Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,832
- 2,790
Kila kona sasa hivi hapa Dar es Salaam ukikutana na mtu ukagusia milipuko ya bomu Arusha hakika wengi wanailaani CCM na UCHAFU WAKE wa tangu enzi na enzi!! Kitu cha kujiuliza ni kwamba bado CCM wanadhani wananchi bado ni mbumbumbu wa siasa kama enzi za TANU na ASP. Yale anayoongea Nape hakika amekishushia hadhi Chama cha CCM.
Nimekutana na Askari mmoja wa FFU nikamtania japo simfahamu kabisa nikamwambia "Wazee sasa hivi mko enzi za ukoloni Afrika Kusini, alinielewa nilichokuwa nataka kugusia. Jibu lake likawa hivi. "Ndg yangu yote hayo ni matokeo ya hofu ya kunyang'anywa madaraka. Hawa wakubwa wanahofia kwamba ikiwa Chadema kitachukua nchi wao wataishia kushitakiwa hivyo wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanabaki madarakani, sisi tunatumwa kutekeleza mambo yao. Akasema ukiangalia ya Mwangosi na sasa hivi huko Arusha huwezi shangaa. Mlipuaji analiwa fedha nyingi ukiangalia hata donge nono walilotangaza la milioni mia moja ni danganya toto kwani wanajua watapindisha ushahidi.
Sasa kutokana na mambo kadhaa ambayo Polisi wamehusika tunategemea busara za IGP Said Mwema ajitathimini kama anafaa katika nafasi hiyo. Tulichokichoka ni zile tambwe za tutahakikisha tunawakamata watuhumiwa kokote waliko hata ndani na nje ya Tanzania, haya sasa tumeyachoka. Tumeyachoka kwasababu raia amegeuka ni bidhaa ya kugombewa na wanasiasa na mwanasiasa akizidia bidhaa inamwagwa chini yaani kuuawa.
Mr IGP I don't think we need you anymore, could you please step aside???