Mwekezaji adaiwa kuwanyanyasa wananchi Serengeti

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
49,282
19,617
Mwekezaji adaiwa kuwanyanyasa wananchi Serengeti
Na Mwandishi Wetu, Serengeti

SERIKALI wilayani Serengeti imeombwa kufuatilia vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, unaofanywa na askari wa wanyamapori kwa kushirikiana na kampuni ya Grumet.


Kilio hicho, kimetolewa hivi karibuni na wakazi wa kitongoji cha Makundusi Kata ya Natta kwenye mkutano mkuu kufuatia askari hao kuvamia nyumbani kwa mkazi mmoja wa kitongoji hicho na kumpiga kijana wake na kupora fedha Sh 4 milioni.


Wakizungumza katika mkutano huo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa wakazi hao, William Ikumbo kwa nyakati tofauti walisema askari hao wanawatesa na kuwanyanyasa na hivyo kuishi kwa hofu.


Walisema licha ya mwekezaji huyo kuwepo katika kitongoji hicho, amegeuka kuwa adui mkubwa kwa jamii kutokana na kupigwa bila makosa yoyote.


Walidai kuwa malalamiko yao yamekuwa yakipuuzwa na ngazi mbalimbali za polisi kwa kuwa mwekezaji huyo anawasaidia polisi hao mambo mbalimbali na hivyo kusahau wajibu wao wa kulinda raia na mali zao.


Wananchi hao kwa hasira walidai wamekuwa wakikamatwa na kupigwa kwa madai wao wanajihusisha na uwindaji haramu na kupelekwa polisi.


�Wakati anaomba kuwekeza hapa alikuwa akitumia lugha nzuri za mahusiano, tena akiwatumia viongozi wetu. Jamii inajuta kuishi karibu na mwekezaji huyu kutokana na vipigo na kero mbalimbali zikiwemo za kuvamiwa kwenye majumba yao bila hata utaratibu,�alisema mkazi mmoja.


Sadock Majura alidai mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 anayesoma darasa la sita katika shule ya Natta akiwa anachunga mifugo alikamatwa na kupelekwa polisi Mugumu bila kuwa na uthibitisho wowote unaohusika na ujangili.


Ikumbo akizungumzia matukio hayo alidai Juni 28, saa 9.45 alasiri askari hao wa wanyama pori na kampuni hiyo na walimpiga kijana Muhabe Marwa (20) ndani ya nyumba ya ndugu yake na kufanya upekuzi na baadaye ilibainika kupotea kwa Sh 4 milioni za Nyambura Nyamhanga alizozipata baada ya kuuza ng�ombe.


Mwenyekiti wa Kijiji hakupatikana ili kuzungumzia tuhuma hizo. Pamoja na kutopatikana juhudi zinaendelea za kumtafuta mwekiti huyo ili kupata maelezo zaidi wa malalamiko ya wakazi hao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom