Mwekezaji afunga shule, wanafunzi washindwa kuendelea na masomo

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Points
1,225

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 1,225

Imeandikwa na John Nditi, Mvomero; Tarehe: 27th August 2011

WANAFUNZI wa shule ya awali katika Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero, wameshindwa kuendelea na masomo yao kwa muda mrefu baada ya jengo la shule yao lililojengwa kwa nguvu za wananchi kuzuiwa na mwekezaji wa kigeni kwa kuzungushia uzio wa seng'enge.

Pamoja na jengo la shule hiyo, sehemu kubwa ya ardhi ya wananchi wa kitongoji hicho imemezwa na mwekezaji na kusababisha kujitokeza kwa mgogoro mkubwa wa kugombea mipaka ya ardhi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa hadhara uliolenga kuzikutanisha pande mbili zenye mgogoro huo chini ya Mkurugenzi wa Wilaya hiyo na maofisa wake wa Idara ya Ardhi, wananchi hao wameulamu uongozi wa Halmashauri kwa kushindwa kutokea katika mkutano huo.

Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, waliandika barua ya kuutaka uongozi wa Serikali ya Kijiji kuitishwa mkutano wa pamoja wa pande hizo, Agosti 23, mwaka huu, kwa ajili ya kujadili mgogoro huo, walishindwa kutokea akiwemo Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji na Mwekezaji huyo.

Mwenyekiti wa zamani wa Serikali ya Kijiji cha Kipera, Ally Kidunda alidai kuwa kushindwa kutokea kwa viongozi hao ambao wenyewe ndio walioandika barua na kupanga siku ya mkutano huo, kunawatia wasiwasi juu ya kutaka kuficha ukweli wa mambo.

"Wananchi wa Kipera wanachokitafuta ni kujua huyu mwekezaji ameingiaje kijijini hadi ameuziwa ardhi kubwa ndani ya kijiji, tumefikia hatua ya Kamati ya kufuatilia jambo hili imefika sehemu nyingi wilayani na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, hadi sasa hatujamwona kiongozi yeyote kufika eneo hili kupata picha kamili na kuangalia mgogoro huu mipaka ya ardhi.

"Sisi hatuna imani na viongozi wetu, kama wao ndiyo wameandika barua yenye kumbukumbu namba MVDC /V.10/4/12 ya Agosti 4, mwaka huu na kutaja tarehe 23 mwezi huu ni siku ya kufanyika mkutano wa pamoja wa mgogoro wa shamba namba 296 Kinyezi , Kipera, Wilaya ya Mvomero, sasa mbona wameshindwa kutokea?" Alihoji Kidunda.

Mkazi mwingine wa Kitongoji hicho, Said Ahamad alisema wakazi wa kijiji hicho ni watu wanaoheshimu sheria na kufuata utaratibu wa kutatua migogoro, lakini itafika wakati watashindwa kuvumilia na kujichukulia sheria mikononi, jambo ambalo alisema ni hatari kwa amani na utulivu.

Kwa upande wao, Mwajabu Shaabani, Hadija Mwinyipembe na Mawazia Kibwana, wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo, walidai kuwa uzio huo pia umefunga njia kuu iliyokuwa ikitumiwa kwenda katika mashamba yao hivyo kusababisha mazao kuharibikia shambani zikiwemo nyanya.

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Points
1,225

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 1,225
Mbunge wa Mvomero aliwahi kuwa Mweka Fedha wa CCM - CC (Jina limenitoka)...

Anajihusisha sana na Lady JayDee, sasa hajui mwekezaji gani huyu? wakati Jimbo lilipokuwa na Mbunge Mhindi (nimesahau jina) hawakuwa na Matatizo haya.

Walimpigia Campaign ya Nguvu, Lady JayDee alikuwa akienda kumuimbia Sasa ndio wanagawa Ardhi kwa Walafi???

Rugaijamu

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2010
Messages
2,930
Points
2,000

Rugaijamu

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2010
2,930 2,000
Mbunge wa Mvomero aliwahi kuwa Mweka Fedha wa CCM - CC (Jina limenitoka)...

Anajihusisha sana na Lady JayDee, sasa hajui mwekezaji gani huyu? wakati Jimbo lilipokuwa na Mbunge Mhindi (nimesahau jina) hawakuwa na Matatizo haya.

Walimpigia Campaign ya Nguvu, Lady JayDee alikuwa akienda kumuimbia Sasa ndio wanagawa Ardhi kwa Walafi???

Mbunge wao wa sasa ni pedeshee Amos Makala.

Forum statistics

Threads 1,356,388
Members 518,903
Posts 33,131,724
Top