Mwanzo wa binadamu, maswali ni mengi kuliko majibu…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanzo wa binadamu, maswali ni mengi kuliko majibu…!

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Mtambuzi, Oct 3, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katika dini tulifundishwa kwamba binadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa Adam na Eva, na nilipokuwa shule, napo nilifundishwa kuwa chanzo cha binadamu ni nyani, halafu akawa anabadilika hadi kufikia kuwa binadamu.

  Lakini bado kuna Maswali najiuliza, hivi ni kwa nini, nyani wengine wamegoma kubadilika hadi leo? Yaani wamebaki kuwa nyani badala ya binadamu.
  Je na sisi kwa nini tumesita kuendelea kubadilika?

  Kama tulikuwa kama nyani, halafu tukabadilika na kuwa binadamu, inakuwaje tusiendelee kubadilika zaidi na zaidi? Au kulikuwa na mipaka ya kwamba tukifikia mabadiliko kama haya tuliyonayo iwe ndio basi?

  Kama ingekuwa binadamu aliumbwa kama nyani na kubadilika kufuatana na mazingira labda na mambo mengine, mbona basi leo hii uhusiano wa kinasaba kati ya binadamu na nyani sio mkubwa kama ule uliopo kati ya binadamu na panya weupe?

  Yaani wale panya wanaotumika kufanyia utafiti masuala mengi yenye kumgusa binadamu, kwani kinasaba, panya hawa wanakaribiana na binadamu.

  Basi kuna haja ya kuamini kwamba binadamu wa kwanza alikuwa ni panya kisha akabadilika na kuwa kama alivyo leo. Lakini bado najiuliza kwa nini huyu panya asiendelee kubadilika, amefungwa na kitu gani?

  Hivi karibuni wakati naperuzi peruzi katika mtandao nimekutana na mijadala mikali kuhusu asili ya viumbe hai. Kwa mfano nchini Marekani mjadala huu umeingia mashuleni ukiwa na nguvu mpya, kutokana na vijana wengi nchini humo kupambazukiwa na kukataa kukaririshwa elimu za wanasayansi wa kale zisizo na mashiko.

  Vitabu vingi vya Baiolojia vilikuwa vikisema kwamba asili ya viumbe hai ni mwendelezo wa mabadiliko (Evolution). Walimu wengi wa nchini Marekani na Ulaya ambako jambo hili limeshika nguvu wanapinga nadharia hii ya mabadiliko na wanaamini kwamba viumbe hai viliumbwa na kitu, jambo au nguvu yenye akili. Wataalamu wa mabadiliko nao wanapinga na kusisitiza kwamba nadharia yao ni ya kisayansi na ya wale wanaopinga ni ya kidini.

  Hivi sasa hata wale waumini wa nadharia ya mabadiliko iliyoasisiwa na Charles Darwin wameanza kuitilia mashaka nadharia hiyo kiasi cha kuitupilia mbali ili kutafuta nadharia mbadala.

  Kwa mfano, Mwanabaiolojia mashuhuri kutoka nchini Sweden, Sren Lvtrup, ameweka wazi kwamba, anaamini siku moja nadharia hii ya Darwin ya mabadiliko itakuja kuwekwa wazi kwamba ni nadharia ya uongo kupita kiasi katika historia ya sayansi.

  Lakini Nadharia hii ya mabadiliko inaendelea kufundishwa katika mashule yetu ambayo yanahudumiwa na kodi za walalahoi, huku nadharia hii ikiendelea kutiliwa mashaka kila uchao.

  Kwa kuwa nadharia ya kidini ina msimamo wake tofauti na ule wa sayansi, sasa kwa nini wanafunzi wasifundishwe nadharia zote mbili, kila moja ikiwa na ushahidi wake ili waweze kupembua ubora na udhaifu wa kila nadharia na kuwawezesha kwa ridhaa yao wenyewe kuamua nadharia ipi kati ya hizo mbili ina ushahidi bora kuzidi nadharia nyingine?

  Bado napata kizunguzungu katika kujadili hii mada, kwani kila ninavyozidi kutafuta ukweli nakutana na nadharia zinazopingana, ingawa kila moja haitoi ushahidi unaojitosheleza.

  Je wenzangu mnayo maoni gani juu ya hili?
   
