Mwenendo wa Siasa na Upinzani Tanzania

kabon14

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
1,233
867
Habari wakuu

Kuna kitu nmkaa na kujaribu kufikiria kuhusu mwenendo mzima wa kisiasa na upindanzani hapa nchin nimefikia kuhitimisha kuwa ni muda sahihi wa kuwa hapa tulipo hivyo kutokukubaliana na hali ilivyo sasa ni kuupinga ukweli na uharisia kitu ambacho itatugharim muda mrefu na resources nying bila mafanikio.

Binafsi sijawahi kaa na kuikubaki CCM kwa sababu kubwa ambayo ni kwamba nimewahi kuwa affected na hii kitu directly hivyo kuikubali nitakuwa napingana na ukwel na uharisia.
Tangu nijitambue kisiasa nimekuwa mfuasi wa CDM kwa sababu ni chama chenye watu makini,(hilo liko wazi hata CCM wanajua) lakini kuna tukio lililo nifanya nijiweke mbali na siasa (nitaeleza)

Matukio yanayotokea sasa nchini ambayo kwa namna moja ama nyingine yanahusishwa na siasa si mageni machoni kwetu.
Masuala ya kuminywa kwa uhuru wa habari, kutekwa,kuteswa na kuuawa kwa raia kwa sababu za kisiasa yamekuwepo hata kabla ya awamu ya tano na katika kipindi hcho chote yamekuwa yakilaaniwa na kupigiwa kelele kama ilivyo sasa.
Tofauti ya zamani na sasa ni kuwa kwa kiasi flani zamani watu walikuwa huru kusema na kuikosoa serikali hadharani kitu ambacho kwa sasa hakuna, tumeshuhudia msururu wa matukio ya watu kuwekwa ndani kwa kujaribu kufanya hivyo (ishara mbaya kisiasa).

Madhara ya kuwaziba watu midomo ni pamoja na kukosa nafasi ya kujitathmini kama kiongozi hivyo utashindwa kujikosoa maana kila atakaye simama atazungumza mazuri ya kukufurahisha tu (ndo kinacho endelea sasa). Tunakosa watu wa kuyasemea mambo makubwa ambayo kwa namna moja ama nyingine yanatuyumbisha kama nchi katika nyanja za kijamii na kiuchumi. Ukisema, unadaiwa vyeti vya kuzaliwa vya bibi zako (Upuuzi).

Matukio ya watu kuhama vyama vyao.
Haya yamekuwa yakitokea kwa kiasi kikubwa tangu CDM ipate nguvu kubwa ya upinzani miaka ya 2009 hivi, ambapo tulishuhudia watu weng sana wakihama kutoka CCM na kwenda CDM. Hadi mwaka mwaka 2015 tuliona CDM ikiwa na nguvu kubwa mpaka baadhi ya mawaziri wastaafu waliamua kuihama CCM (Hapa kama ni mtu mwenye akili utapata cha kujiuliza).
Ghafla upepo umebadilika sana, mwaka huu tumeshuhudia viongoz wengi wa vyama vya upinzani wakihamia CCM ikiwa mambo niliyozungumza awali bado yako palepale na hata zaidi.( Ni mwendo wa kusoma upepo tu)

CHADEMA inajiua yenyewe ndani kwa ndani. Tujikumbushe tukio kubwa ambalo kwa maoni yang naona ndo chanzo cha kuiporomoa CDM.
Niimani yang hiki chama kilikuwa na misingi imara sana hadi kufikia hatua ya kuiteka Tanzania katika tasnia ya upinzani, hivyo ilipaswa CDM iendelee kusimamia misingi yake. Tukio la kumsimamisha Lowasa kuwa mgombea kupitia CDM punde tu baada ya kujiengua CCM ni tukio lililo badilisha mwenendo mzima wa siasa nchini na hii ilinipa fursa ya kuifahamu picha harisi ya siasa Tanzania, kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusiana na tukio hilo.
Tangu hapo tulishuhudia kuondoka kwa vichwa matata sana vya CDM ambavyo ni imani yangu vilijua misingi na mwenendo wa CDM (Mwanzo wa upinzani kuanza kuyumba)

Nilichanganua mambo kwa utashi wangu ni kaona ni muda sahihi wa kuachana na mambo ya kuwa mfuasi wa siasa na kuwa huru maana tangu hapo nilikosa mvuto na siasa ya aina hii.
Kwa sasa CCM wanautumia udhaifu wa CDM kustawi upya, hii ni baada ya kugundua kuwa CDM kuna njaa hivyo wanapenyeza rupia tu na kuwavuta (Ni sawa kwa sababu CDM walimruhusu adui kuujua udhaifu wao).

Hapa mimi binafsi nahitimisha kwa kusema siasa za Tanzania ni za kuchumia tumbo na ni wanasiasa wachache wenye uzalendo na vyama vyao. Tujipange upya.
IMG_20180929_150517.jpg
 
Hili badiko ukilisoma kwa umakini na kuwa freeminded utapata kaukweli fulani.

By the way siasa ya Tanzania haina misingi zaidi ya opportunities.
 
Hapa mimi binafsi nahitimisha kwa kusema siasa za Tanzania ni za kuchumia tumbo na ni wanasiasa wachache wenye uzalendo na vyama vyao. Tujipange upya.View attachment 882008
Umenena vyema sana, hongera kwa kuwa mkweli na muwazi
 
Kotekote hata kwa Misuxx FC,hawapendi kuambiwa wanapenyeza rupia
Mbona lowasa alipenyeza rupia ili dr silaa mfia chama akimbizwe nduki..wakati tofauti na wengine ye alimuweka kwenye maandamano hadi mkewe bila kujali hatari mbele yake.
 
Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    15.1 KB · Views: 19
Back
Top Bottom