Mwarobaini wa kudhibiti kubambikiziwa bili ya maji waja

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,277
9,912
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Anthony Sanga kutoa taarifa kwa mamlaka zote za maji nchini kuanza kutumia mfumo wa malipo kabla ya matumizi (LUKU) ili wateja walipe maji kutokana na matumizi yao.

Aweso amesema hayo leo Mei 31,2021 mkoani Arusha, wakati akitembelea miradi mikubwa ya maji inayosimamiwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (AUWSA)

Amesema endapo mfumo huo utaanza kutumika utasaidia kuweza kupunguza malalamiko kwa wananchi.

“Lazima tuanze na mfumo wa Luku na tutaanzia kwa viongozi na taasisi za serikali ili tutapata uzoefu na kujifunza ndipo twende kwa wananchi,“ aliongeza.

Aweso amesema wamenunua mitambo katika baadhi ya mamlaka za maji ili kuweza kuona malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa kwa wananchi kama ni kweli na kupunguza ubambikizi wa bili za maji.

Sambamba na hilo, pia Aweso amewaagiza mamlaka za maji kote nchi kupitia kwa wasoma mita za maji kuhakikisha wanaposoma mita za maji wanaweza kuwashirikisha wananchi ili waweze kufahamu kiasi cha maji wanachokuwa wametumia .

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema miradi ya maji inayotekelezwa katika wilaya hiyo imekuwa na mafanikio makubwa.

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Arusha, Justine Rujomba amesema tayari wameshatekeleza miradi mingi ya maji na mpaka kufika Septemba wananchi wote katika Jiji la Arusha watakuwa hawana shida ya maji.
 
Imekaa vzr Sana hiyo na kuna siku waziri alishangazwa kwanini kila mamlaka Ina Aina yake ya meter nikajua kwanza angerudisha mfumo wa kutumia card maalum km zamani msoma meter akija anaandika pale na mwenye nyumba Ana saini kabisa Hili la mfumo wa luku tuone kama utekelezaji wake utachukua muda gani.
 
Back
Top Bottom