Mwekezaji asiyejua kiswahili asije jimboni kwangu -mbunge kigola

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]

Na Francins Godwin Mzee wa matukio Daima- Iringa


MBUNGE wa jimbo la Mufindi kusini Mendrady Kigola aishauri serikali kutowaruhusu wawekezaji wasiojua Kiswahili kufika kuwekeza katika jimbo lake ili kuzuia utapeli unaofanywa na baadhi ya wawekezaji kuingia mikataba feki na wananchi wasiojua lugha za kigeni.


Kigola alitoa ushauri huo jana wakati wa kikao cha pamoja Kati ya wawekezaji wakubwa katika msitu wa Sao Hill na waziri wa maliasili na utalii Ezekiel Maige.


Alisema ni vema serikali kuweka utaratibu wa mzuri wa wawekezaji kupewa kipindi cha miezi sita ya kujifunga lugha ya Kiswahili na iwapo watashindwa kufanya hivyo basi wasikubaliwe kupewa nafasi ya kuwekeza katika jimbo hilo.


"Mheshimiwa waziri lazima tuwe na utaratibu wa kuwapa muda wa miezi sita ya kujifunza lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya Taifa ili kuepusha wananchi kuingia mikataba na wawekezaji hao pia kujua nini wamesaini katika mkataba husika"


Kigola alisema Kama kweli wawekezaji hao wanataka kuwekeza kwa wananchi wa jimbo hilo ni lazima kuwepo utaratibu wa wawekezaji na wananchi kujua vema aina ya mikataba hiyo na lugha rahisi kwa wananchi hao wa vijijini ambao wanakwenda kuwekeza ni Kiswahili pekee.


Hivyo alisema kuwa iwapo wawekezaji wenye lengo la kuwekeza katika jimbo la Mufindi kusini na wilaya ya Mufindi lazima kwanza wapewe muda wa kujifunza lugha ya Kiswahili na pale wanaposhindwa kuelewa kwa muda waliopewa basi watakuwa wameshindwa kuwekeza katika maeneo yao.


Alisema hata migogoro ya ardhi inayojitokeza Kati ya wizara ya maliasili na utalii hasa kwenye maeneo ya hifadhi za Taifa na wananchi ni kutokana na wananchi kuingia mikataba na kuuza ardhi Yao bila kujua aina ya mikataba kutokana na baadhi Yao kutoelewa vema lugha ya kiingereza ambayo hutumika kwenye mikataba husika.


Hata hivyo katika ukumbi huo kilikuwa na wawekezaji wa kigeni watatu ambao lugha hiyo ya Kiswahili Kwao ilikuwa ni tatizo .


Ushauri huo uliungwa mkono pia na waziri Maige nakutaka kikao hicho ambacho tayari kilikuwa kikiendeshwa kwa lugha ya kiingereza kulazimika kutumia lugha ya Kiswahili mwanzo hadi mwisho.


Waziri Maige alisema kuwa ushauri wa mbunge Kigola ni ushauri wa kuungwa mkono Kwani hivi sasa Tanzania ipo katika mchakato wa kufikisha lugha ya Kiswahili zaidi na hivyo lazima ushauri huo uanze kutumika katika kikao hicho.


Kwa upande wao wawekezaji hao kutoka makampuni mbali mbali likiwemo la Green Resource na kiwanda cha karatasi cha MPM Mgololo walikubaliana na ushauri huo wa mbunge Kigola na kuwa kwa upande wao tayari wameajiri mwalimu wa kufundisha lugha ya Kiswahili ambaye ameanza kuwafundisha lugha hiyo.
 
Atapata Wawekezaji Uchwara - WACHINA; Watakula vijidudu vyote jimboni kwake...
 
Kama huo msimamo ungekaziwa, pangekuwa na nafuu kiasi fulani.
 
Back
Top Bottom