Mwelekeo wa Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Wazua Kiwewe CCM

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,217
Yanayojitokeza kila mahali hapa nchini kuelekea uchaguzi mdogo wa Madiwani jumapili hii umezua kiwewe kikubwa kwa viongozi, wanachama na wapenzi wa ccm (mpaka humu JF) kwa hofu ya kushindwa kwa aibu.
Hali katika kampeni za uchaguzi huo inaonyesha wazi wagombea wa ccm hawana mvuto tena na watu hawana habari nao kiasi cha kufanya hata hao wahamasishaji wao kutoa taarifa huko juu kuwa hali ni tete.
Wapo viongozi ndani ya ccm wamekubali yaishe kwa kusema Mwenyekiti ndio katuponza, kwa vile haambiliki basi acha aibu aipate yeye. Hadaa za kuwa chama kimeboresha maisha ya watu kwa kipindi hiki cha miaka miwili hazijakubali kwa wananchi na wamezibeza kuwa wanataka kufanywa wajinga.
Sasa zimebaki propaganda za watu eti wanakimbia Chadema na magazeti yamewekwa sawa kulijengea hoja hilo ila wananchi wameona magazeti sio shibe yao lazima wakishikishe adabu chama cha mapinduzi. Imefika wakati hadi wananchi wa Dar kama vile hawana akili wanadanganywa eti zile huduma za meli ya Tiba ya China ni juhudi binafsi za Makonda na Magu! Eti hata gharama zimelipiwa na Magu kwa vile anajali afya za raia? Hata aibu hakuna kwa uongo wa kitoto?
CCM IANDIKE IMEUMIA UCHAGUZI WA MADIWANI, vinginevyo wacheze rafu lakini watu wataelewa nini kimetokea.
 
ee790075772beeb72eeaaac185d6b3ee.jpg

Hali kama hii mzee Sizonje ataacha kupata kiwewe?
79740d80f43616a144398e8f5e235024.jpg

Na mtindo huu watu wameushtukia. Hawataki kufanywa kokoto tena
 
Kwa sasa kete yao ni kuwa watu wanaondoka na kujiunga na ccm. Lakini bado hawajiulizi mbona wapiga kura wanawakimbia kwa maelfu kama hapo juu?
bae306086be6dbb53971d24fd8083545.jpg
 
Kama bado mnaamini kuwa mtakishinda chama tawala kwa wingi wa wananchi wanaohudhuria mikutano yenu ya kampeni basi mna safari ndefu ya kushika dola. Jiandaeni tu kulalamika kuwa mmechakachuliwa.
 
Wafanyeje sasa! Maana kwa uhalisia kura ndio ushindi halisi vinginevyo ni wizi mtupu
 
Kwa sasa kete yao ni kuwa watu wanaondoka na kujiunga na ccm. Lakini bado hawajiulizi mbona wapiga kura wanawakimbia kwa maelfu kama hapo juu?
bae306086be6dbb53971d24fd8083545.jpg
harafu huyo polepole aambiwe wakati wa kupiga picha awe anatabasamu tu sio kukenua mimeno
 
Back
Top Bottom