Mwenendo wa serikali ya awamu ya 5, je ni matokeo ya CCM kupoteza dira?

electroma

Member
Jul 29, 2017
6
15
Amani iwe nanyi, nimetafakari kwa kina mwendokasi wa serikali ya awamu ya tano na kugundua sarakasi za kutisha. Mosi serikali hii haijatambua kipaumbele chake na wananchi kwa ujumla, yaani hakuna dira tunaelekea wapi zaidi ya kufanya mambo kwa kujihami na kutisha wananchi wake.

Sijaona wezi mapapa wakishughulikiwa zaidi ya vidagaa na kambale, sijaona ujenzi wa viwanda na kufufua vya zamani alivyotuachia mwalimu Nyerere na serikali ya kifisadi ya CCM kuviuza kwa bei ya kutupa, na kujimilikisha baadhi ya viwanda hivyo, sijaona maboresho ya maslahi ya watumishi wa umma pamoja na makazi yao na afya zao ni mwendo wa sarakasi za uhakiki mwaka wa pili huu n.k.

Napenda niwakumbushe watanzania CCM kwa kushirikiana na genge la wizi wamesaini mikataba mibovu na ya kinyonyaji inayowanufaisha wao na familia zao, anaebisha ajiulize kwa nini mpaka leo mijizi mikubwa nchi inalidwa na kutetewa na mwenyekiti wa CCM? Kama kweli huyu ndugu anatupenda watanzania na kututakia mema kwanini aingilie uhuru wa mahakama na bunge?

Mwenye macho haambiwi tazama tumefika hapa tulipo ndani giza kutokana na ulafi na wizi uliofanywa na viongozi wakuu ndani ya CCM ambao wanalindana na watalindana milele tusitegemee neema ndani ya utawala wa CCM hawa ni watu wakuogopa kama ukoma, tatizo watanzania wengi tumedumazwa akili na hawa ccm kiasi hata mtu akitukana wananchi wapiga makofi na kushangilia km majuha.

Tafakari kwa ajili ya kuja kuchukua maamuzi sahihi siku za mbeleni. Mungu tubariki watanzania. Viongozi wa CCM waliotupandikiza umasikini huu, na wao na familia zao kujitajirisha na kuishi kitajiri huku wakihubiri nchi hii ni masikini sana na sasa wanatupigania; unafiki ulioje?
 
Huyu bwana mkubwa angekuwa mzalendo wa kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu, angepeleka mswaada bungeni mshahara wake ukatwe kodi, hapo ningepambana ukoo wetu wote wawe wanaccm.
 
Hivi Seth Singh na Rugemalila sio mapapa? Wewe hupongezi hata makinikia? Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!!
 
Usitegemee ccm kuwa na mipango endelevu kamwe! Huko ni kujidanganya sana na kujitia ujinga. wengi Wapiga makofi hawajielewi wafuata Mkumbo. Poor peasants ndo walio wengi.
 
Dira ya Chama cha Mapinduzi kama sikosei ni " Chama kushika hatamu ya maamuzi,kurudisha maadili,nidhamu,hofu ya Mungu,cheo ni dhamana na watu wote ni sawa."
 
CCM kama ingalukuwa mboga wala nisinge igusa kabisa, na hata ikimwagwa wala roho yangu haiwezi kushtuka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom