Mwarubaini Mmea Mjarabu Kutibu Maradhi Mbalimbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwarubaini Mmea Mjarabu Kutibu Maradhi Mbalimbali

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jul 31, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG] [​IMG]
  Mti wa Mwarubaini (Neem)  KATIKA karne hii ya sayansi na teknolojia, Mwenyezi Mungu amewajaalia baadhi ya wanadamu (Madaktari) kuwapa taaluma (elimu) ya kufahamu maradhi yanayosumbuwa wanaadamu wenzao kwa kutumia vifaa mbalimbali ikiwemo vya kisasa na dawa katika kuwatibu.
  Hata

  hivyo uwezo wa aina hii ulikuwepo hata kabla ya kuja sayansi na teknolojia ambapo binadamu wa awali alitumia tiba za asili kwa kujitibu na maradhi ya aina mbalimbali.
  Hivi sasa toka kuwepo sayansi na teknolojia, asilimia kubwa ya watu wanadharau kutumia dawa za asili na

  badala yake wameelemea sana katika matibabu ya dawa za kemikali.
  Kwa mtazamo, takribani miti yote iliyopo duniani ni dawa hivyo ni vizuri kwa jamii kuelimishwa ili kuweza kujuwa ni jinsi gani wataweza kuitumia miti hiyo kwa kuitibu miili yao.Kutokana na hali hiyo na matibabu

  hayo, inaonekana wazi kuwa mti wa Muarubaini ama wengine huita Mtunda, ni mjarabu kwakutibu maradhi mbalimbali na hivyo upo umuhimu wa kila mtu kuupanda katika makaazi yake na pia kwa kupitia Wizara ya kilimo kutenga eneo maalum kwa ajili ya kupanda miti ya

  aina hii.
  Mti wa Mwarubaini ambao kwa kiingereza unajulikana kama ‘Neem’ , ulianza kugunduliwa kama tiba ya maradhi zaidi ya miaka 4.000 iliyopita.Mti huu hutibu maradhi ya aina mbalimbali kwa kuanzia mizizi, magome, mbegu na majani yake.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa

  baraza la tiba asilia Zanzibar Mayasa Salum Ali, alisema mti wa Mwarubaini unapatikana au unaota zaidi katika nchi za joto kote Ulimwenguni.
  Mwenyekiti huyo ambae pia ni mtaalam wa fani hiyo alisema kwa upande wa watu wa India, kwao mti huu unasifa sana katika matibabu yao na unajulikana kama duka la dawa la kijiji.Aidha alifahamisha kuwa wanauthamini kama dawa kutokana na matibabu yake

  kwani unatibu maradhi ya aina mbalimbali ambayo humuandama mwanadamu na hata wanyama na mimea ya shambani.
  Hata hivyo kwa upande wa wataalamu wa India kutokana na umuhimu wa dawa hizi za asili, wamefakiwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kupitia mti huu ili kurahisisha matumizi ya watu kwa kupitia tiba ya mwarubaini.Bidhaa hizo ni pamoja na dawa za kumeza, dawa za mswaki, sabuni, vipodozi

  vya aina mbalimbali kama vile krimu, mafuta ya kujipaka ‘lotion’ , majani ya chai na vitu vingine vingi.
  China nayo haipo nyuma katika kutumia dawa za mti huu kwani nao wameweza kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali ili kurahisisha matumizi.Kwa upande wa Zanzibar,

  sehemu ndogo sana ambayo inatumia mti huu kama ni dawa ya malaria na sehemu hiyo ni kwa wale watu wazima wanaoishi vijijini. Wao kidogo wanatumia mti huu kama ni dawa ya kutibu malaria sugu huku ikiwa mti wa Mwarubaini unatibu maradhi ya aina mbalimbali.
  Watu wengi husikia wakisema kuwa Mwarubaini ni dawa ambayo inatibu maradhi arobaini (40) kumbe sivyo ilivyo kwani mti huu unatibu zaidi ya

  maradhi arubaini lakini tu jamii haijui na haina utaalam wa kufahamu kwa maradhi mengi yanayotibiwa kwa kutumia mti huo.
  Hivyo upo umuhimu kwa upande wa wataalamu wa tiba asilia kutoa elimu hiyo kwa jamii ili kuweza kujuwa kutumia mti huo ili kuweza kuondokana na maradhi ya aina mbalimbali.Kutokana na ufahamu huo mdogo kwa Wazanzibari katika tiba zinazopatikana kutokana na Mwarubaini, wengi

