leo yupo huku Mara kule,


IFIKE SEHEMU VIONGOZI/WANASIASA WASIMAMIE WANACHOKIAMINI WASIYUMBISHE NA VYAMA VYAMA WAFANYE VITU KWA AJILI YA VIZAZI VIJAVYO WASIFANYE VITU KWA MASLAHI YAO BINAFSI(CONFLICT OF INTEREST)

Nawasilisha...
 
Back
Top Bottom