Mwenendo kesi za madai Tanzania!

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,007
1,893
Tafadhali, kwa wanasheria, tujaribu kujadili hapa na kuweka material. katika kesi za madai /civil nini kinaanza nini kinafuata hadi mwisho. stages zake. kuna watu wanauliza sana maswali humu hasa wanafunzi, naomba tusaidiane kuweka civil procedure kuanzia uandaaji wa plaint, kinachofuata ninini hadi mwisho hukumu. tuorodheshe iwe rahisi kwa wanaojifunza. pia nafikiri itasaidia raia wasiowakilishwa mahakamani kujua nini kinaanza nini kinafuata. kama una case laws nzuri pia tafadhali weka kwa faida ya wengi.
 
Suala la mwenendo wa makosa ya madai ni pana mno, nadhani njia nzuri ya kusaidiana kwa anayehitaji kufahamu atumie fursa hii kuuliza lolote ili ajibiwe kwa upana wake.
 
Nauliza kuna msemo unaoaminiwa sn mtaan kuwa... Deni halmfungi mtu.
Hii imekaaj ndg wanasheria.
Km n kweli je mdaiwa hupewa adhabu gn iwapo akigoma kulipa??
 
Nauliza kuna msemo unaoaminiwa sn mtaan kuwa... Deni halmfungi mtu.
Hii imekaaj ndg wanasheria.
Km n kweli je mdaiwa hupewa adhabu gn iwapo akigoma kulipa??
Katika kesi za madai kuna mazingira ya kisheria ambapo mtu anaweza kufungwa kwa madai ama deni, lakini mfungwa huyo wa madai yaani Civil prisoner atagharimikiwa matunzo na anayemfunga(mdai), lakini suala la anapogoma kulipa zipo taratibu za kisheria hufuatwa ili mdai aweze kupata stahiki zake, mfano mali zake zinaweza kuwa attached na kuuzwa ili kupata kiasi anachodaiwa.
 
Je, kuna ukomo kisheria mtu kudaiwa? Maana mwingine anaweza asikatae kukulipa bali hasemi ukomo.
 
Katika kesi za madai kuna mazingira ya kisheria ambapo mtu anaweza kufungwa kwa madai ama deni, lakini mfungwa huyo wa madai yaani Civil prisoner atagharimikiwa matunzo na anayemfunga(mdai), lakini suala la anapogoma kulipa zipo taratibu za kisheria hufuatwa ili mdai aweze kupata stahiki zake, mfano mali zake zinaweza kuwa attached na kuuzwa ili kupata kiasi anachodaiwa.

Mimi nina kesi ya madai dhidi ya halmashauri ya wilwyw ya Hai ambayo hukumu ilitolewa na mahakama kuu; je naweza kukamata mali zao ili kukaza hukumu?
 
Kwa hiyo unataka watu wasio Wasomi wajifunze na wakijua sisi Wasomi tutapata wapi hela.
Hilo si lengo langu, kama unachokisema ni sahihi, unadhani uwepo wa vipindi vya radio na televisheni vinavyojadili masuala ya kisheria pamoja na vitabu, makala za magezeti na vinginevyo vinaathiri upatikanaji wa wateja kwa watu wenye weledi kama mawakili na wengine wa kada ya taaluma ya sheria?

Najaribu kufikiri yaani unachokitaka watu wa kawaida wasijue chochote kuhusu sheria na haki zao ili wewe upate wateja?
 
Hapana, hilo laweza kufanyika kwa amri ya mahakama na kwa mujibu wa matakwa ya kisheria ila si chaguo tu la mtu

Je ni kweli kuwa mali za halmashauri haziwezi kukamatwa ili kukaza hukumu hata kwa amri ya mahakama kwani kuna sheria imepitishwa kuzilinda ?
 
Kimsingi na kisheria mali ya serikali haiwezi kuwa attached kwenye excution of decree( yaani kuwekwa kwenye kukaza hukumu)

Una maana raia hawana haki ya kulipwa na serikali mara seriakali[ kupitia watumishi wake ] wanapowakosea raia na mahakama kuamua hivyo?
 
Je raia hana haki ya kudai na kulipwa haki yake na serikali mara mahakama inapoamua hivyo? Kama serikali haitii amri ya mahakama na mali zake kisheria haziwezi kuwa attached, je raia wana njia gani ya kupata haki zao kufuatana na hukumu
Kimsingi na kisheria mali ya serikali haiwezi kuwa attached kwenye excution of decree( yaani kuwekwa kwenye kukaza hukumu)

ya mahakama ?
 
Kuna Dada nilikuwa nafanya nae Biashara ya Mchele yaani Mimi natoa Mchele Igunga na kusafirisha kumpelekea Ngara Dukani kwake alikuwa na duka kubwa tu nilikuwa namtumia mzigo baada ya week 1 anatuma hela kupitia account yangu sasa tulianza na kilo 500 toka mwwzi wa8 mwaka Jana alikuwa mwaminifu sana Lakini Mara ya mwisho Nilimpelekea Mzigo Kilo 3000 yaani tani3 nikasubiri kutumiwa hela hola baada ya week2 akaniambaia Kuna MTU alimwacha Dukani akauza mchele wote na kitoroka na hajui alipo hivyo kaibiwa kwa kweli nilichanganyikiwa sana nilipomwambia nini kifuatacho akasema nimpatie muda atakuwa analipa kidogo kidogo huu ni mwwzi wa3 sasa hajanilipa hata cent 1 nadai Million 4.5 sasa kila nikiomba ushauri nimshitaki mahakamani watu wananiambia nitapoteza gharama kubwa Bora nisamehe ukweli moyo wa kusamehe milion 4.5 huku sina hela naishi maisha ya kuunga unga nashindwa hebu nipatieni msaada nifanyeje???
 
Kabla haujachukua hatua za kisheria ,,kwanza hakikisha umeandaa vithibitisho ambavyo vitakufanya upate pakushika kama sehem ya ushahidi wa awali,kama vile "sms* wakati mnafanya mawaxliano ktk madai hAyo ,au vdiocall ,,audio & mashahidi wanao faham vizuri mtiririko wa biashara yenu. Lakini kabla ya hayo yote anza kumtengenezea mazingira yaushahidi bilA yeye kujua ,kwmba unamtengenezea mazngiera kama hayo.
 
Habari na pia poleni na majukumu! Hii mada niliitafuta kwa muda mrefu sana. Naombeni mnisaidie tatizo langu linalo nitia wazimu na kuishi kwa wasiwasi. Iko hivi uku nilipo kuna taasisi binafsi za kifedha ambazo sio benki na sijui kama zimesajiliwa ila zinatoa huduma za mikopo kwa watumishi kwa riba ya asilimia 40%kwa sh laki moja. Ambapo ukikopa unawapa kadi yako ya atm alafu wao ndio wanatoa pesa yao benki. Sasa mimi pia nilienda kukopa kwenye hizo taasisi na nikalipa deni likaisha. Ila nikaenda kukopa tena ila ghafla nikaanza kukatwa na bodi ya mkopo ivyo nikashidwa kuendelea kulipa deni lao kwa kuwa mshahara wangu ni mdogo sana. Na mbaka leo ni mwezi minne sasa wale watu wanataka kunishitaki na wananitishia kuwa nitafukuzwa kazi. Sasa je ni kweli nitafugwa? Kwa kesi hiyo
 
Katika kesi za madai kuna mazingira ya kisheria ambapo mtu anaweza kufungwa kwa madai ama deni, lakini mfungwa huyo wa madai yaani Civil prisoner atagharimikiwa matunzo na anayemfunga(mdai), lakini suala la anapogoma kulipa zipo taratibu za kisheria hufuatwa ili mdai aweze kupata stahiki zake, mfano mali zake zinaweza kuwa attached na kuuzwa ili kupata kiasi anachodaiwa.
Hapa nadhani ni wanapokuwa wanadaiana raia kwa raia,je inapokuwa raia anaidai serikali baada ya kuishinda mahakamani inakuwaje kwani sheria za kuishitaki serikali kuu tanzania zinazuia kukamata mali za serikali kuu
 
Hapa nadhani ni wanapokuwa wanadaiana raia kwa raia,je inapokuwa raia anaidai serikali baada ya kuishinda mahakamani inakuwaje kwani sheria za kuishitaki serikali kuu tanzania zinazuia kukamata mali za serikali kuu
Kisheria, hakuna mahakama yoyote yenye mamlaka ya kukamata mali za serikali ama kufanya jambo lolote linaloendana mfano kuuza, pale ambapo serikali ina kesi na inawajibika kulipa na mdai anataka kukaza hukumu. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa madai dhidi ya serikali yaani Government Proceedings Act. Kifungu cha 16 kifungu kidogo cha 3.

Kimsingi kama ingeruhusiwa hivyo, basi mali kama vile magari ya wagonjwa nayo yangeweza shikiliwa ama kuwa sehemu ya kukaza hukumu ili tu mdai alipwe stahiki zake, ni wazi kufanywa hivi kungeleta athari kubwa haswaa kuhatarisha haki za kimsingi za raia na maslahi ya uma. Kinga hii kwa serikali haimaanishi kwamba mdai hana haki ya kulipwa, sheria imeipa nguvu mahakama ili kuhakisha mdai anapata stahiki zake
 
Kuna rafiki yangu walikuwa na kesi ya kudaiana na jamaa yake mahakama ya mwanzo. Yeye huyo rafiki yangu ndiye alikuwa mdaiwa.

Kesi imemalizika takribani wiki moja iliyopita na mahakama imemwamuru huyo rafiki yangu amlipe deni lake huyo mdai la Tshs 6,500,000.

Amepewa siku 30 kama haridhiki na uamuzi huo akate rufaa mahakama ya wilaya

Tumemshauri aachane na rufaa na alipe tu deni hilo kuepuka usumbufu na gharama zingine.

Ndugu mwanasheria, baada ya hukumu ni nini anachotakiwa kufanya au kuomba mdaiwa kwa mahakama ili kumpa unafuu was kulipa kuepuka shida kubwa zaidi mbeleni?

Nauliza hivi kwa sbb lengo kweli ni kulipa. Lakini hana uwezo wa kulipa kwa mkupuo hiyo milioni 6,500,000 bali anataka aiombe mahakama alipe kwa awamu tatu kila baada ya mwezi mmoja mmoja.

Je, asubiri hizo siku 30 kisha aende mahakamani aiombe mahakama alipe deni kwa awamu tatu? Au aende kabla siku 30 hazishaisha kuomba huo utaratibu?

Ni upi utaratibu tafadhari kisheria?
 
Back
Top Bottom