Mwelekeo wa siasa ya Tanzania ni hatari kwa siku za usoni kama haitabadilika

Herbert Nkuluzi

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
2,430
2,436
Ndugu zangu Watanzania kwa sasa taifa letu linajiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu lakini dalili za amani ya taifa hili kupotea zinaanza kunukia hebu tujiulize haya:-

1.Kama Lipumba na Dr.Slaa wamenunuliwa na CCM kwa lengo la kumchafua na kumwonesha LOWASA kwamba hafai
km inavyosemwa mtaani,hao ccm hawatatumia hata jeshi ili kudhibiti kile kinachoonekana kufeli baada ya wao kutumia pesa kuwalaghai Dr.Slaa na Lipumba?

2.Kwa nini ccm hawataki kujenga siasa safi(za kutomjadili mtu zaidi) jambo ambalo taratibu linawaamshia watu hisia kwamba wanataka kubaki madarakani kwa faida zao binafsi na co za watanzania hali inayowafanya kuwa ktk sintofahamu japo wao ndo wapga kura?

MIMI BINAFSI NAAMINI SOTE(WATANZANIA) TUNA JUKUMU LA KUWATAZAMA KWA MAKINI VIONGOZI WENYE MWELEKEO WA KUVUNJA AMANI YA TAIFA NA KUTOWAUNGA MKONI ILI KURA YETU IAMUE NANI ATAKUWA RAISI WETU WA 5

TUKUMBUKE:
Mithali 18:18"Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu".
 
Back
Top Bottom