Mwanzo wa mwisho wa michango mikubwa ya sherehe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanzo wa mwisho wa michango mikubwa ya sherehe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kivato, Dec 30, 2010.

 1. k

  kivato Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE  Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe kubwa inavyozidi kushika kasi, ikipelekea ule wigo wa kuomba michango kupanuka kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza kukuomba mchango.  Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo wanaochangiwa na kulazimika kulipa michango hiyo kwa miaka mingi. Je, wajua kuwa kuna familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze mashamba au mifugo mtaji ili kupata fedha za kuchangia sherehe?. Je, wajua kuwa kuna watu ambao zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia kuchangia sherehe na huku wakishindwa kulipia huduma muhimu kama shule, matibabu, lishe, nk. Na kuwa wakati mwingine wewe au mimi (au wengine kama mimi na wewe) ndio wenyeviti na makatibu wa sherehe hiyo?. Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia milioni 30 au zaidi kwenye sherehe usiku mmoja?


  Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amwekwama kwenda. Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii si hadithi, ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia.


  Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na huu mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi kubwa (na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia mambo ya msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe. Wengi wanaamini kuwa tumeshatumbukia kwenye lindi la mazoea ambapo hatuwezi kujitoa mpaka upepo uje ubadilike wenyewe!.


  Mimi nafikiri wasomi tuna jukumu muhimu la kuwa chachu ya mabadiliko pale ambapo mazoea yenye madhara yanavuka mipaka na kuweza hata kuwa chanzo cha ufukara na kuviza maendeleo.


  Ili kubadilisha hili jambo, lazima tuanzie mahali. Mimi napendeleza na kuanza kutekeleza. Kuanzia Januari 2011, nitapunguza michango ninayotoa. Nitatoa tu kwa mtu wa karibu sana, na nitachanga kidogo. Usishangae nikakuchangia 20,000/= kama ulitegemea 50,000/= kwa mfano. Kuanzia July 2011, nitaacha kabisa kuchangia sherehe. Badala yake nitakuwa nachangia elimu pale ambapo mzazi hayupo au mhusika kweli hana uwezo na pia nitachangia miradi mingine ya jamii na maendeleo.


  Je waniunga mkono? Kama ndiyo sambaza huu ujumbe kwa mtandao wako.
   
 2. tama

  tama JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 604
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,493
  Likes Received: 2,738
  Trophy Points: 280
   
 4. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  I think Author na Original Source ni Dr. Olomi wa UDSM.

  Ikiwezekana ni vema ku-aknowledge.
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,562
  Likes Received: 3,858
  Trophy Points: 280
  Ndivyo tulivyo!

  mtoa maada anyecontrol michango siyo wewe ni -ukaribu wa familia tulionao! unapokuwa na sherehe inakuwa siyo yako ila ya jamii! ni kansa mbaya ambayo ku-remedy ni kuanza kama ulivyosema, mimi nafuatia.
   
 6. p

  p53 JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  vipi na wale wanashindwa kumchangia mgonjwa ambaye anaweza kuwa ndugu/jirani/jamaa,apate matibabu mazuri,ili ikiwezekana apone,lakini akifa wanakuwa wa kwanza kutoa michango,tena mikubwa mikubwa na hata kununua sanduku la kifahari na ng'ombe 'wa shughuli'??
   
Loading...