Mwenendo wa CUF unanifanya nizichukie siasa za vyama vingi nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenendo wa CUF unanifanya nizichukie siasa za vyama vingi nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Penguine, Oct 4, 2012.

 1. P

  Penguine JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Mnamo mwaka 1992, rasmi Taifa letu liliingia katika Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa. Inaelezwa kwamba Mfumo huu haukuwa chaguo la Wananchi waliowengi (80% ya idadi ya watanzania waliohojiwa miaka hiyo).

  Hata hivyo, Mwl. Nyerere akaona siyo kweli kwamba waliowengi ndiyo wako sawa wakati wote; akaamuru nchi ifuate mtazamo wa wananchi wachache waliotaka vyama vingi (20% ya idadi ya watanzania waliohojiwa miaka hiyo). Mtazamo mpana ilikuwa ni katika umuhimu wa vyama vingi vya siasa nchini katika kuchochea uwazi, ufanisi na uwajibikaji wa serikali iliyopo madarakani.

  Kwa mtazamo wangu binafsi naona kama CUF inaenda kinyume na mtazamo huo mpana aliokuwa nao Mwl. Nyerere. Mtazamo wa vyama vingi vya siasa kusaidia kuleta maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla kwa kuchochea uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa Serikali iliyoko madarakani. CUF mmejisahau kabisa, mnatia aibu, mnaaibisha mmetupilia mbali dhana ya kuchochea maendeleo kwa kudai uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa serikali iliyoko madarakani. CUF mnapambana na SERIKALI KIVULI YA CHADEMA. Great shame!

  Siyo vibaya kuleta siasa za kukosoana, kuelimishana, kujengana na kurekebishana pale mnapoona mwenzenu fulani (here to mean chama fulani cha siasa miongoni mwenu) kinaenenda kwa namna ambayo haifai kwa ustawi wa taifa na watu wake. MKOSOENI na KOSOANENI kwa kuwa Tanzania ambayo kila chama cha siasa kinaililia kuiongoza ni yetu sote. Lakini katika hili, CUF hamko hivyo! Shame on you! Kazi yenu imekuwa ni kupambana na Serikali kivuli ya CHADEMA huku mkisahau kuleta uchochezi katika huduma bora za maji safi na salama mjini na vijijini, huduma za viwango vya juu ya elimu na mafunzo ya ufundi, kushuka kwa mfumuko wa bei na MFUMUKO WA UFISADI nchini.

  CUF mmekuwa mkiimba nyimbo zinazotyuniwa na CHADEMA kwa lengo la kukandamizana nyie wenyewe mlio vyama vya upinzani. Mfano wa nyimbo hizo ni wimbo wa Operation Sangara Mkauitikia, Wimbo wa M4C mmeuitikia, nasikia mmeanzakuitikia hata kwa wananchi kujishika kichwani ati kulaani wanaowatumia vijana katika siasa. very shame and severe lack of innovativeness.

  Ni maoni tu.
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni kweli wanaharibu upinzani...
   
 3. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Haoku peke yako Mkuu! Profesa Lipumba anajidhalilisha yeye, familia yake na wasomi wote kwa ujumla. Profesa wa Uchumi, lakini njaa inamsumbua na kutumiwa kirahisi na JK.
   
 4. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mimi pia nakuunga mkono ukisemacho ndicho nilicho kishuhudia kwenye mkutano wa hadhara ulioanda liwa na CUF leo jioni Lindi mjini.
  Viongozi wa Cuf na Mbunge wao waki piga porojo ambazo hazina maana katika siasa za vyama vingi japo baadhi ya hoja zao hasa za kiuchumi walikua sahih
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  CUF si wapinzani ni vibaraka
   
 6. P

  Penguine JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Mwalimu wangu wa somo la historia alikuwa anapenda sana kuyalaani baadhi ya makabila ndani ya Tanzania (Tanganyika as it was then) kuwa walikuwa collaborators walioungana na Wazungu kuwatesa na hata kuwaua Watanganyika Wenzao.


  Yule Mwl. alikuwa anapenda kila akiingia darasani kutuuliza: who can mention atleast three collaborators during colonial administration in Tanganyika? Tukawa tunayataja makabila hayo. Baadhi ya Wenzetu walioluwa wanatoka kwenye makabila hayo wakawa wanaona aibu, wanatazama chini, hawatuangalii usoni, hawakutaka hata tujue makabila yao japo hatukuwa na haja ya kutafuta ukabila. Halafu yule Mwl akawa anasema yazomeeni makabila hayo kwa kile walichokifanya, nasi tukawa tunazomea.

  Katika zama za vyama vingi tulizopo sasa endapo yule Mwl wangu angeniuliza mention just one political party which collaborates with the prevailing status quo? Ningewataja haraka CUF, nao CUF kwa aibu wangeniona ama kusoma majibu yangu wangeogopa kunitazama, wangeinamisha vichwa vyao chini, wangeficha kadi za uanachama wao katika chama hicho. Halafu yule mwl angesema wazomeeni hao ningezomea.


   
 7. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Acha kabisa tabia ya kupenda kusema wake za watu. Sio vizuri hivyo kwani mumewe ndie anayemtuma.
   
 8. Mwakitobile

  Mwakitobile JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 453
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Vibaraghashia 4 change. Rais profesa, waziri sheikh darasa la saba.
   
 9. P

  Penguine JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Una maana gani Kiongozi? Katika hili nani ni mume na Mke ni yupi?
   
 10. k

  kigu Senior Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni Chadema kufikiri kuwa wao wenyewe tu ndo wana weza kutatua matatizo ya watanzania !!.....Chadema wakiwashambulia CUF kuwa ni ccmb na huko mikoa ya kusini viongozi wa kitaifa wa CUF wakashambuliwa kwa matusi lakini ikaonekana chadema wako sahihi kabisa kuwashambulia CUF, tatizo linaonekana tu CUF wakiwaambia wananchi CCM haifai na Chadem vilevile haifai, tena inaonekana wanaua upenzani...., ni ujinga kufikiri kuwa CUF itakaa kimya kuona upotoshwaji dhidi yao.

  Tuwaache wananchi waangalie sera za vyama waamue ....huu sio muda wa propaganda, acha CUF inadi V4C yao na chadem waendelee na M4C yao.
   
 11. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,796
  Likes Received: 36,820
  Trophy Points: 280
  Hivi bado kuna kitu inaitwa cuf?

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 12. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kilianza CHADEMA kusema vibaya CUF. CUF wanajitetea tu! Halafu ONDOA hizo fikra mgando za kudhani CDM ndio upinzani pekee, huu ni ujinga wa ki-meku!
   
 13. n

  nemasisi JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 1,881
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hofu yangu ni kwamba mwisho wa siku vyama vya upinzani vinaweza kuanza kutafunana vyenyewe kwa vyenyewe au kiongozi mmoja dhidi ya mwingine
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  USINIUE.jpg
  Kilichobaki ni atakaye cha Uvunguni Sharti Ainame... Halafu Unaponda Kichwa Chake... Sasa Kama ni CUF na kukopi JUST PONDA KICHWA YAO HIYO CCM-B
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Wasingependelea Maneno ya JUSSA basi kama kweli wanapenda Upinzani wa Ukweli!!!
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Tangu lini CHADEMA wamesema hivyo ? Mbona CUF wasema watapiga kambi ARUSHA ? kama VILE hakuna Vyama Vingine ? Isipokuwa CUF na CUF pekee, na wakapokelewa na MKUU wa POLISI wa MKOA, MKUU wa MKOA Viongozi Waandamizi wa Mkoa Sasa hapo hauoni ya kuwa ni furaha na faraja kwa CUF kupendwa na CHAMA TAWALA ? Haukuona MKUTANO wa CUF ulifanana kama wa CCM ? Ulikuwa na MALORI na MABASI ya kubebaWananchi; Wananchi walikuwa Wamevaa Sare za CUF za kupendeza haswa kama wa CCM; Walisimika Mwanachama MMOJA tu kuingia CUF... na MAPOLISI HAWAKUWEPO KAMA VILE MKUTANO ULIKUWA WA CCM...
   
 17. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Viroba vya Lema @ work! Vijana angalieni, mnaharibikiwa!
   
 18. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Na nyie na mawazo ya kale ya nyerere hamfiki popote hivi bado hamuelewi ubovu wa sera zake ndio umetufikisha hapa leo
  Kwenye siasa opposition una oppose aliyeko madarakani pamoja na opposition wenzako
  CDM ya 2010 hayayatatokea 2015
  CUF wana stand juu zaidi
  Haya yalitokea wakati wa mrema
  Na ndio itavokua 2015


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. kukomya

  kukomya JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 344
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwa faida ya mume wao CCM! Shame on them.
   
 20. P

  Penguine JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Freeworld,
  Wasomi hawatukanani jukwaani, hurumbana kwa hoja. Hujenga utetezi kwa hoja, uthibitisho na mifano. Ndipo wanapotokea ama kubainika Great thinkers and not Great Sinkers. Jifunze busara ya namna hiyo mwanajamii; itakusaidia sana uwapo peke yako ama uwapo na Wenzio.

  Mimi siyo mwanachama w CDM bali mchambuzi tu wa mwenendo wa masuala ya kisiasa nchini. Ningeweza hata kuanza kumsifia Mhandisi Mbatia kwa ujenzi na uzito wa michango yake Bungeni. Hii isingekuwa na maana kwamba kwa kufanya hivyo naona NCCR MAGEUZI ndiyo chama pekee cha upinzani Bungeni rather giving the devil his due.

  Karibu kiongozi

   
Loading...