Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,021
- 2,478
- Thread starter
- #81
Nakujibu kwa ufupi kama ifuatavyo:Hoja yako namba 4 naipinga;
Chadema iko Mbeya, Tarime, Nkasi- Kaskazini lakini bado kuna watu mnakuja na propaganda ya ukanda mpaka leo?!
Udini; sijui ni kigezo gani kimetumika kuhalalisha hii hoja yako, umewahesabu walutheri walioko Chadema ukaona idadi yao inazidi madhehebu mengine au dini nyingine? au umeangalia juu juu kwa baadhi ya viongozi ndio ukaja na hii hoja yako?
Usiasa-biashara; hii nayo ni hoja dhaifu, nadhani kwa hii dunia tunayoishi kwa sasa huwezi kulikwepa hili, sisi sio wajamaa tena, na huu mfumo umewekwa na CCM wenyewe, na wapo viongozi wengi wa CCM wanaofanya biashara kwa kificho, midomoni wanajiita wazalendo lakini kiuhalisia hawana lolote, hivyo hapa napo kuilaumu Chadema haiwezi kuendesha nchi kwasababu haya ni maoni yako binafsi yasiyo na uhalisia wowote.
Umeandika: Chadema iko Mbeya, Tarime, Nkasi- Kaskazini lakini bado kuna watu mnakuja na propaganda ya ukanda mpaka leo?!
Najibu: Kitu kinachoitwa KAMATI NDOGO YA KAMATI KUU (KNKK) ndicho hapa nimeitwa CHADEMA DEFENSE MASTERS. Hutaona Rules of Procedures zake na hutajua anazitunga nani, hutajua ziko wapi, lakini zipo. Kama wewe sio kutoka "majuu" huwezi kuingia humo. Na ujue KNKK ina nguvu kuliko Katibu Mkuu, kuliko KK, kuliko BK na kuliko MM. Dr. Mashinji ameng'olewa na KNKK. Fanya utafiti ndugu yangu. KNKK "imechinja" wengi.
Umeandika: Udini; sijui ni kigezo gani kimetumika kuhalalisha hii hoja yako, umewahesabu walutheri walioko Chadema ukaona idadi yao inazidi madhehebu mengine au dini nyingine? au umeangalia juu juu kwa baadhi ya viongozi ndio ukaja na hii hoja yako?
Najibu: Tatizo lilianza miaka ya 2000 pale kijana aitwaye MAXX alipotambulisha Dr. Bagonza kwa Dr. Slaa kama mtu mwenye mapenzi mema na Chadema. Bagonza akatumia jigger principle (kanuni ya funza)--Maafisa Usalama wanaijua zaidi! Akapenya mpaka jikoni Chadema. Ghafla nafasi ya Dr. Slaa ikachukuliwa na akapewa Lowassa. Ghafla nafasi ya Mwenyekiti ikachukuliwa na Bagonza. Mwenyekiti akabaki ni ceremonial mpaka leo. Maamuzi mengi ya Chadema yanafanyika chini ya uratibu wa Bagonza. Ana veto juu ya Wagombea ubunge na urais. Takwimu za wagimbea ubunge mwaka 2015 na 2010 hujaziona. Asilimia kubwa ni walutheri. Kwa ujumla, Bagonza anatumia Chadema kutanua ulutheri. Huu ni udini wa kisayansi. Leo hii Mbowe anatoa maagizo kwa wasaidizi wake, lakini Bagonza anawambia wasaidizi wasiyatekeleze, na Mbowe ananyoosha mikono. Mbowe is a ceremonia Chairperson! Fanya utafiti wako.
Umeandika: Usiasa-biashara; hii nayo ni hoja dhaifu, nadhani kwa hii dunia tunayoishi kwa sasa huwezi kulikwepa hili, sisi sio wajamaa tena, na huu mfumo umewekwa na CCM wenyewe, na wapo viongozi wengi wa CCM wanaofanya biashara kwa kificho, midomoni wanajiita wazalendo lakini kiuhalisia hawana lolote, hivyo hapa napo kuilaumu Chadema haiwezi kuendesha nchi kwasababu haya ni maoni yako binafsi yasiyo na uhalisia wowote.
Najibu: Hoja ya Usiasa-biashara ninayoiongelea mie sio hiyo. Lengo kuu la siasa za dola sio kutafuta faida ya kibiashara. Ni kukuza na kuhami maslahi ya pamoja katika taifa. Kanuni ni maslahi ya pamoja kwanza, faida binafsi baadaye. Lakini seleka za kisiasa ndani ya Chadema zinapindua mizania hiyo. Kanuni yao ni faida binafsi kwanza, maslahi ya taifa baadaye. Hii ndiyo miwani inayotumika kuchuja nani ni insider na yupi outsider. Yeyote anayepingana na kanuni ya "Faida binafsi kwanza, maslahi ya taifa baadaye" anapaswa kuundiwa zengwe na kuondolewa. Hujawahi kujiuliza ni kwanini kina Suzan Lymo wako pale CDM HQ kama mzimu wa ukoo? Wanawekeza kwenye siasa ili kutafuta faida binafsi. Hivyo ndivyo miradi ya helikopta za Ndesapesa na Mafuso ya Chadema ilivyotekelezwa. Hawa Chadema Defense Masters wana utayari wa kubeba risk kubwa, na wakifanikiwa wanapata riba kubwa. Unaweza kukuta 50% ya ruzuku na michango ya chama unarudi kwao. Wabunge juzi walikuwa wanapiga kelele bila kupata majibu sahihi juu ya wapi zimekwenda ruzuku zao. Mawakala wa chama mwaka 2015 na 2020 hawakupata uwezeshaji wakati fedha zimetafuta. Nadhani hata wewe unashangaa mabilioni ya Lowassa yalikwenda wapi hadi mawakala washinde njaa vituoni. Lakini mifereji ya fedha hizi zote ndiyo hiyo inaelekea Kaskazini.
Umeandika: Chadema kusema wataweka rehani madini kwa ajili ya mikopo; hili naona CCM mmeamua kulielezea mnavyopenda nyie, kiuhalisia, haya madini yetu hata leo hii mmeyaweka rehani siku nyingi sana kwa kumnufaisha mzungu wakati ndugu zetu maeneo ya uchimbaji bado wamezungukwa na umasikini wa kutisha, mikataba mliyosaini nao ni ya kinyonyaji, mmekula 10% hamuwakumbuki tena masikini wa nchi hii. Sasa kama Chadema wao watakuja na mbinu nzuri zaidi itayomsaidia mtanzania kupata chochote toka kwenye madini waliyopewa na Mungu kwangu naona nafuu, kuliko madini kuishia kwa mzungu na sisi tunabaki na mashimo tu kwa sababu ya sera mbovu za serikali ya CCM.
Najibu: Sikubaliani na maelezo yako. Kwanza, two wrongs dont make a right. Pili, ukiwa na redio ukaiweka rehani ili mtoto wako alipiwe karo, kabla ya kulipa deni huwezi kusikiliza taarifa ya habari. Ukishindwa kulipa deni redio inachukuliwa. Hivyo, kuweka rehani madini yaliyo ardhini ni sawa na jaribio la kuuza nchi. Kiusalama, sera ya kuweka madini rehani ni blunder kuu iliyofanywa na waandishi wa Ilani ya Chadema. Usiwatetee.
Nimemaliza.