CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
Na Thadei Ole Mushi
Kwa Muda Mfupi niliowapima viongozi wapya wa Chadema hasa Katibu Mkuu na wenyeviti wa Kanda mbalimbali nimeona mambo makuu yafuayayo. Pamoja wingi wa press ila anaongea vitu vyepesi sana. Jana nimemsikia akisema sijui CCM inaogopa Rangi nyekundu na blah blah kibao.
1. Katibu Mkuu anafanya press nyingi mno ambazo hazina maana. Matokeo yake anayoyazungumza hayawi viral wala hayabadili mwelekeo wa kisiasa ambao upo.
2. Anakitoa Chama Kwenye mikakati na mipango anakirudisha chama Kwenye harakati. Kila akizungumza analalamika haonyeshi Mipango yaani Plan B ya alipokikuta chama ni wapi.
3. Mkakati wa wenyeviti wa kanda kuitisha press una maana nimevutiwa zaidi na press ya kanda ya Ziwa ya Wenje. At least unasikia hoja ndani yake. Press kama zile zenye hoja, data, na facts ni Sumu kwa CCM na Dola yake. Lakini press za kukitishia CCM hazikuwahi kufanikiwa kamwe kwa kuwa ndani ya CCM kuna mifumo yenye Misuli kuliko Chadema. Nimemsikiliza mfano Nyalandu anaongea utafikiri anaoga njee hakuna lolote LA Msingi analoliongelea. Kuitisha press imekuwa fashion watu wameanza kuzoea.
4. Nilitarajia Katibu Mkuu aje na mkakati mkubwa wa Katiba na tume huru maana Chadema ndio waathirika wakuu wa mambo hayo mawili. Matokeo yake namuona akivishwa uchifu huko mwanza nk.
5. Nilidhani viongozi hawa watajikita kufanya Assessment ya majimbo yote wanayoongoza kujua ni mangapi wanayoweza kuyalinda. Kuna hatari kubwa upinzani ukapoteza majimbo mengi 2020. Je ni majimbo gani ambayo wataweza kuyalinda? Ni majimbo gani ambayo CCM wanayawinda? Mbinu za kuyalinda ni zipi nk haya ndiyo mambo ya msingi ya kujadili. Naona wametoka mapema sana baada ya kuchaguliwa.
6. Nilidhani ni wakati muafaka wa kuanza kuscreen vijana wapya ambao watagombea maneneo mbalimbali. Ndani ya wabunge walionao kuna waliochoka na ambao hawataweza tena kugombea je eneo hili Katibu mkuu kajipangaje?
CCM sio wepesi kama Mnyika anavyofikiria, na kakabidhiwa chama katika wakati mgumu haswa ambao unahitaji akili kubwa na ya ziada. Namuona kama iliyopo mbele yake hajaijua kwa kiasi kikubwa. Hata ni baadhi ya maeneo tu kati ya maeneo Mengi ya kimkakati nineonyesha.
Siasa za harakati zimeshapitwa na wakati Tanzania. Karibuni jalalani