Mwema mambo kama haya ndiyo watu huamua yale ya Kyela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwema mambo kama haya ndiyo watu huamua yale ya Kyela

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Jul 18, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Utata watawala mauaji ya mfanyabiashara na kauli za polisi[​IMG]Na Mwandishi Wetu

  WAFANYABIASHARA wa Moshi wanaoishi jijini Mwanza, wamehoji ukweli wa kauli ya Polisi kuwa inawasaka wafanyabiashara watatu matajiri wakati watu hao wanaendelea na shughuli zao jijini Mwanza.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alikaririwa akiwaomba wananchi wenye taarifa za mahali walipo wafanyabiashara hao waziwasilishe kwa siri polisi ili waweze kuunganishwa na kesi ya mauaji namba PI 9/2009.

  Lakini wafanyabiashara hao waliliambia Mwananchi Jumapili hivi karibuni kuwa watuhumiwa wapo, lakini wanapowaeleza polisi taarifa hizo, hujibiwa kuwa ‘walishamalizana’ na polisi Kilimanjaro.

  Wafanyabiashara hao wanamiliki vitega uchumi kadhaa jijini humo likiwemo jengo la ghorofa lenye maduka makubwa zaidi ya 20, duka kubwa la vifaa vya ujenzi na ghala la kuhifadhia magari yanayoaigizwa toka Dubai .

  “Hawa watu wapo hapa Mwanza, ebu muulizeni huyo RPC, anaposema anawatafuta anawatafutaje? Mbona tukiwauliza polisi hapa wanasema hizo habari wanazisoma tu kwenye magazeti?,” walihoji wafanyabiashara hao.

  Wafanyabiashara hao wanadaiwa kumpigia simu meneja wa baa ya Mo-Town, James John Massawe wakimweleza kuwa kaka yake amekufa kwa ajali na alipokwenda eneo walilomuitia, walimteka nyara na kwenda kumuua.

  Habari zinadai kuwa sababu za kufanya hivyo ilikuwa ni kulipiza kisasi kwa kile kinachodaiwa kuwa marehemu alihusika na mauaji ya mama wa wafanyabiashara hao alitajwa kwa jina la Martha Kisoka anayedaiwa kuuawa Mei mwaka huu.

  Kamanda wa Polisi jijini Mwanza, Jamal Rwambo alipoulizwa jana iwapo amepokea ombi lolote kutoka polisi mkoa wa Kilimanjaro la kuwakamata wafanyabiashara hao, alisema wanashirikiana vyema na wenzao wa Kilimanjaro.

  Hata hivyo, alikataa kueleza kwa undani iwapo ni kweli wamepokea taarifa za kusakwa kwa wafanyabiashara hao, zaidi ya kusisitiza kuwa kama wanatafutwa basi watakamatwa tu na kurejeshwa Kilimanjaro wanakotakiwa.

  Ndugu wa marehemu wanamnyooshea kidole kamanda Ng’hoboko kuwa anawakingia kifua wafanyabiashara hao kutokana na ‘fadhila’ aliyoipata kutoka kwao wakati akiwa Mkuu wa upelelezi (RCO) mkoa wa Mwanza.

  Hata hivyo Kamanda Ng’hoboko amekaririwa akikanusha vikali kuwakingia kifua wafanyabiashara hao na kusema hakuna mtu yoyote mwenye haki ya kujichukulia sheria mkononi na kuchukua uhai wa mtu mwingine hata kama ni kulipiza kisasi.

  Wasiwasi dhidi ya Kamanda Ng’hoboko ulianza kujengeka baada ya kutoa taarifa kwa waandishi wa habari kuwa marehemu aliuawa na wananchi wenye hasira huko Kindi Kibosho, taarifa iliyokanushwa na wananchi.

  Mkuu wa wilaya ya Moshi, Alhaji Mussa Samizi alikaririwa akisema taarifa iliyokusanywa na maofisa usalama wa Taifa ilithibitisha kuwa marehemu hakuuawa na wananchi wenye hasira bali waliomuua ni ndugu wa familia moja.
  Tayari watuhumiwa wawili, John Mallya maarufu kama 'Small boy" na Idrissa Munisi wamekwishafikishwa mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi, Lugano Kasebele na wafanyabiashara hao watatu wanatakiwa kuunganishwa na kesi hiyo.
  Tuma maoni kwa Mhariri
   
Loading...