Mwarobaini wa ajali za usafiri wa vyombo vya majini huu hapa

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
serikali inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vinavyotokana na ajali za usafiri wa vyombo vya majini endapo itaanzisha utaratibu wa kulazimisha vyombo vyote vya usafiri wa majini viwe na life jackets zitakazovaliwa na abiria wakati wa safari kama ambavyo abiria wanaosafiri kwa kutumia mabasi wanavyolazimika kufunga mikanda wakati wa safari. Utaratibu huu wa sasa unaotumika wa kufungia life jackets chache stoo na kusubiri ajali itokee ndipo watu waanza kugombania maboya machache yaliyopo utaendelea kugharimu maisha ya wananchi wengi. Serikali sasa inapaswa kusimama kidete na kuhakikisha vyombo vyote vinavyosafiri majini vinakuwa na life jackets za kutosha na kuhakikisha abiria wote wana hamasishwa kuvaa life jackets kabla ya kuanza safari.


Nawasilisha.
 
Basi rekebisha kichwa cha habari, ni kweli nafasi ya kupona inakua kubwa zaidi kama makoti ya kuokoa maisha yapo kwa wingi na yanapatikana kwa urahisi pindi ajali itokeapo. Lakini kwa namna yoyote ile siyo "mwarobaini" wa ajali za meli. Makoti hayo ni muhimu tu ajali inapotokea, sasa sijui ni mwarobaini kivipi.

Mwarobaini wa ajali za meli ni kama vile kutokujaza abiria na mizigo kuliko uwezo wa chombo husika, ukaguzi wa mara kwa mara na kukomesha rushwa kwa maafisa wa SUMATRA.
 
Back
Top Bottom