Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Katika uchambuzi wa ripoti za CAG za mwaka 2019/20, WAJIBU imeainisha maeneo yenye viashiria vya rushwa, udanganyifu na ubadhirifu wa fedha za umma. Kiasi ambacho aidha hakikukusanywa au kimetumika na Serikali pasipo kupata tija yoyote kimeongezeka kutoka TZS 232.52 bilioni mwaka 2018/19 hadi TZS 1,770.84 bilioni mwaka 2019/20.
Mamlaka ya Serikali zaMitaa ndizo zimekuwa na ongezeko kubwa zaidi kutoka TZS 103.93 bilioni mwaka 2018/19 hadi TZS 863.85 bilioni kwa mwaka 2019/20 kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 3.
Kati ya makusanyo na matumizi ambayo yanaviashiria vya rushwa, udanganyifu na ubadhirifu kwa mwaka 2019/20, Mamlaka ya Serikali za Mitaa ilikuwa na TZS 863.85 bilioni sawa na asilimia 49 ya TZS 1,770.84 bilioni ambapo kasoro nyingi zilionekana katika eneo la ununuzi wa umma na usimamizi wa mikataba.