Mwekezaji mwenza anahitajika: Pata Faida ya Laki 5 kila mwezi

Mshimba1971

Member
Dec 13, 2021
75
66
Wadau,

Niko kwenye hatua ya mwisho za kuanza mradi wa biashara ya Mboga Mboga, hii ni baada ya kufanya utafiti na majaribio kwa muda wa miezi 6 na kuwa na uhakika wa uwepo wa soko la Mboga Mboga( kwa jumla) katika eneo la Bunju B, Dar es salaam.

Naitafuta mwekezaje mwenza(Partner) atakaewekeza Tshs. 800,000 (kwaajili ya kununulia Pampu ya kumwagilia shamba na mipira ya umwagiliaji ya mita 100), na atapata gawiwo la Tshs. 500,000 kila mwezi kwa muda wa miezi 4 mfululizo(faida ya jumla kwa miezi 4 ni Tshs. 2,000,000/=). Mashine/Pampu ya umwagiriaji na mipira atakayonunua mwekezaji mwenza, itakua bado mali ya muwekezaji na anaweza ichukua baada ya mradi kuisha au msimu wa mboga mboga kuisha (miezi 4 kuanzia sasa) au kuniuzia vifaa hivyo.

Mchaganuo:
Eneo la kilimo: Shamba liko maeneno ya Bunju B, Dar es salaam.

Soko: Soko la kuuzia mboga mboga ni kina mama wanaokuja shambani na kununua kwa jumla na wao kuuza rejareja(kwenye soko la Bunju B au kwenye nyumba za wati binafsi)

Chanzo cha Maji: Kuna chanzo cha uhakika cha maji(bwawa) lililoko Mita 230 kutoka shambani).

Mchanganuo wa Mapato gafi kwa mwezi: Shamba limetoa idadi ya matuta 30 ya mboga mboga, na tunauza kwa bei ya jumla shmabani ya Tshs. 50,000 kwa kila tuta (Tshs. 50,000 x 30 = Tshs. 1,500,000 )

Gharama za uendeshaji: Tshs. 500,000 kwa mwezi(mafuta ya kuendesha pampu ya umwagiliaji na gharama zingine).

Uwekezaji niliofanya tayari(au mchango wangu kwenye mradi)
  • Shamba (limeshasafifya na kungolewa visiki)
  • Nimeajiri vijana wawili wa kufanya kazi muda wote kwanye mradi
  • Nimetoa Nyumba na Chakula kwajiri ya vijana wa kazi
  • Usimamizi wa mradi kila siku (naishi hatua 5 kutoka shambani)
  • Gari la kubebea mbolea na maitaji ya shamba
  • Mbegu na mbole ya kupandia na madawa
Mwekezaji mwenza anaeitajika:

Naitaji mwekezaji mwenza mwenye nia ya dhati ya kilimo, atakaechangia Tshs.800,000 kwa makubaliano ya kupata gawiwo la Tshs. 500,000 kwa mwezi, kwa kipindi cha miezi 4. Baada ya miezi 4 tutajadiliana kuwekeza pamoja katika kilimo cha nyanya tutakazouza mwezi wa 8. Hii ni fursa ya uhakika.

Piga simu namba 0754 34 36 42, kwa mazungumzo na kuja kuliona shamba.

NB: MUWEKEZAJI ANAWEZA KUWEKEZA HELA AU AKATOA VIFAA VINAVYOITAJIKA.
 
Mr. Kulwa 1981,umejaribu kufafanua lakini naona kuna vitu haviko sawa labda jazia nyama vzuri.mfano utamlipa mwekezaji @500,000/=kwa mwezi ikiwa umeandaa vizimba 30 na kila kizimba utauza kwa @50,000/=30*50,000=1,500,000/=umlipe mwekezaji yake @500,000/= alafu gharama za uendeshaji @ kama'nukuu' 500,000/= umeajiri vijana wawili unawalipaje?mbolea unanunua kiasi gani?na vizimba ulivyo viandaa ni 30 hauoni bado inakuwa ngumu kumshawishi mtu awe ubia na wewe pia mboga mboga zinakuwa baada ya siku ngapi?kuvuna?(tukilenga mwezi tena).
 
Hapa kuna harufu ya kupigwa. Haingii akilini hata kidogo mwekezaji mwenza umlipe laki 5 kila mwenzi.
 
Mr.kulwa 1981,umejaribu kufafanua lakini naona kuna vitu haviko sawa labda jazia nyama vzuri.mfano utamlipa mwekezaji @500,000/=kwa mwezi ikiwa umeandaa vizimba 30 na kila kizimba utauza kwa @50,000/=30*50,000=1,500,000/=umlipe mwekezaji yake @500,000/= alafu gharama za uendeshaji @ kama'nukuu' 500,000/= umeajiri vijana wawili unawalipaje?mbolea unanunua kiasi gani?na vizimba ulivyo viandaa ni 30 hauoni bado inakuwa ngumu kumshawishi mtu awe ubia na wewe pia mboga mboga zinakuwa baada ya siku ngapi?kuvuna?(tukilenga mwezi tena).
Ahsante kwa maswali. Ni wazi mimi nimeweka uwekezaji mkubwa zaidi, nashauri kama una nia njoo tuzungumze ikiwaa kilakitu na utajua inawezekana. Mboga tunazolima zinakomaa ndani ya siku 21 mpaka 28. Kwaana hiyo kila mwezi tunavuna. Vijana nawalipa kutoka vyanzo vingine kwani pia wanaangalia mifugo(ngombe wa maziwa)
 
Hivi hamjawahi kuona uzi kama huu?

Nafikiri kuna member akasema si ukakope benki ili faida iwe yako peke yako?
Ahsante Mkuu kwa mawazo. Ni mara ya kwanza kuweka bandiko hili, bank ni wazo pia, ila nazani unajua milolongo ya bank kwa watu wasio sekita rasimi, itachukua miezi 3 kupata mkopo. Kipindi cha mwezi wa kwanza mapaka wa 4 ndio kuna soko kubwa la mboga mboga,suala la muda ni muhimu sana.
 
Ahsante kwa maswali. Ni wazi mimi nimeweka uwekezaji mkubwa zaidi, nashauri kama una nia njoo tuzungumze ikiwaa kilakitu na utajua inawezekana. Mboga tunazolima zinakomaa ndani ya siku 21 mpaka 28. Kwaana hiyo kila mwezi tunavuna.
Mmi ninapenda sna kuona vijana wenzagu mnapambana ila ukifikiria jambo ukaona linawezekana usikurupuke.kwanza fanya research iliyokamilika alafu unapo kuja kutafuta mtu maelezo yako yanakuwa yameshiba.alafu ujue kunawatu wana hela ila hawajui wawekeze wapi?wapate hela,na kuna watu hawana hela ila wanavitu vilivyo simama vzuri sna.tutumie jukwaa hili kwa mapana sna .kutokana na maelezo yako embu tulia kwanza alafu tafakar kidogo utaelewa nasema nini?.kingine ukiangalia umesema unavuna baada ya siku 28 ndg hapa 'waza kidogo'maana unaweza ukavuna ata wiki nzima au ukavuna siku 2 -mtu akiwa na kiu ya maji usimpe maji ya moto.kingine chakukusaidia embu jazia Nyama MAELEZO yako,idia yako nzuri ila boresha usivunjike moyo
 
Mawazo yako Mkuu ni mema. Nimefanya research kwa miezi 6(kwa kulima sehemu ndogo) na kwa uwekezaji wangu binafsi, naitaji partner wa kupanua shamba(kama umeelewa maelezo yangu) kwahiyo na uhakika na nachokiandika. Mwenye nia hasa atakuja shambani na kuuliza maswali yote, kama nia haipo hata niandike pages 200 bado maswali yatakuwepo tu. Karibu sana shambani tuwekeze mkuu
 
Niliona niseme jambo kupitia idia yako kuna mtu inaweza kumsaidia.pia umesema faida ya jumla una maanisha nni?moja hiyo @2,000,000/=kama faida + hela aliyo wekeza au ni julma pamoja na hela aliyo wekeza na kama ndo hivi inamaana mwekezaji atavuna 1,200,000/=kwa mda huo.sijui kama umenipata hapo.kwamsaada kwa MWENYE uhitaji pia
 
Mboga inalipa me nafanyia mkoa mwingine ila soko letu kubwa lipo Dar , mboga inalipa sana hasa kuanzia Dec , Jan- Apr baada ya hapo piga majani ya maboga msimu wa kiangazi huwa adimu sana !!!
 
KAMA VIZIMBA 30 UNAPATA FAIDA YA 1.5M KWA MWEZI, KWANINI UTAFUTE MWEKEZAJI MWENZA WA KUWEKA 800,000/= ILHALI UNAWEZA KUIPATA PESA HII NDANI YA MWEZI MMOJA KUTOKA FAIDA YA MAUZO YAKO?

Aquila non capit muscas!
 
KAMA VIZIMBA 30 UNAPATA FAIDA YA 1.5M KWA MWEZI, KWANINI UTAFUTE MWEKEZAJI MWENZA WA KUWEKA 800,000/= ILHALI UNAWEZA KUIPATA PESA HII NDANI YA MWEZI MMOJA KUTOKA FAIDA YA MAUZO YAKO???

