Mwanzo wa mwaka wa fedha 2011/12 na kupanda gharama za vitu kwa ghafla

BUBE

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
846
253
Wanajamvi.
Nilimsikiliza mh Mkulo wakati wa mawasilisho ya bajeti. Bidhaa kama dizeli, petrol ziliondolewa kodi wakati mafuta ya taa kodi ziliongezwa/rudishwa. Cha ajabu, wauza mafuta tangu juzi tar 2/7 wamepandisha mafuta ya taa hadi Tshs 2000 wakati huo huo mafuta ya dizeli na petrol ama bei imebakia vile vile na pengine imepanda kidogo. Uchunguzi wangu nilofanya Dar na Dodoma unadhibitisha hivyo. Je inawezekana mzigo wa mafuta ya taa ulopandisha bei ni ule uliofika tareh 1 Julai? Je TRA wanaweza kutuambia kama wali-clear uingizaji mafuta tarehe 1/7 na siku iliyofuata yakawa sokoni? Mbona mabadiliko haya ni kwa mafuta ya taa kupanda wakati yale mengine hayashuki kama tulivyoahidiwa?
Pili, hapa Dodoma maeneo mengi hadi siku ya Ijumaa jioni walikuwa wanauza bundle 1 ya bati geji 30 kwa shs 238,000. Jana Jumamosi saa 4 bei imebadilika ghafla maduka ya bati hadi sh 245,000!
Wana jamvi ni nani anaweza kuwa na majibu muafaka kwa hili?
 
Back
Top Bottom