Mwekezaji anakuwaje mwekezwaji! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwekezaji anakuwaje mwekezwaji!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 1, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,208
  Trophy Points: 280
  Date::9/27/2008
  Mwekezaji anakuwaje mwekezwaji!
  Na Daniel Mwaijega
  Mwananchi

  INASHANGAZA sana, kwani wakati mwingine huwa tunafanya vitu kama vya mchezo wa Pwagu na Pwaguzi. Naamanisha kwamba, kuna vitu tunaamua hapa nchini kama vile tuko katika mchezo wa kuigiza usio na manufaa hata kwa waigizaji wenyewe.

  Hicho ndicho kinachonishangaza, kwani siku hizi hakuna kitu cha bure, hata hao wachekeshaji mitaani hawafanyi bila kutupiwa fedha. Sasa inakuwaje baadhi ya watu tunaowapa mashirika ya umma au miradi iliyokuwa ya umma kwa mgongo wa uwekezaji wanashindwa kuiendeleza mpaka serikali inawasaidi?

  Hoja hii inafuatia mwekezaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) baada ya kushindwa kuwalipa wafanyakazi kiwango alichoahidi Machi mwaka huu kwamba angewapa kuanzia Agosti na wao kutishia kuitisha mgomo nchi nzima, na serikali kulazimika kumkopesha ili kunusuru hali hiyo.

  Si jambo la kawaida kwa mwekezaji kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza bila kuwa na mtaji wa kutosha kuboresha uzalishaji na huduma kwa wafanyakazi wake. Si jambo la kawaida pia kwa serikali kumkopesha fedha mwekezaji mgeni, ambaye binafsi naamini kwamba kutokana na masafa marefu aliyosafiri kutoka nchini kwao kuja kwetu alikuwa amejipanga kwa kuwa na mtaji wa kutosha, kufufua na kuendesha mradi alioomba kuwekeza.

  Mwekezaji wa TRL ambaye ameikabidhi menejimenti ya kampuni hiyo majukumu ya usimamizi na uendeshaji wa shughuli zote na kuhakikisha kuwa inapata faida na kuwatunza vizuri wafanyakazi ili waweze kufanyakazi wa bidii na furaha, amefanya kinyume na kusababisha mgogoro wa kimaslahi uliotunga mimba ya mgomo wa wafanyakazi kudai haki zao.

  Wadau mbalimbali wanauliza kwamba, ni kwa vipi serikali iliamua kutoa mkopo wa Sh350 milioni kwa kampuni hiyo ili kunusuru mgomo uliokuwa unafutuka, tena ikiwa ni mara ya pili baada ya Sh3.6 bilioni ilizoikopesha Aprili mwaka huu, wafanyakazi hao walipogoma nchini nzima?

  Swali lingine ni kwamba je, wakati mwekezaji huyo anaomba na kushinda zabuni hiyo, ulifanyika uchunguzi wa kutosha juu ya uwezo wake kifedha na si maneno matupu au siasa kibiashara ambazo wajanja huzitumia kujitajirisha kwa kuja kukopa katika benki hapa kwetu?


  Ninachojua ni kwamba, mwekezaji hata kama hana fedha za kutosha, ili kuficha aibu, aidha hukopa kutoka kwenye taasisi za fedha nchini kwao au hukusanya nguvu kutokana kwa wafanyabiasha wenzake chini ya mkataba maalum ili kuwa na mtaji wa kutosha. Kwa huyu bwana mambo yalikuwaje?

  Nakumbuka wakati wa mchakato huo na hasa baada ya kushinda zabuni hiyo, watu wengi walikuwa na hofu naye na hata kufikia kupiga kelele kwamba wana mashaka kama anaweza kufufua huduma ya reli hiyo kutokana na wasiwasi wao juu ya uzoefu wake katika uendeshaji wa huduma hiyo. Lakini alitamba kwamba ana uwezo wa kufufua huduma hiyo ya reli kwa kununu injini na mabehewa mapya ya abiria.

  Swali lingine ni kwamba je, serikali kweli imemkopesha mwekezaji huyo au inampa azitumie tu, yaani arudishe au asirudishe yote sawa, kama isemavyo methali ya Kiswahili kwamba, Ā‘Kiendacho kwa mganga hakirudiĀ’.

  Lini pia nakumbuka wakati wa mgogoro wa mwezi Machi, Waziri Mkuu alinukuriwa na vyombo vya habari akisema kwamba kulingana na makubaliano yake na uwekezaji, serikali ilikuwa haijalipa mchango wake wa uwekezaji kama mwanahisa. Je, ni kweli hiyo?

  Naogopa tusije tukawa tunamkandamiza mwekezaji wa nje kumbe yeye alishatoa sehemu yake ambayo ilitumika kugharamia vitu vingine katika mkakati wake wa kuboresha huduma, hivyo baada ya kuona mwanahisa mwenzake kala jiwe na yeye akaamua kuweka mgomo baridi kama njia ya kumsukua atoe. Nani anapenda kupata hasara.

  Si mnajua kwamba mwekezaji ni mfanyabiahara na hakuna mfanyabiashara makini anayependa hasara.

  Inawezekana kwa kutoa kiasi hicho cha fedha mara mbili mfululizo ni njia ya serikali kufidia mkopo wake wa kuchangia mataji wa uwekezaji. Ndiyo, kama kweli haikutoa, ni mkopo usioonekana wazi, lakini katika vitabu vya mahesabu ya kampuni hiyo vinaonyesha kwamba mwekezaji X hajatoa kitu.

  Katika mikataba ya uwekezaji ambapo watu wawili au zaidi wanaungana kuendesha biashara, maana yake wanagawana hisa ambazo hugeuzwa katika fedha kwa ajili ya kuwekeza mtaji au amana, ambazo hufanywa mtaji wa kuwekeza, hivyo kama mmoja wao hajatoa maana yake kuna majukumu yatasimama na kusababisha uendeshaji kukwama kulingana na makubaliano ya wanahisa kuchangia.

  Naomba ieleweke kwamba, wakati tunazungumzia mwekezaji ambaye anashirikina na wenzake, maana yake wote kwa pamoja wanafichwa chini ya mwamvuli mmoja.

  Namaanisha kwamba, mwekezaji wa TRL ni pamoja na serikali na kama mgomo ungetokea , kwa kuwa ni sehemu ya uwekezaji, hivyo na yenyewe inaathirika ikiwa ni pamoja na kulaumiwa na waathirika wa huduma mbaya.

  Kwa ujumla ni kwamba, jamii imechoshwa na uwekezaji wa kubabaisha kama ilivyo kwa TRL, ndiyo maana tunahoji kwamba huyo ni mwekezaji wa aina gani, ambaye kila wakati anabebwa au anawezeshwa au anawekezwa, badala ya kuwekeza.

  Kuna tatizo moja ambalo baadhi ya wawekezaji wanalipuuzia ambalo ni suala la uwekezaji katika rasilimali watu ambayo isipotunzwa vizuri inaweza kusababisha hasara kubwa pengine hata kampuni au shirika kuvunjika.

  Waajiri wengi wanathamini zaidi mashine na mitambo ya uzalishaji kuliko wafanyakazi (watu) kiasi cha kuwa tayari kuikarabati kila wakati huku wanaoisimamia na kuiendesha wakisahaulika. Je, mitambo bila wasimamizi inaweza kwenda?

  Mbona wakigoma kazi ina simama au chukulia mfano wa mgomo wa wafanyazi wa TRL ulipotokea Machi, mbona treni zote zilisimama licha ya kutokuwa na matatizo ya kiufundi?

  Mgomo mwingine ni wa wafanyakazi wa NMB uliofanyika mwanzoni, na kusababisha huduma kutoka na kuweka fedha kukwama licha ya kuwapo kwa machine za kutoa fedha, ambazo hazikuweza kufanyakazi kwa muda mrefu kutokana na kutokuwepo watu wa kuweka fedha?

  Hilo ni fundisho kwa wakwekezaji na serikali kwamba, tunahitaji kuwa makini na watu wanaojiita wawekezaji wakati ni wababaishaji, wanaolenga kupata faida kubwa kwa kutumia gharama kidogo pamoja na kutojali wala kusikilia kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi.

  Pia lazima tuwe makini na wawekezaji wanaojua kuahidi uwongo kama ilivyofanya TRL mwezi Aprili, kwamba itaanza kuwalipa wafanyakazi wake mishahara mipya ya Sh200,000 kuanzia Agosti mwaka huu, na ulipofika muda wakashindwa.

  Kwa nini waliahidi kama hawakuwa na uhakika wa kuongeza mapato? Nani asiyejua kwamba faida ya uwekezaji haipatikani ndani ya mwaka mmoja kwa mradi mkubwa kama wa usafiri wa reli, ambao mpaka wakati wanauchukua ulikuwa katika hali mbaya?

  Hili ni fundisho kwamba mwekezaji lazima awe muwazi na mipango thabiti ya kuboroshea huduma katika seketa zote kwa awamu zinazolingana. Kwa sababu kama utasema nitanunua mabehewa na injini bila kukumbuka wafanyakazi itakuwa kazi ngumu sana.

  Jambo lingine baya kwa waajiri ni tabia ya kutowashirikisha wafanyakazi wao mambo yanavyokwenda katika kampuni, ikiwamo katika kupanga mikakati ya kuboresha huduma kwa malengo maalumu ya kupata faida.

  Tatizo hilo hujenga ufa mkubwa unaozaa migomo, kwa sababu hata kama kampuni inapata hasara, wafanyakazi wanakuwa hawajui na watagoma kuliko kama wangeshirikishwa. Hata kama wakidai wanakuwa na kiasi au subira kutokana na kujua hali halisi na kujiona sehemu ya kampuni kwa kuwa wanashirikishwa kikamilifu katika mambo yote.

  Baruapepe: mwaijega@yahoo.com

  Simu: 0713 704 898
   
Loading...