Mwenendo wa matukio ya ugaidi, upinzani na vyombo vya ulinzi Tanzania

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Sina tafsiri halisi ya GAIDI ya Tanzania ila TERRORISM /noun the killing of ordinary people for political purposes. UGAIDI/jina[nomino] ni kuua watu wasio na hata kwa mlengo wa Kinshasa.

MAANA YA HATIA
Hatia ni ile hali ya kuvunja sheria au kuwa na kosa kisheria.
MAANA YA BILA HATIA
Bila hatia ni pale mtu anapopatiwa adhabu ama kwa kupindisha sheria au kutopefikishwa katika vyombo vya sheria.

MIFANO.
Mfano 1.
Tundu Lisu alipigwa risasi na tukio lile ni la kigaidi na sio la wasiojulikana wala ujambazi. Yawezekana Lisu kuna watu aliwakera na wakaona hana hatia, ndipo walipochukua short cut way.

MAAAJABU YA TUKIO HILI.
Serikali kupitia vyombo vya ulinzi 1. Hawajampata mhusi hadi leo na jarada limeliwa na mchwa.
2. Serikali via, hawajatambua ni kama shambulio la kigaidi
3. Seriikali ikaja na mthamiati mpya WASIOJULIKANA.

KWANINI MHUSIKA HATAPATIKANA
1 Kwa sababu waliotekeleza shambulio lile ndio hao hao wanaochunguza tukio. Hakuna mamlaka wala chombo kilichowahi kuchunguza tukio lile hadi leo.
2. Mganga hajigangi.

Mfano 2.
Mbowe yupo mahabusu kwa tuhuma za Ugaidi ambao haujawahi kufanyika.
Fikiria Ugaidi gani? Ule wa KIBITI?,MTWARA, RUVUMA? Ni vigumu kusema ana connection na Somalia.
Hapa naona kabisa Mbowe hana hatia na atafungwa bila hatia kwa sababu za kusiasa(UGAIDI NDIO HUU).

NANI ANAFADHILI UGAIDI TANZANIA?
Hapa labda serikali hii ya CCM ije iseme kwa namna ileile ya Hamza na Mbowe kuwa ni MAGAIDI.

TUKIO LA LISU KUSHAMBULIWA KWA SIRAHA ZA MOTO VS SHAMBULIO LA HAMZA DHIDI YA POLISI.
Naunganisha dots kwenye matukio haya mawili ambayo hayana mahusiano ila yana mfanano wa utokeaji wake.
1 barabarani
2 mchana
3 kuzua taharuki
4 siraha za moto kusikika
5 umwagaji wa damu.
Matukio haya mawili yanautofauti kwa namna ya;
Lisu ni Ugaidi na Hamza ni kisasi.
MAJIBU YA SERIKALI.
Lisu ni watu wasiojulikana na Hamza ni gaidi.
MASWALI.
Qn1.Kwa nini shambulio la LISU sio UGAIDI?
Facts gani zimetumika kusema tukio la Lisu sio Ugaidi?
Qn2. Kwa nini Hamza ni gaidi na uchunguzi wake haukuwa na mda?.

HISIA ZANGU MIMI FRUSTRATION.
1.Serikali inajua undani wa matukio haya ila wameweka siri kwa faida ya wachache.
2. Serikali haitambui umuhimu wa mwananchi kutoka upinzani na CCM ni Mwananchi na MPINZANI ni mgeni asie na kwake.

OMBI LANGU KWA SERIKALI
1 .Kuwafungulia mashtaka mawaziri na maofisa wote waliohusika na shambulio la Lisu.
2. Kuwa fungulia mashtaka wahusika wote waliomdhulumu Hamza mali zake.
3.Kesi ya Mbowe iendelee na haki itendeke. Nb kama amebambikiwa kesi basi watu wote waliohusika wafunguliwe mashtaka.
3. Katiba mpya ipatikane haraka.

FAIDA YA KUFANYA HIVYO
1. Kutengeneza jamii yenye umoja na upendo katika Taifa letu.
2. Kuondoa hali ya watu kuitesa jamii kwa kivuli cha madaraka na kinga
 
Kila zama na kitabu chake, ila wajao watakisoma hata kama mtu huyo yuko kaburini hakika matendo yake yatamfuata , na kila amdhulumuye mtu au kumuua dhuluma na damu ile hupatiliza vizazi vyake. Wako wapi watoto wa Hitler, Stalin , Samwel Doe, Polpot na wengineo na ulinganishe na wale waliotenda wema kama Mwinyi, Nyerere, Samora, Kenyatta, Churchhil, Che Guevara nk.
 
Back
Top Bottom