Aquila non capit muscas!
Yuko sawa amesema kwa ajiri ya kununua pump ya maji + mipira yakuvutia maji hiyo siyo kesi.yye alitakiwa ajazie nyama maelezo yake mfano mtu kawekeza 800,000/=lakini atapata 500,000/=kila mwezi sawa je?anapo sema miezi 4 mfurulizo atapata 2,000,000/= swali kwahiyo aliye wekeza hata pata 500,000/= bali ni 300,000/=kwa maana jumla utapata 2,000,000/= ukitoa hela uliyo wekeza utapata 1,200,000/= maana haja ongelea 2,000,000+ 800,000= ?ndo nilikuwa namshauri atulie kwanza alafu aje kwa mapana ila hakuelewa.ndg njoo bado tunataka kuboresha wapate faida wengi kwa wazo lako usipo faidika wewe watafaidika wengine watakao soma baadae.
 
Mmi ninapenda sna kuona vijana wenzagu mnapambana ila ukifikiria jambo ukaona linawezekana usikurupuke.kwanza fanya research iliyokamilika alafu unapo kuja kutafuta mtu maelezo yako yanakuwa yameshiba.alafu ujue kunawatu wana hela ila hawajui wawekeze wapi?wapate hela,na kuna watu hawana hela ila wanavitu vilivyo simama vzuri sna.tutumie jukwaa hili kwa mapana sna .kutokana na maelezo yako embu tulia kwanza alafu tafakar kidogo utaelewa nasema nini?.kingine ukiangalia umesema unavuna baada ya siku 28 ndg hapa 'waza kidogo'maana unaweza ukavuna ata wiki nzima au ukavuna siku 2 -mtu akiwa na kiu ya maji usimpe maji ya moto.kingine chakukusaidia embu jazia Nyama MAELEZO yako,idia yako nzuri ila boresha usivunjike moyo
Mawazo yako Mkuu ni mema. Nimefanya research kwa miezi 6(kwa kulima sehemu ndogo) na kwa uwekezaji wangu binafsi, naitaji partner wa kupanua shamba(kama umeelewa maelezo yangu) kwahiyo na uhakika na nachokiandika. Mwenye nia hasa atakuja shambani na kuuliza maswali yote, kama nia haipo hata niandike pages 200 bado maswali yatakuwepo tu. Karibu sana shambani tuwekeze mkuu
KAMA VIZIMBA 30 UNAPATA FAIDA YA 1.5M KWA MWEZI, KWANINI UTAFUTE MWEKEZAJI MWENZA WA KUWEKA 800,000/= ILHALI UNAWEZA KUIPATA PESA HII NDANI YA MWEZI MMOJA KUTOKA FAIDA YA MAUZO YAKO???

Aquila non capit muscas!
Mkuu soma vizuri maelezo. Naitaji kupanua shamba ili lifikie matuta 30, ili kupanua naitaji mashine kubwa ya umwagiliaji ya Inchi 4 pamoja na mipira mita 100, bira hivyo sinafikia fully capacity ya kulima matuta 30.
 
Yuko sawa amesema kwa ajiri ya kununua pump ya maji + mipira yakuvutia maji hiyo siyo kesi.yye alitakiwa ajazie nyama maelezo yake mfano mtu kawekeza 800,000/=lakini atapata 500,000/=kila mwezi sawa je?anapo sema miezi 4 mfurulizo atapata 2,000,000/= swali kwahiyo aliye wekeza hata pata 500,000/= bali ni 300,000/=kwa maana jumla utapata 2,000,000/= ukitoa hela uliyo wekeza utapata 1,200,000/= maana haja ongelea 2,000,000+ 800,000= ?ndo nilikuwa namshauri atulie kwanza alafu aje kwa mapana ila hakuelewa.ndg njoo bado tunataka kuboresha wapate faida wengi kwa wazo lako usipo faidika wewe watafaidika wengine watakao soma baadae.
Mkuu uko sahihi na ahsante kwa kupanua wazo langu. Muwekezaji atawekeza Mashine na Mipira ya mita 100. Hii itakua bado mali yake akiitaji kuchukua baada ya miezi minne(kwani msimu wa mboga mboga unaisha mwezi wa 4 au 5) hilo ni sawa kwangu. Akitaka kuendelea kwenye kilimo cha nyanya mwezi wa 5 au tutafanya makubaliano mapya. Naitaji uwekeza wa vifaa sio lazima hela cash.
 
Hivi hamjawahi kuona uzi kama huu?

Nafikiri kuna member akasema si ukakope benki ili faida iwe yako peke yako?
Afu benki riba ni ndogo Sana. Milioni moja kwa mwaka anawalipa laki na sabini faida Yao basi.kuliko kuumia na hela za watu mkuu.
 
Kwa mtaji wa 800K (ambao sio mwingi na unaweza kuupata kwa wadau saccos au mtu wa karibu) kwa ushauri kama kweli una soko na kila kitu fanya hili jambo mwenyewe...

Partnerships comes with some extra baggage..., unless otherwise unahitaji zaidi ya pesa pekee kwa huyo partner (yaani akusaidia masoko n.k.)
 
Back
Top Bottom