Mwekezaji wa madini ya mchanga anavyosumbuliwa Kigamboni

Hodar

Member
Oct 27, 2018
16
8
Kampuni hii ya JACANA/Strandline Resources, imeshakopa hela benki ya kuwalipa wenye maeneo pale Mwasonga pamoja na kuendeshea mradi huo.

Walishakubaliana na wananchi kwamba wanakodi yale maeneo kwa miaka minane, baada ya mradi wao kwisha, watarudisha hayo maeneo kwa wenyewe.

Katika kipindi hicho cha miaka 8 watakuwa wanawalipa hawa wenye maeneo hela kiasi fulani ambacho kimekokotolewa kwa kuzingatia mita za mraba alizonazo mtu, hela hiyo itakuwa inalipwa kila baada ya miezi mitatu. Kampuni hii imeshachukua taarifa za wananchi wote na mali zao, na wako tayari kuwalipa watu ili waanze mradi wao.

Cha ajabu, baada ya kufikia hatua hiyo, viongozi fulani wa wilaya ya Kigamboni wanalazimisha kwamba wanataka halmashauri ya wilaya ya Kigamboni ndiyo ichukue yale maeneo, iwalipe wananchi waondoke ili sasa wao ndo waendelee na hiyo kampuni.

Option nyingine ni kwamba kampuni hiyo inunue kabisa hayo maeneo halafu baada ya mradi ikabidhi hilo eneo la mradi kwenye halmashauri ya wilaya na sio kwa wananchi.

Hii kampuni imeshaelewana na benki kwamba itakuwa inapewa hiyo hela kila baada ya miezi mitatu, sasa hiyo hela ya kuwalipa wananchi mara moja wataitoa wapi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli anasema mara kwa mara kwamba wawekezaji wasisumbuliwe lakini baadhi ya watendaji hawajali.

Naomba mawaziri wanaohusika na uwekezaji, madini, na TAMISEMI wamsaidie Rais katika hili ili wananchi wapate haki yao, na kampuni isibughudhiwe.



Ndimi Raia Mwema.
 
Wasubiri kutumbuliwa tu hao viongozi wanaokwamisha huo mradi huko mwasonga kigamboni na...

Mheshimiwa Magufuri
 
Back
Top Bottom