Mwekezaji anahitajika katika project hii

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,460
TAA ZA KUCHAJI KWA AJILI YA WAFANYABIASHARA ZA USIKU.

Hizi ni taa zinazo faa kwa matumizi aina zote yanayo hitaji mwanga mkali kwa muda mrefu.Vijijini na Mijini.

SIFA ZA KIMATUMIZI YA TAA HIZI.

1.Ikiwa full charge inauwezo wa kuwaka masaa 8 (full light),bila kuchaji simu,na masaa 6 (full light) ukichaji simu.

2.Zina uwezo wa kuwaka masaa 15 (mean light),bila kuchaji simu,na masaa 12 (mean light) ukichaji simu.

3.Zina "brightness control nob"ambapo mtumiaji anaweza kupandisha ama kushusha mwanga kwa kiwango anachotaka,mfano kama anasoma ataweka mwanga unao mfaa kwa ajili ya kusomea.

4.Zina uwezo wa kuchajiwa na Solar au umeme wa Tanesco.

5.Zina USB port kwa ajili ya kuchaji simu.

6.Ina full charge indicator na low charge indicator.

7.Ina uzito wa gram 540

8.Taa na charger yake ni removable

9.Ina switch ya ON na OFF

SIFA ZA KITAALAM ZA TAA HIZI.

1.Zinatumia Lithium-ion power bank battery with 7AH.

2. Output voltage 12VDC

3. Maximum output current 700mA (0.7A)

4.Zina Over Charging control na Over Discharging control

5.Zina battery thermal protection.

6.Zina solar charging port na Electrical charging port

7.Zina ON na OFF switch

8.Over load protection

9.Zina USB port with 5VDC 500mA

10.Zina Variable light switch

ASPECT YA KIBIASHARA YA TAA HIZI.

1.Kwa maeneo ya mjini mfano Dar es Salaam.

*Maeneo ya Dar wafanyabiashara wengine wenye vibanda vinavyotembea na vile vilivyo simama wamekua wakifanya biashara zao usiku,hivyo huhitaji mwanga mzuri kwa biashara zao.

Ukipita usiku utakuta wafanyabiashara wengi wamening'iniza taa kwenye vibanda vyao,basi hao ndiyo wateja mojawapo wa taa hizi.

Tayari nimeshafanya tafiti na kuwapelekea bidhaa hii wafanyabiashara hawa na ndiyo kwa ushauri wao walipokuwa wakitumia taa hizi walitoa mapendekezo ambayo yaliboresha baadhi ya vitu katika taa hizi ambavyo toleo la awali halikua navyo.

COMPETITOR WA BIASHARA HII.

1.Taa za kichina zilizotengenezwa maalumu kwa ajiri ya wafanyabiashara wadogo wadogo wa usiku.

*Hizi taa za kichina zinakodishwa kwa wafanyabiashara hawa,kwa bei ya kuanzia 500 hadi 600,kutegemeana na maeneo.

*Mfanyabiashara hukodi ndani ya masaa 12 (wanakodi kuanzia saa 10 jioni,na hutakiwa kurudisha taa hizo kabla ya saa mbili asubuhi siku inayofata ili ichajiwe).

Taa hizi zinasifa karibia sawa na taa ambazo natengeneza mimi,ila tofauti kubwa ni hizi.

1. Taa hizi za kichina zinafanya kazi kwa timer,baada ya masaa saba taa inazima hata kama inachaji,baada ya hapo haiwaki tena,hadi urudishe kwa aliyekodisha azi reset,hvyo ukienda nayo nyumbani huwezi itumia,as longer muda wa masaa hayo umeisha.

*Hazina charger individual zinachajiwa as a group.

*Haiuzwi kwa moja moja.

*Ni za kugombania,zinakodishwa kwa kujuana.

*Mwanga wake haufikii hizi zangu.

Tutapambanaje na huyu mchina?

1.Bei yetu iwe tofauti ya shilingi mia ya wale wanaokodisha za mchina.

2.Mteja awe na uwezo wa kutumia taa hata akienda nayo nyumbani as longer taa bado inachaji.

3.Mteja akitaka kununua aruhusiwe,hata kwa kuweka kidogokidogo hadi amalize,kulingana na bei tutakayo weka.
Akimaliza kulipia apewe chaji yake.

4.Faini ya kupoteza au kuibiwa taa iwe chini ya ile faini waliyoweka wale wanaokodisha za mchina,ambapo nimeambiwa ya mchina ukipoteza unalipa 100,000/,sisi tunaweza fanya 80,000/

5.Muda wa kurejesha tunaweza usogeza mbele.

PROTECTION DHIDI YA WATEJA WAJANJA JANJA.

*Mteja akikodi ataweza kuitumia hata akiwa nyumbani LAKINI asiwe na uwezo wa kuichaji hata kwa kufoji chaji.

Hili litawezekana kwa kufunga automatic infrared switch ambazo zitakua zinakubali kuwasha mfumo wa chaji baada ya kuditect infrared transimitter ambayo itakua katika chumba chetu cha kuchajia,ambapo taa ikiingizwa katika hicho chumba itakubali kuchaji ikitoka haikubali.

Mteja akitaka kununua taa za model yetu,tutamtengenezea ambayo haina charging protection.

* Taa zinatakiwa ziwe sealed kulinda kufunguliwa,na kama ikionekana imefunguliwa mteja atainunua.

GHARAMA ZA UTENGENEZAJI WA TAA HIZI.

Kwa toleo hili la mwisho taa moja ilinigharimu 40,000/- na chaji ya umeme,na kama utanunua na solar yake itafika 55,000/-

MAJARIBIO YA KIBIASHARA.

Nilifanikiwa kupeleka taa hizi zilikua tatu katika eneo la wafanyabiashara wa usiku wa Gongolamboto nikakodisha 400,kwa kila taa,baada ya kuzijaribu walizipenda sana wakasema wanazihitaji na wanapiga simu kuziulizia.

Nilipeleka pia taa hizo mbezi sokoni pale stand ya Goba na mwenge walizipenda,hawa hawakutaka hata nirudi nazo walizinunua zote tatu!

Nilipanga nipeleke sample,Mbagala,Buguruni na Tandika ila ckufanikiwa sababu nilikua nimesha ziuza.

UFANYAJI BIASHARA HII MJINI
Utatakiwa uwe na kituo cha kukodishia taa hizi,kituo kiwe jirani na wafanyabiashara hawa wa usiku.

Kituo hichi ndicho ambacho utakitumia kuchajia taa zako,iwe kwa umeme au solar.

BIASHARA HII VIJIJINI
Bado cjafanya utafiti vijijini,ila mfumo wa taa hizi unaweza kutumika vijijini katika namna mbili.

1.Kuwakodishia wanakijiji,ambapo unakua na center ambayo unazichaji kwa solar,na mteja anakuja kukodi taa,ambayo ataweza kuitumia siku 3,na kuirejesha.

Mteja ataitumia taa hiyo kwa ajili ya mwanga lakini pia kuchaji simu.

2.Unamuuzia mteja taa kwa malipo kidogo kidogo,ambapo taa hizi na solar yake inagharimu 55,000/-kuitengeneza.

FAIDA YA TAA HIZI KIMFUMO.
1.Ni rahisi kuzifanyia service zikiharibika.Spea zake zpo
2.Ni rahisi kuziboresha kulingana na mahitaji ya soko,bila kununua nyingine.
3.Zina guarantee ya miaka 2.

FAIDA ZA KIUCHUMI
1.Zinasaidia wafanyabiasha kufanya kazi zao bila kujali giza
2.Zinakuza uchumi wa Taifa,mkodishaji,mfanyabiashara na mtengenezaji.
3.Inasaidia kukuza technolojia ya wabunifu wa kisayansi wa hapa kwetu.
4.Biashara isiyo expire au kupitwa na fasheni

Kwa ambaye atataka kuwekeza katika hili naomba tuwasiliane.

Kwa project zangu nyingime za ubunifu tembelea post zangu za hapa jamiiforums...unaweza ukavutiwa na yoyote na ukawekeza.

Asanten...
Transistor.
 
Attachments

  • A.jpg
    A.jpg
    113.7 KB · Views: 70
  • Aaa.jpg
    Aaa.jpg
    115.8 KB · Views: 72

Ungependa mtu awekeze kiasi gani , pm
 
Umeleza vizuri na kila kitu unakiweza, soko pia umeshalipata sasa ni wewe kutekeleza tu au unahitaji nini labda?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom