Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,797
- 730,110
Mko pale ubungo bus terminal mnasubiri bus la mkoani, linakuja bus jipya kabisa zuri na la kuvutia mnafurahia na kupanda kwa kuridhika mno safari inaanza
Lakini anatokea abiria na kutoa angalizo kuhusu dereva na wasaidizi wake kuwa walikuwa wafanyakazi kwenye bus la zamani na walifanya makosa mengi....!abiria huyu anapingwa kiasi hata cha kuzomewa
Mwanzo wa safari huwa mzuri lakini huko njiani kuna mashimo milima kona mbaya miteremko nk nk...kufika salama safari pamoja na kudra za Mwenyezi Mungu lakini umahiri na umakini wa dereva ni muhimu mno
Magufuli alianza vema sana safari yake barabara pana nzuri lakini sasa gari imeshatoka nje ya mji inakata mbuga barabara imeshaanza kuwa mbovu na tabia za watendaji wake aliowaamini sasa zishaanza kuonekana dhahiri
Kama konda alikuwa mwizi kwenye bus la zamani hata kwenye hili jipya hawezi kuacha
Team ya Magu imeshaanza kuchokonolewa wanaotumbuliwa majipu bado walikula na wateule wa sasa wa rais...nani atakubali kuumia pekeyake wakati aliyekula naye anapeta? Ni mwendawazimu pekee anaweza kupotezea
Yalianzia kwenye flow meter, yakaja ya katibu mkuu ikafuatia uteuzi na utenguzi wa NSSF, leo kinachoendelea huko mitandaoni ni tuhuma za watoto wa mzee Makamba
Gari la Magu limeanza kupita vipande korofi vya barabara!wasaidizi wake wameanza kujenga chuki za kimya kimya wanaona si dereva mzuri si dereva mahiri anaharibu mambo....ila wanasema kichinichini na kisirisiri...waliotumbuliwa majipu nao wana chuki zao...ugali umetiwa omo ulaji umeharibiwa, mtandao wa wapigaji ulikuwa mkubwa mirija imezibwa watu wanaugulia kimyakimya
Hili ndio kundi baya na hatari kwa Magu , linafanya kila mbinu kuonyesha maovu ya wateule wako na wanasubiri kuona reaction yake....maamuzi yake yoyote yatakuwa na impact kubwa sana huko mbeleni kama kweli anaweza au la
Mwanzo wa safari huwa mzuri....kufika ni Majaliwa...je tutafika salama? ???