Mwanzo wa meditation

Nafikiri Mkuu Rakims Hapa Ndio Ungeendeleza Darasa Hili Kwa Ufasaha Zaidi Maana Kule Kwenye Uzi Wa Psychic Powers Kuna Viherehere Wanatuchafulia Nafikiri Ungehamishia Somo Upande Huu Ili Wanaoleta Udini Tuwape Dawa Yao Kabisa Waache Kutusumbua,ni Ushauri Tu Natoa Angalia Namna Nzuri Ya Kufanya Mkuu
Asante
 
Chapter 2:

"Maajabu Ya Koo La Chakula Au Kidaka Tonge"

"Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno, Nae Neno Alikuwa Kwa Mungu Nae Neno Alikuwa Ni Mungu" John 1:1

"Na Alikuwa Na Nyota Saba Mkono Wake Wa Kulia, Na Nje Ya Mdomo Wake Kulikuwa Na Upanga Mbili Zilizokali"
Revelation 1:16


2:1 Msuguano Wa Koo

Hili Ni Zoezi Ambalo Pia Baadae Husaidia Kuamsha Jicho La Tatu, Chini Kidogo Ya Koo La Chakula Kwa Nyuma Mtetemeko Wake Unatokea Unapopumua Ndani Au Nje Hutokea.. Huunda Kiupepo Aina Ya Sauti.. Sauti Hiyo Yaweza Kuwa Humming Au Buzzing, Sauti Hiyo Yatakiwa Iwe Ile Ile, Wakati Wakuinhalling na exhalling.. Kama Utaweza Jaribu Kutumia Sauti Ndogo: Itakuwa Ni Rahisi Kukufanya Uweze Kufanya Kwa Muda Mrefu, Kabla Sijatoa Mbinu Za Kufanya Throat Friction... Ngoja Niwawekee Pointi Chache Ambazo Ni Sahihi Zaidi..

Usifanye Na Usianze Jitihada kwa Throat Friction Iliyo Kamili..
Fanya Tu Kiaina Iache Yenyewe Itajisogeza Na Muda..
Kama Ukijaribu Kuifanya Kikamilifu Na Kwa Jitihada Zaidi Basi Mwisho Wake Utakuwa Unakosea Kabisaa...
We Pumua Tu Nje Ndani Kwa Sauti Za Ajabu Ajabu Utaona Zenyewe Zinajipanga Sawiya..

Zifuatazo Ni Mbinu Za Kucheza Na Throat Friction Next Time Tutaunganisha Third Eye Na Throat Utaona Mambo Yanavyoenda Poa..

Ukitaka Uende Fasta Fasta Itabidi Utafute Chuo Pale Utakuta Vitabu Vya Kila Aina Vya Throat Friction Sounds Za Kila Aina Lakini Never Loose Hope Wakuu "Wherever Theres A Will Theres A Way"

Kule Waweza Kukuta Aina Nyingi Za Sauti Za Throat Friction Lakini Tambua, Sauti Yoyote Inafaa Kukuwezesha Kuamsha Jicho La Tatu..

Haijarishi Utapumulia Mdomo, Pua Au Vyote Kwa Wakati Mmoja.. Mdomo Tu Unatakiwa Uwe Wazi Kidogo Taya La Chini Liwe Limekosa Mtetemo Na Limetulia.. Ili Sasa Uweze Kupata Mtetemo Utakao Fikia Consciousness Yako..

Chukulia Mfano:
N - sehemu ya juu kwa nyuma ya koo la chakula,

F- Eneo La Mdomo Kwa Mbele

M- Eneo La Kati Hapa Kabla Hujafikia Matundu Ya Pua

L- Eneo La Nyuma La Koo ambapo msuguano hutokea


Msuguano Wa Koo Ni Sahihi Zaidi Ukitokea Eneo L Nyuma Ya Koo. Usitokee mbele Eneo La M, wala Eneo Karibu Na Mdomo Kwa Mbele F, 0‰4kitoa Sauti Yako Kuitengeneza Kwa Eneo F Au M Basi sauti Itakuwa Kubwa Na Huwezi Kuivuta Kwa Ndani,
Sauti Inayotoka Kwenye Eneo L Ukifanya Hata Mara Ishirini, In Out In Out Utahisi Kama Kuna Mzigo Ulikuwa Nao Mwilini Umeutua...
Kosa lingine linaloweza Kutokea Ni Kutoa Sauti kutokea Eneo Eneo N Katika Hali Hiyo Ambayo Sio Ya Usahihi sauti Itatoka Kama Mtu Anaekoroma Kwa Kutumia Pua..
Kusibitisha Hili Tafuta Watu Wawili Ambao Wakilala Wana Koroma, Muangalie Anaekoromea Pua Akiamka Kachoka Hana Raha Hadi Baadae, Mcheki Jembe Aliekoromea Koo, Yupo Fiti Ndoto Alizoota Zimemfurahahisha Mwingine Yule Hana Jipya Za Kutisha tu.. kwa Anaekoroma Kwa Vyote Yeye Huwa Hakumbuki Kaota Nini,.. Asie Koroma Akiamka Yupo Kawaida Hana Makuu Na Anakumbuka Pointi Zote Alizoota Na Mwili Upo Vile Vile,

Pia Unapoendelea Kufanya Throat Friction Utajiskia Kimtetemo Kidogo Kwenye Kidaka Tonge Kinagusa Tufaha La Adam.. Tufaha La Adam Ni Ule Uvimbe Wa Wanaume Katikati Ya Shingo.. Ipo Sana Kwa Wanaume Zaidi Ya Wanawake.. Mwanzo Mtetemo Huonekana Kupatikana Zaidi Wakati uKivuta Pumzi Zaidi Kuliko Kutoa.. Hata kama Ni Sauti Ile Ile Inayotoka, Ni Ndani Kiasi Gani Hewa Inatakiwa Iwe? inatakiwa Kuwa Kawaida Tu.. Itakuwa Ngumu Kidogo Kwa Mara Ya Kwanza, Lengo Pia Ni Kuactivate Nguvu Ya Koo Kwa Kulisugua, Lengo Sio Kupumua Staili Gani, Lengo Ni Kuamsha Nguvu Ya Koo...

Faida Ya Throat Friction Ni Kureinforce Your Connection With The 'Energy', itakuwa Ni Ya Ajabu Ajabu Kwa Wanaoanza Mara Ya Kwanza Lakini Itakuwa Zaidi Na Zaidi Ya Maana Kama Utaendelea Kuiamsha Kwa Jicho La Tatu, Kadri Utakavyozidi Kuifanyia Mazoezi Ndio Itakavyozidi Kukufungua Uweze Kucontrol Power Inayokuzunguka Mwilini Kukulinda Wakati Wa Meditation,, Faida Nzuri Ni Kutembea Na Energy Zinazokuzunguka Sio Zinaenda Kulia Wewe Kushoto...
Zaidi Unavyozidi Kuvuta Pumzi Ndani Ndio Zaidi Power Za Throat Chakra Zinavyovujishwa, mdomo Umebaki Wazi Ni Muhimu Kuhakikisha Mdomo Upo Wazi Uwazi Ambao Unaweza Kupitisha Ulimi Katikati Ya Meno Ya Juu Na Chini... Na Muhimu Taya La Chini Liwe Limetulia Kuhakikisha Haliingilii Zoezi.. Maana Hapo Utahamia Chakra Ingine.. Vibration Itakapofika Kwenye Eneo La Jicho La Tatu, Ndio Ujaribu Kuanza Kupractise Huku Umefumba Mdomo,
Wanaoanza Mara Nyingi Huhisi Makoo Yanawakauka Au Yanakuwa Mabichi Zaidi, Waweza Kutumia Asali Kula Kila Siku Mara Mbili Itasaidia Tatizo Hilo Vijiko Vi3 Vya Chai.. Baadae Kila Kitofauti Kitapotea Na Utaanza Kuwa Mjuzi Zaidi.. Hii Pia Inakufanya Uwe Na Sauti Nzuri Sana Wakati Wa Maongezi Na Utaskia Watu Wanasema Jamaa Au Yule Sister Anasauti Ya Kipekee..

Swali:
Kwanini Uvimbe Wa Koo Unaitwa Tufaha La Adam?

Jibu:
Inasadikika Pindi Ilipofika Zamu Ya Adamu Kulishwa Tunda Na Hawa(Ever/Eva) Lilimkwama Kwa Muda Na Kutokea Hiyo Alama...


2.2 Faida Na Athari Za Msuguano Wa Koo..

Msuguano Wa Koo Ni Sauti Ya Nguvu..

Inakusaidia Kuelewa Wapi Uangalie Kwenye Third Eye..

Baadae Inaweza Kukupa Uwezo Wa Kuangalia Chakra Zote, Ndio Chakra Kubwa Ya Kwanza Kujifunza, Maana Itakujuza Kwa Mtetemo Wake Kwamba Hapa Kuna Crown Chakra Uangalie Vipi Hapa Kuna Third Eye Chakra Uangalie Vipi N.k

Itaanza Kujiweka Kama Kikisu Ikiwa Unataka Kungua Chakra Fulani Itafanya Kama Shoti Eneo La Chakra Hiyo Na Wewe Kuifikia Kirahisi,..

Pia Ina Maajabu Mengine Kibao Kama Inaweza Kuku Cure Na Magonjwa na Inatengua Sumu Mwilini..

Mara Zingine Hufanya Seli Hai Nyeupe Ziongezeke Na Kukufanya Uwe Fiti Muda Wote,

Pia Ina Tabia Ya Kurejesha Baby Skin Unaweza Kuonekana Kama Kijana Mbichi Wakati Ni Kabibi...

Ni Nyingi Naachia Hapo..

2.3 Maajabu Ya Koo

Ni Kubadili Sauti Katika Historia Kuna Historia Ya Wanasauti Anasemekana Alikuwa Na Psychic Powers MbaliMBALI, Ambapo Mmoja Kati Yao Aliitwa Vac- Siddhi (vac- voice) ambapo alikuwa akisema kitu kinatokea kweli,.. Ilifika kipindi wakavamiwa Na Wandugu Wa Kiume Wa 5 Wakataka Kwa Usalama Wao Wawaoze Yule Mwanasauti Mmoja Wakamuoza Na Kumwambia Kwa Uzuri Wa Sauti Yake Hamuwezi Kuishi Nae Milele, Wakamchukua Wakasema Harusi Itafanyika Kwao Wakishamwambia Mama Yao Wakafika Kwa Mama Yao Akawaambia Wote Mmempenda Binti Huyo Hivyo Mtamuoa Wote, Wakamuoa Akawa Mke Wa Mtu 5, Kila Akiulizwa Yule Wa Kike Umekubali Kuolewa Akisema Ndio Kwa Uzuri Wa Sauti Yake Ndugu Wale Wakagombana Na Kumkosa Wote..

The creative power of the voice was clearly expressed in Sanskrit, where vac, voice is often regarded as a synonym for sakti which is the creative Energy, the power of manifestation,

Kigiliki kuna Neno Linaitwa Logos, Mwanzo Wa tafsiri logo ni word, baadae Tunakuja Kuona mwanzo kulikuwako neno nae neno........??? John 2.1)

Na Pia Tukiangalia Katika Kitabu Cha Mwanzo Mungu Aliumba Ulimwengu Kwa Nguvu ya Neno Kuumba,

"Na Mungu Akasema, Pawe Na Mwanga, Na Pakawa Na Mwanga" genesis 1:3, 1:6, 1: 24 and so on..

Kumbe Kuna Nguvu Pia Katika Maneno Yetu, Hapa Ndipo Tunampata Yesu Pia Kwa Kusema Ikiwa Mnaimani Mwaweza Kuamuru Milima Ihame..

Kusema Hivyo Sikaribishi Walokole Hapa Nimetumia Tu Mfano....
Naomba Niachie Hapo

Jinsi Ya Kufanya:

2.4 Humming Sound And The Magic Of Bees..

Kaa Katika Mtindo Wa Meditation, Mgongo Wako Ukiwa Umenyooka Sawiya, Kuwa Muelewa Kati Ya Eneo La Spine Katika Shingo, Na Kunyoosha Mgongo Inatakiwa Wote Uwe Umenyooka,

Fumba Macho Yako..
Paelewe Kwenye Koo..
Anza Kutoa Sauti Ya Kukoroma, Ifanye Koo Yako Itetemeke, Ifanye Sauti Itoke Wakati Wa Kuingia Na Kutoka Kwa Hewa,..

Fanya Kuvuta Pumzi Kwa Ufupi Na Itoe Kwa Kireefu,
Endelea Kuielewa Mitetemo Inayotoka Kwenye Koromeo Kwa Kukoroma, Endelea Kufanya Zoezi Hili Kwa Dakika Kadhaa, Halafu Ukae Kimya Na Usijitingishe.. Sikilizia Koo Linavyoendelea Kutetemeka...

To Be Continued....!

Takuja Kumalizia Halafu Tutaendelea Topic Ya Tatu,

AWAKENING THE THIRD EYE

Hiyo ilikuwa ni Awake The Throat Chakra, Tunakuja Third eye Tutaenda Crown

#Rakims
 
Nakaribisha Maswali..

