Mwendokasi mna mambo ya kuudhi

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
10,596
2,000
Imagine Kimara Mwisho asubuhi abiria wanaoenda Kivukoni na Gerezani mistari ni mirefu hadi inafika sehemu inaingiliana (overlapping) na hivyo waendaji wa Kivukoni wanakuwa wanagombania gari na wanaoenda Gerezani.

Hii imepelekea mama mmoja jana kusukumwa na kuzama mguu katikati gari na ngazi.

Kwanini wasipange ruti ya MOROCCO na KIVUKONI wakae sehemu moja na GEREZANI wakapandie wanapopandia wa Morocco kwa sasa?? Hawa hawaingiliani ruti hivyo hawawezi kugombea gari.

Ishu ya pili ni KIVUKONI.

Unakuta mtu umeingia ndani ya stend tiketi ya 650 umeacha mlangoni, ile umeingia ndani unakuta magari ya Mbezi yapo na abiria sio wengi, ila Kimara mstari ni mrefu sana. Ukiamua kukata titeti ya 400 pale ndani ya stend, wanakuzuia kwenye mlango wa Gari eti lazima uwe na ya 650.

Swali la lijuiliza nani anaweza kuingia stend ya mwendokasi bila kuwa alikata ya tiketi ya 650?, na je, zile tiketi za 400 zinazouzwa ndani ya kituo ni za nini?

Sioni ulazima wa tiketi mbili wakati naingia kwenye gari ya Mbezi kama nina ya 400 mpya haijachanwa.

Hili halihitaji hata certificate ya "the amazon college "
 

Baraja

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
1,254
2,000
Jana mzee alisema kuna mabasi 40 yameshakufa. Sasa najiuliza, yale mabasi yamekufaje ilihali yanatembea kwenye barabara yake!!!! Kuhusiana na ajali, sina hakika hata 10 yanafika yaliyopata ajali kiasi ya kutoweza kurekebishika.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
35,116
2,000
Biashara ya ku manage mabasi katika mazingira yenye abiria wengi namna ile yani wamemonopolize route halafu wanashindwaku manage haieleweki yani
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,067
2,000
Tukubali kuwa serikali yetu inazembea sana kwa sababu ya kupeana ajira kikabila.

Fuatilieni mtajua ni akina nani wejaza a mle.

Ni wazalendo feki tupu. CCM imeajiri watu kikada na kikabila na pia ilipata wabunge kwa wizi wa kura. Sasa unategemea nini kutoka kwa Mwizi kama sio wizi.

Watu wengi wenge umri wa miaka 30 + walioko kwenye ajira mbali mbali ni zao la wizi wa mitihani Sekondari. Wasomi wengi wa Vyuo vikuu vya ndani ni zao la digiri za madesa na kwa wale wa jinsia ya Ke ni zao la digirii za sura zao badala ya akili kichwani.

Kwa hiyo bila kuweka mifumo na katiba kali ya kuwachuja sana wasimamizi ili kupata watu wanunifu hakika tunajidanganya kwa kuwategemea hao waliotokana na wizi kwenye Elimu,wizi kwenye kura , wizi kwenye rasilmali fedha za umma n.k.

Tusimtwishe mama Samia mzigo mzito bure. Tumwache naye afanye anavyoona inafaa ili kuijenga familia yake kimaisha na Eneo analotoka kama wenzake. Akiamua kuwafunga watu midomo wasifurukute na kukosoa sawa tu mana mwezake naye alifanya alivyotaka na akajitangaza mzalendo namba moja duniani.
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,067
2,000
Hawezi kufanya mambo yoote peke yake bila kuoneshwa au wasaidizi wake kuoneshwa uzembe ulipo

Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app


Utaonyeshwa na nani kama unazuia watu kusema na kuandika?

Hivi nani atasema wakati kila idara wamejazana ndugu wa sehemu moja ? Wakikutana wanabonga kilugha na kumsifia aliyewapa mkate huku wakiambizana kuwa wajitahidi wajenge tubanda tuwili tutatu kabla ya msimu kuisha mana nafasi hizo watazijutia?

Hakuna nchi inayoweza kujengwa na mtu mmoja katika ulimwengu wa sasa uliojaa wataalam na watu wenye maarifa makubwa kabisa.

Serikali ijenge mifumo inayochochea uadilifu kwa nguvu zote. Kizazi kijacho hakitaweza kuvumilia Ubadhirifu wa wachache kujinufaisha bila kuchukuliwa hatua eti kwa hofu ya kuua chama . Nguzo kuu ya Ubadhirifu na kulindana na CCM na hofu ya kushindwa.

Wakurugenzi walivuruga uchaguzi chini ya Jeshi la Polisi sasa sijui ni mbunge gani aliyepewa ubunge mezani anaweza kuijadili Ripoti ya CAG wakati serikali nduyo iliyompa Ubunge na sio wananchi.!!!

Ukitaka kupata Taarifa weka hata wale wanaokukosoa kwa nia njema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom