Mwekezaji MUTEX Moh Dewji (MB) akubali kufufua kiwanda baada ya tishio toka kwa Nyerere (MB)

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Sitta Tumma, Dodoma

MWEKEZAJI wa Kiwanda cha kutengeneza nguo cha Mutex kilichoko Musoma, mkoani Mara, amesalimu amri iliyotolewa na mbunge wa Musoma mjini ya kumtaka kuanza mara moja uzalishaji wa kiwanda hicho, vinginevyo atashukiwa na nguvu ya umma.

Mwekezaji huyo tayari ameahidi kuanza uzalishaji kiwandani hapo hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuondoa matumizi mengine yaliyokuwa yakilalamikiwa na wananchi ambapo kiwanda hicho kilidaiwa kugeuzwa kuwa ghala la kuhifadhia vitu, badala ya kuzalisha na kutoa ajira kwa Watanzania.

Akizungumza mjini Dodoma hivi karibuni, mbunge wa Musoma mjini, Vincent Nyerere (CHADEMA), alisema mwekezaji huyo ambaye pia ni mbunge wa Singida mjini, Mohamed Dewji (CCM), yuko katika mikakati maalumu ya kuanza uzalishaji kiwandani hapo siku za usoni.

Kwa mujibu wa Nyerere, kuanza kwa uzalishaji wa kiwanda hicho cha Mutex kutasaidia maradufu upatikanaji wa ajira kwa vijana wa Kitanzania, hasa wa mji na mkoa huo na kwamba hatua hiyo imekuja baada ya yeye kulivalia njuga suala hilo.

"Huyu mwekezaji wa kiwanda cha Mutex ambaye pia ni mbunge wa Singida mjini, Mohamed Dewji, amenihakikishia kwamba kiwanda kitaanza uzalishaji wake hivi karibuni, na hii itasaidia sana upatikanaji wa ajira kwa vijana wetu," alisema. Hivi karibuni, mbunge huyo alimtaka mwekezaji huyo kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kutumika katika uzalishaji wake wa nguo kabla hajarudi kutoka Bungeni mwezi huu, na kwamba iwapo agizo lake hilo lingepuuzwa angeitisha maandamano makubwa kumtoa mwekezaji huyo.
 
Back
Top Bottom