#rakims

nimejaribu kufanya ya kuangalia mshumaa,nimefanya kama dakika 10 hv bt ni kama naiona image yngu mbele ya mshumaa af macho yng kama yanatoka machozi.hi imekaaje mkuu
nifanye kila baada ya cku ngp au unaweza fanya hata kila cku?
 
nimejaribu kufanya ya kuangalia mshumaa,nimefanya kama dakika 10 hv bt ni kama naiona image yngu mbele ya mshumaa af macho yng kama yanatoka machozi.hi imekaaje mkuu
nifanye kila baada ya cku ngp au unaweza fanya hata kila cku?

kwa Siku Mara Mbili, Usiusogelee Sana Mshumaa Weka Distance Kidogo, Kapua Macho Pia Inapobidi Mkuu.. Vuta Pumzi Ndefu Machozi, Unamafua Ya Ndani Yale Ukiamka Asubuhi Unakuta Pua Inawaka Moto Au Imeziba Jitahidi Kufanya Healing Meditation Mkuu Mambo Yatakuwa Sawa..

#rakims
 
Mkuu Rakims kwanz hongera sana kwa somo adhimu Nimekuwa nikifatilia mada kimyakimya tangu kwny uzi wa psychic powers, tatizo tangu nianze kufanya meditation nimekuwa mwoga kutoka nje usiku wa giza au hata kutembea pekeyangu usiku sehem zenye giza yaani nahisi kama ntakutana na makitu/spirits.

Vp Kuna tatizo au mimi mwenyewe najishtukia tu?
 
Mkuu Rakims kwanz hongera sana kwa somo adhimu Nimekuwa nikifatilia mada kimyakimya tangu kwny uzi wa psychic powers, tatizo tangu nianze kufanya meditation nimekuwa mwoga kutoka nje usiku wa giza au hata kutembea pekeyangu usiku sehem zenye giza yaani nahisi kama ntakutana na makitu/spirits. Vp Kuna tatizo au mimi mwenyewe najishtukia tu?

Still Bado Meditation Haijakuingia Vizuri, Na Bado Hujagain Psychic Powers Hizo Spirits Kuziona Bado Sana Mkuu, Huo Ni Ubongo Wako Utachange Kutokana Na Mazingira.

Ikikaribia Kuanza Kuona Aura Ndio Unakaribia Kuona Spirits Hapo Unakuwa Tayari Umeshajaa Ujasiri Moyoni Na Akilini Hata Itokee Nini Huto React Fasta Utataka Utambue Ni Nini Na Kwanini Ndio Utareact... Bado Endelea Tu Mkuu..

Rakims
 
Na hii ya kuona image yng mbele ya mshumaa je?

Hiyo Ni Third Eye Inajijaribu Lakini Bado Sana... Mpaka Takataka Ziishe Ubongoni Badala Ya Hiyo Sura Yako Utaanza Kuona Matukio Yako Clear..

Ngoja Nimalizie Somo La Jana

#Rakims
 
Inaendelea....

Baada Ya Kusikiliza Vibration Inayoendelea Baada Ya Kuacha Kuunguruma..

Hiyo Mbinu Huvunja Sumu Zote Zilizoganda Eneo Hilo La Throat Chakra, kama Itafanyika Kwa Muda Mrefu Na Wa Kutosha Huweza Kuanza Kutetemesha Kwa Mpumuo Kwenye Consiciousness. Effect Inakuwa Kubwa Na Kukufanya Upaelewe Vema Eneo La Third Eye Kwa Muda Huo Huo, Yani Unaangalia Third Eye Chakra Na Throat Chakra At The Same Time..

Njia Moja Wapo Ya Kufanya Zoezi Hili Ni Kufanya Sauti Yako Ya Humming Inakuwa Kama Muungurumo Wa Nyuki Tena Hii Hufaa Zaidi Kama Umekaa Pozi La Hatha-yoga, Kama Inakuwa Ngumu Usijali, Sauti Yoyote Ya Humming Itafaa Tu, Waweza Kupima Kama Koo Lako Linavibrate Kwa Kuweka Kidole Chako Kwenye Koo Na Kuskiliza Vibration.. Asali Nimeihusisha Hapa Kwa Sababu Muungurumo Mzuri Unaohitajika Ni Kama Wa Nyuki Nyuki Muungurumo Wake Husaidia Mmea Kukua Huku Yeye Akichukua Vichemchem Na Kuvitengenezea Asali Hiyo Ikiwa Unahisi Utofauti Lamba Asali Throat Chakra Itaamka Pia Mpaka Utashangaa.. Ukiweza Kuamsha Throat Chakra Basi Ni Rahisi Sana Kufungua Third Eye Kwa Msaada Wa Throat Chakra...

Honey, Interestingly Enough, Has Always Been Considered An Excellent Remedy For The Throat, And Bees A Symbol Of Eloquence. in Hebrew One Of The Words For Voice Is Dibur, Coming From The Root Daber That Gives The Verb Ledaber, To Speak. and Bee Is Dvora, coming From The Same Root.

(the Name Deborah Comes From The Hebrew Dvora, bee.)

Next Time Tutaendelea Na Kuamsha Jicho La Tatu

Chapter 3:
Awakening The Third Eye

3.1 Jicho La Tatu Ni Nini?

3.2 Kufungua Kwa Mara Ya Kwanza.. Phase ya 1 hadi ya 6

3.3 Uzoefu Mbali Mbali...

3.4 Marejeo Ya Uzoefu

3.5 Kama Hujahisi Vibration Yoyote Baada Ya Yote

3.6 Zaidi Kuhusu Jicho La Tatu..

3.7 Taamuli Ya Jicho La Tatu
Phase 1-4.. Mwanga machoni,mtetemeko katikati ya nyusi,nafasi, mtetemeko kwenye koo viungane.. N.k

3.8 Muungurumo Zaidi

3.9 kupangilia mazoezi

3.10 mysteries of the space

Ndio Tuingie Topic Ya Nne Channel Release..

Mmmnh! Parefu Wakuu Hadi Naona Uvivu Kuendelea...

#Rakims
 
JINSI YA KUFANYA MEDITATION
Meditation:
Ni ile hali wakati mawazo yanapokuwa yameyeyushwa na kufikia mahali ambapo hakuna fikra yenye kuingia tena.
¡¤ Wengine wanaielezea tahajudi kwamba, ni sala za usiku wa manane.

FAIDA ZA MEDITATION
1. Husaidia kuratibu msukumo wa damu pamoja na usafirishwaji wa damu mwilini.
2. Husaidia pumzi pamoja na kurahisisha usagwaji wa chakula mwilini.
3. Husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini.

4. Husaidia kuleta furaha ya nafsi.
5. Husaidia kuimarisha nguvu yako ya machale pamoja na nguvu zako za ziada.
6. Husaidia kutibu matatizo mengi ya kisaikolojia kwani hubadili hali ya mfumo wa fahamu na mawazo (endapo itafanywa kila siku).
7.meditationpia inaweza kutumika kuomba kitu unachohitaji,kamavile kazi au mahitaji mbalimbali,
Hatua zinazotakiwa wakati unajiandaa


Kufanya meditation ni kamai fuatavyo:
1. Tafuta sehemu iliyotulia, isiyo na makelele. Kaa kwenye kiti au chini, au lala kitandani. Hakikisha huumii mahali popote. Legeza mwili wako pamoja na misuli yote ya mwili wako kwa kadri utakavyoweza.
2. Sahau matatizo yako yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Sahau matatizo yako ya kazini au nyumbani. Jitahidi usifikirie chochote.
3. Ni muhimusanakujali hisia zako wakati unafanya tahajudI.
4. Pumua kwa kuingiza pumzi ya kutosha mapafuni, halafu toa pumzi yote na kufanya kifua kiwekamakitupu. Weka mawazo yako yote kwenye pumzi zako
.
Aina za :meditation
1.meditation ya pumzi.
Ni kongwe zaidi. Ilianzia china naIndia. Ni tahajudi nzuri au muhimu kwa wale wanaoanza kujifunza.
2.meditation ya mkono:
Hii inakuonyesha ni kwa jinsi gani mawazo yako yana nguvu zaidi kuliko mwili. Lakini pia inakuonyesha uhusiano uliopo kati ya mawazo yako na mwili wako.
.
3.Tahajudi ya namba:
Hapa, unatakiwa kuhesabu namba kinyumenyume huku ukiwa umefumba macho. Unaweza ukaanzia 100, 99, 98, 97, 96, ¡-mpaka 1, au unaweza kuanzia 200, 198, 196, 194, 192, ¡-mpaka 2. hakikisha wakati unahesabu namba hizi hukosei, na ikitokea ukakosea namba yoyote hata
kamaumekaribia kumaliza, itakulazimu kuanza upya. Tahajudi hii ni nzurisanakwa kurejesha kumbukumbu, ingawa pia ina faida nyingine.

Hizo ni baadhi ya tu ya aina za meditation.... By Rakims

Umefanya vyema sana kuanzisha huu Uzi.
 
Ni lazima kukaa mkao wa meditation X style??? Maana wengine huo mkao haiwezekani vp kulala?? Au kama ntaegamia kitu..... Leta majibu mwl. Rakims.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom