Mwapachu: Naunga mkono dawa lakini siyo za wafanyabiashara wapuuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwapachu: Naunga mkono dawa lakini siyo za wafanyabiashara wapuuzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 28, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Upinzani wa mashirika ya kiraia kuwa sera ya kupambana na bidhaa bandia katika Afrika Mashariki inawez kusababisha kuzuia dawa za bei nafuu na halali zinayotengenezwa kwa leseni una lengo la kuzusha hofu miongoni mwa watu "wasiokuwa na utashi mpana" katika kanda. Hayo ni maoni ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Juma Mwapachu kama alivyoeleza katika mahojiano na Wambi Michael wa IPS.
  [​IMG]Mwapachu


  WANAHARAKATI wameonyesha wasiwasi wao kuwa sera za kitaifa na kikanda za karibuni na miswada ya sheria itanyima Waganda, Wakenya na wananchi wengine wa Afrika Mashariki fursa ya kupata dawa za bei nafuu na salama zinazofanya kazi na bora ambazo hutengenezwa kwa leseni ambazo ni zinazotumiwa katika kanda hii.

  Wakati akishindwa kuthibitisha ni kwa jinsi gani wasiwasi wa dawa zinazotengenezwa kwa leseni utakuja kudhibitiwa katika sera ya EAC na sheria za bidhaa bandia, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Juma Mwapachu anasisitiza kuwa serikali za Afrika Mashariki hazitakiuka maeneo ya haki miliki yanayohusiana na biashara ambayo yanaruhsu nchi zenye maendeleo duni (LDCs) kubadilika kirahisi kuhusu haki miliki na dawa.

  Swali: Wasiwasi wa mashirika ya kiraia ni kwamba sera inayopendekezwa inaonekana kuja kuingiliana na uwezekano wa mabadiliko kama ulivyotolewa na mkataba wa Shirika la Biashara Ulimwenguni wa TRIPS.

  Jibu: Ninakuambia kuwa hatupo mahali popote pale karibu ya kupeleka muswada katika Bunge la Afrika Mashariki. Kwa sasa upo kwa washauri wataalamu. Kwa bahati mbaya, sijaona rasimu ya muswada.

  Swali: Nimeiona na tatizo ni kwamba sera na muswada unaonekana kupendekeza mambo mengine badala ya afya ya umma.

  Jibu: Mimi kama katibu mkuu naweza kukuambia kuwa sijaona rasimu ya muswada. Kwa hakika, ilikuwa tu (Aprili 26) uliletwa kwangu. Hii ni kutokana na kushiriki katika mkutano wa kilele wa Mfuko wa Mazingira ya Uwekezaji (ICF) jijini Dar es Salaam Mei 3 na 4 (ambapo suala la bidhaa bandia lilikuwa katika ajenda).

  Nilitaka kuanzia pale tulipofikia. Lakini hata sijaupitia. Hata mwanasheria wangu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hajauona muswada. Hivyo, tunazungumzia nini hapa?

  Swali: Ni jukumu gani ICF imekuwa nalo katika mchakato huo? Inadaiwa kuwakilisha maslahi ya makampuni ya kimataifa yanayopinga upatikanaji wa dawa zinazotengenezwa kwa leseni.

  Jibu: Huo ni uongo unaoenezwa na wale wanojiita vyama vya kiraia. Tuna uhusiano wa kikazi na Mfuko wa Mazingira ya Uwekezaji ambao unakwenda zaidi ya sera na kupambana na bidhaa bandia. Katika kushirikiana na ICF tumekuwa katika mradi mwingine kufanya sheria za biashara za nchi wanachama zifanane wakati tunapojiandaa na soko la pamoja.

  ICF imeandaa orodha ya sheria kama hiyo. Hadi sasa sheria 45 za biashara, usajili wa biashara, uwekezaji, bima na benki zimeshabainishwa na washauri wataalamu. Hawajavutiwa tu na sheria zinazopambana na bidhaa bandia, kama inavyoonekana kupendekeza.

  Swali: Wasiwasi ni kwamba sera walizowahi kufadhili zinaweza kuondokana na hali ya kubadilika kirahisi ambayo LDCs zinapaswa kufaidika chini ya TRIPS wakati linapokuja suala la usajili wa majina ya biashara na upatikanaji wa dawa.

  Jibu: Wanachama wetu wote wamesaini mkataba wa WTO (Shirika la Biashara Duniani). Hakuna jinsi kwamba tunaweza kuwa na sheria ya kikanda ambazo zinaingiliana na sheria za kimataifa. Usisambaze hofu miongoni mwa Waafrika Mashariki, hasa wale ambao wanaugua ugonjwa huu (wa Ukimwi). Hii inasababisha hofu zisizokuwa na msingi. Hatuna watu wanaofikiria mambo kwa undani.

  Swali: Una imani kuwa dawa zinazotengenezwa kwa leseni zinapaswa kuachwa katika fasili pana kama ilivyo katika rasimu ya sera na muswada wa EAC?

  Jibu: Hatutakuja kukiuka TRIPS, ambayo iko wazi katika dawa zinazotengenezwa kwa leseni. Tutawezaje kukiuka sheria ya kimataifa ambayo nchi zetu zimesaini? Haiwezekani.

  Swali: Je, kuhusu dawa zinazotengenezwa kwa leseni?

  Jibu: Naweza kukuhakikishia kuwa tutazingatia sheria za kimataifa, hasa TRIPS. Natumia dawa zinazotengenezwa kwa leseni kwa sababu siwezi kununua dawa za kampuni halisi. Hivyo nitakuwa mtu wa mwisho kuzuia uingizwaji wake.

  Naunga mkono mipango ya upatikanaji wa dawa lakini siyo zile zinazosambazwa na wafanyabiashara wapuuzi ambao wanafanya mahusiano na wauzaji waliojificha na kuleta panadol extra, ambayo ni chaki au metakalfin ambayo siyo metakalfin halisi. Wanataka kuua watu wetu. Hapana, hapana, sitaruhusu uingizaji nchini wa bidhaa hizi bandia na kuangamiza maisha ya watu wetu.

  Mwapachu: Naunga mkono dawa lakini siyo za wafanyabiashara wapuuzi
   
Loading...