  wanapoumwa na maradhi ya aina mbalimbali na hata malaria hukimbilia hospitali kupata dawa za vidonge au sindano vitu ambavyo hutokana na mchanganyiko wa kemikali mbalimbali ambazo zinauwezo wa kusababisha madhara makubwa kwa mwili wa mwanadamu.
  Miongoni mwa dawa ambazo zina madhara yanayoweza kumpata mwanadamu ambayo husababisha na vidonge au sindano

  hizo ni pamoja na Fansida au Chloroquine ambapo utafiti unaonesha kuwa baadhi ya wagonjwa waliotumia dawa hizo wameathirika aidha kwa kuwashwa na mwili na wengine wameathirika na macho kwa kutumia Fansida.
  Ili kuondokana na athari kama hizo, Mwenyekiti huyo amewashauri Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutumia dawa za asili ili kuondokana na matatizo kama hayo.Hata hivyo Mwenyekiti

  huyo alifahamisha kuwa katika baadhi ya maradhi badala ya kutumia pesa nyingi kwa kununua dawa za kemikali ambazo bei zake zinapanda siku hadi siku ukilinganisha na dawa za asili ambazo bei zake ni nafuu.
  Hata hivyo aliwashauri wagonjwa kufuata ushauri wa kitaalamu kabla ya kutumia dawa hizo ili kuzidi kuboresha afya na kujiepusha na matatizo yasiyo ya lazima.Majani ya mti wa Mwarubaini

  yanatumika kwa kutibu maradhi mbalimbali kama vile homa za watoto, suruwa na kwa upande wa watu wazima hutibu malaria, muwasho, maradhi ya moyo, Ukimwi, mkanda wa jeshi na maradhi ya buba.
  Mengne ni maradhi ya ganzi ya mwili, kisukari na mtu ambae anaupungufu

  wa kinga mwilini, mapele sugu yalioshindikana kutibika hospitali na maradhi mengine.
  Dk. Mayasa pia alifahamisha majani hayo yanauwezo wa kuuwa hata kwa upande wa wadudu wa shambani ambao wanakula mazao.Mbegu za Mwarubaini zinatengenezwa mafuta ambayo

  mafuta hayo yanajulikana kwa jina la (Neem oil) ambayo yanauwezo wa kutibu maradhi ya aina mbalimbali kama vile kuondoa chunusi, mapele, fangasi na mabaka mwilini.
  Pia mafuta hayo huuwa wadudu mbalimbali ambao wanatambaa na kuruka nyumbani na hata vijidudu

  (bacteria), sisimizi na wadudu wengine.
  Mizizi na magome ya mwarubaini huuwa wadudu wa aina mbalimbali kama vile funza, maradhi ambayo huwapata wanawake kama vile vikanga na maradhi mengine mengi ambayo ni maradhi sugu na yameshindwa kutibiwa basi

  Mwarubaini huyatibu.
  “Kwani hata wanyama tunaofuga nyumbani mfano ng’ombe na wengine ambao hugandwa na kupe na wadudu wengine, mnyama huyo ukimkogeshea maji hayo uliosaga magome ya mti huo huondoa wadudu wote”, alifahamisha dk. Mayasa.Mtaalamu huyo alifahamisha kuwa dawa za mti huo hazina madhara kama zilivyo dawa nyengine za kemikali lakini kwa ushauri unatakiwa kumuona

  daktari mwanzo alio karibu nawe kabla ya kuanza kutumia.
  Alifahamisha kuwa dawa za kemikali zinatibu haraka kuliko dawa za asili lakini dawa za asili ni bora zaidi kuliko dawa za kemikali kwani zinatibu kidogo kidogo na zikitibu zimetibu na hazina maradhi yanayosababishwa na dawa hizo. Mwarubaini Mmea Mjarabu Kutibu Maradhi Mbalimbali | Ministry of Health Zanzibar
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ila huu mti/majani ni mchungu sana!! Hasa sie tunaochemsha na kunywa, labda hayo mafuta sijajua bado
   
 3. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  waluga luga wa jf wanajua maana ya neno mjarabu
   
Loading...