Mwekezaji ampa Siku saba DC kumwomba radhi

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
581
1,000
Mkuu wa wilaya ya Longido Frenk Mwaisumbe ameagiza kukamatwa kwa mwekezaji wa Kampuni ya uwindaji ya Green Mille's Safaris LTD Awardhi Abdallah Ally popote alipo na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kutokana na kukaidi kulipa deni la sh,milioni 339 za vijiji 23 wilayani humo.

Awali mwekezaji huyo kupitia wanasheria wake wiki iliyopita alimwandikia notisi ya siku saba mkuu huyo wa wilaya, akimtaka akanushe kauli yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari na kumsafisha,inayodai kuwa kampuni yake inadaiwa na vijiji 23 na kwamba baada ya muda huo kupita angempandisha mahakamani.

Akiongea na vyombo vya habari jijini hapa mapema leo,Mwaisumbe amedai kuwa mwekezaji huyo ameshindwa kulipa deni hilo baada ya kuingia makubaliano na vijiji hivyo 23, tangu mwaka 2013 na kushindwa kutekeleza ahadi yake.

Alisema fedha hizo ni zao la makubaliano ya kusaidia maendeleo katika vijiji hivyo vilivyoko jirani na eneo lake la uwekezaji kama sheria ya uwekezaji inavyosema ikiwa nipamoja na utunzaji wa mazingira ,ulinzi wa maliasili na ujenzi wa miundo mbinu, ambapo alikubali kulipa kiasi cha sh,milioni 4.5 na kiasi cha shilingi milioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya maendeleo ya elimu kwa kila kijiji.

" Tangu ameingia makubaliano na vijiji hivyo mwaka 2013 amelipa mwaka mmoja tu 2014 kwa vijiji vyote na mwaka 2015 alidai anakesi mahakamani hivyo kushindwa kulipa lakini kuanzia mwaka 2016 hakuweza kulipa chochote hadi sasa"Alisema mkuu huyo

Amemtaka Mkurugenzi huyo kujisalimisha popote alipo katika kituo chochote cha Polisi Tanzania bara au Visiwani ili aweze kulipa deni hilo na asipofanya hivyo nimeagiza akamatwe popote alipo.

"Akikamatwa hawezi kutoka bila kulipa fedha za wanakijiji hivyo ajitayarishe sisi hatuna mzaha tupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi " Alisema

Jitihada za kumpatia mwekezaji huyo hazikuweza kuzaa matunda kutokana na kutopatikana kupitia Simu yake ya Mikononi.

Ends......

IMG_20190226_114814.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,977
2,000
Tanzania loooooo ni ya vituko,DC wangu kabla ya kukamata ni lazima ufungue kesi kwanza polisi,kwa hiyo fungua kesi pale polisi na peleka ushahidi wako then polisi watachunguza na wao ndio wenye mamlaka ya to arrest baada ya ku apply their mind na kushauriana na mwendesha mashitaka na kuona kama kuna winnable case!!!!natamani niende pale Mto Ruvuma na kujirusha nipotelee mbali.
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,755
2,000
Tanzania loooooo ni ya vituko,DC wangu kabla ya kukamata ni lazima ufungue kesi kwanza polisi,kwa hiyo fungua kesi pale polisi na peleka ushahidi wako then polisi watachunguza na wao ndio wenye mamlaka ya to arrest baada ya ku apply their mind na kushauriana na mwendesha mashitaka na kuona kama kuna winnable case!!!!natamani niende pale Mto Ruvuma na kujirusha nipotelee mbali.
Mkuu inaonekana hujauelewa utawala huu
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,616
2,000
Kama mpaka mnakwenda hewani juhudi za kumpata huyo Mkurugenzi hazikufanikiwa ninyi hizo taarifa za mkurugenzi kutaka kuombwa radhi ndani ya siku saba mmezitoa wapi?
 

BAF

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
418
1,000
Umenichanganya kidogo na ulichoandika na Kichwa Cha Habari.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom