Mwekezaji mgodi wa El-hillal Mwadui Shinyanga hajalipa mishahara ya wafanyakazi kwa miezi minne

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
323
500
Katika hali ya kushangaza na kustajabisha mwekezaji wa mgodi wa El-hillal maarufu kama Fantom hajalipa mishahara ya WAFANYAKAZI wake kwa mda wa miezi minne kwa kisingizio kuwa mtoa pesa yupo Uarabuni.

Hii imefanya wafanyakazi kushindwa kujikimu kimaisha pamoja na familia zao hata makazi ya wafanyakazi wanaoishi katika mgodi huo hayaridhishi. Nyumba nyumba za mabati ambayo mabati hayo yameshaoza kiasi kwamba mvua zikinyesha mvua huwanyeshea.

Kwa hali hiyo kuna kila sababu idara husika ya wafanyakazi kuingilia kati ili kuweza kutatua tatizo hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
18,164
2,000
Duh waarabu wa Luhumbo hawa balaa tupu. Ila biashara ya Almas sasa hivi sio nzuri. Kuliko kuwadanganya bora awaambie ukweli tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom