Mwekezaji mpya Portsmouth amrudisha Avram Grant | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwekezaji mpya Portsmouth amrudisha Avram Grant

Discussion in 'Sports' started by Richard, Oct 7, 2009.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuinunua timu ya Portsmouth kwa asilimia tisini, mwekezaji mpya wa timu hio bwana Ali Al Faraj, amemrudisha Avram Grant aliewahi kuwa mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

  Muisraeli bwana Grant alihamia katika timu ya Chelsea yenye makazi yake magharibi mwa jiji la London na kuwa mkurugenzi wa mpira kabla ya kuwa meneja wa timu hio baada ya Jose Mourinho kutimuliwa mwezi May mwaka 2008.

  Bwana Grant atashirikiana na meneja wa sasa Paul Hart kuhakikisha timu hio inapanda ngazi na kuepuka kuwa mkiani ambapo mpaka sasa timu hio ina pointi tatu tu ilizozipata siku ya jumamosi ilipocheza na kuifunga timu ya Wolverhampton kwa bao moja bila majibu.

  Pamoja na mambo mengine kazi za mkurugenzi wa mpira kwenye timu ni kushughulikia usajili, kukuza vitalu vya wachezaji kupitia shule maalum (Footbal Academies), na kumwakilisha meneja kwenye vikao mbalimbali vya bodi ya wakurugenzi.

  Timu ya Portsmouth ambayo kama timu ingine ya Newcastle ambayo ilishuka daraja mwishoni mwa msimu uliopita imeanza vibaya msimu huu kwa kupoteza mechi zake zote saba ikiwemo dhidi ya Arsenal ambapo ililambwa goli 4-1.

  Portsmouth au Pompey kama inavyojulikana, inacheza na Tottenham Hotspur siku ya jumamosi mechi itakayofanyika katika uwanja wake wa nyumbani wa Fratton Park.
   
Loading...