 2. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  ndugu yangu mtambuzi binadamu wa kwanza alitokana na nini ni swala ambalo linamaelezo lukuki kutokana na aina ya elimu mtu aipatayo. Microbiologist akikuelezea mwanzo wa kitu kiitwacho uhai utabaki kinywa wazi lakin mwisho wanatuonyesha kwamba binadamu alitokana na masokwe kwamaana kwamba hata genus yetu ni moja ishu ni kwamba specie tutatofautiana.

  ukitaka kuamini hili basi leo hii kama tukikosa kabisa damu ya group A+ tunaweza kuichukua kwa sokwe mwenye group iyo na mgonjwa akaekewa pasi tatizo lolote lile. hivyo kiuumbaji wa Mungu aliumba vitu kwa makundi yake na katika makundi yale mwadamau alipoambiwa avipemajina alivipa kwa utash ambao Mungu aliuweka kwake. na kiukweli si kwamba dhana ya evolution ni nadharia hii ni kweli ila tu huwa inachukua miaka mingi sana hadi kuja kuonekana. kwamfano tunaweza kuchukua karnre moja kushuhudia mabadiliko ya kitu kimoja. na hii iko influenced na mambo mengi sana dunian achlia mbali uumbaji wa kawaida bali hata mazingira na nafasi ambayo kiumbe husika kinaish.

  mathalan waweza kumkuta samaki nile perch akiwa na hata kg 30 ndani ya ziwa victoria lkn samaki huyo huyo akashindwa kufikisha uzito na ukubwa huo pale nyumba ya Mungu hata kama kote hakutavuliwa kwa muda fulan let say for 3 months. sababu kubwa hapa ni mazingira na nafasi. wale wa ziwa victoria watakuwa kwa kasi kwasababua ya vyakula na space nzuri ya kuruhusu miili kutanuka wakati hawa wa nyumba ya Mungu watazaliana wengi sana ila kwa maumbo madogo kwasababuaa ya food competition na space ya kujidai.

  hali hii unaweza hata kuikuta kwa binadamu wanaokaa along rift valley wao wanakuwa na lean body na quick strides ukilinganisha na vibushuti wanaotoka sehem za milimani na ndio maana kwa Tz wakimbaji wazuri wa mbio ndefu ni watu kutoka meru, singida kondoa na wale wa sprint ni watu wafupi wenye bold shapes hasa kutoka mbeya.

  vilevile technology advancement imekuwa kikwazo kwa sisi kutoshuhudia mabadiliko ya kimaumbile simply kwasababu mwanadamu anaweza kutengeneza mazingira ayatakayao akwa wakati wake. mfano vyura wa kihansi walipokuwa pale kihansi waliakuwa wanazaa na kunyonyesha pasi tabu yyte ile but walipaokuwa disturbed walitowekana baadae improvisation ikafanyika ahuko US by mimicking maisha ya hao vyura pale kihansi ili vyura wapelekwe waendelee kuzaliana but hili halikufaanaikiwa kama tulivyo tarajia na baadhi yao awalirudishwa tz. sasa kwa namna hii definately hatutaweza kusoma mabadikliko yyte kwani ytayari ile nature ya kiumbe imesha kauwa disturbed kwa kiwango ambacho hakuna awezaye kukipima especially when it comes to genetics.

  think of today scientist are talking of nanotechnology, na ndani yake kuna fields kama nanomedicine, nanoarchtech, nano engineering and so forth ambapo sasa badala ya kutumia vitu vikubwa kutatua tatizo tunataka kutumia vitu vidogo almost at nano scale ili kutatua tatizo sasa haya yanaweza yakatuletea madhara kwa namna moja ambayo yatatufanya tusiosbserve mabadiliko kabisa. hebu fikiria sasa hivi wanasayansi wanalenga kumfanya mtu badala ya kutibiwa letsay na 250 or 500 mg za dawa akatumia just nano scale of it ili kutibu ugonjwa unaomsibu sasa je wategemea kwa stail hi uone mabadilikoa aliyoyalenga darwin ama mabadiliko yatokaanayo na technolojia?
   
 3. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi nimependa mwalimu gfsonwin alivyochambua hapo juu..kwa kuangalia upande wa science na dini...but binafsi yangu naomba nistick kwenye uumbaji wa Mungu..kwamba binadamu tuliumbwa hivi tulivyo from the begining na hakuna evolution iliyotake place..Ila hapa napo ndio nashindwaga kuelewa.. mfano kama waliumbwa wanadamu wawili..je hizi races zimetoka wapi?..mbona hakuna sehemu inaonyeshwa kuwa hapo ndio mwanzo wa binadamu kuwa na rangi za ngozi tofauti??..Ngoja wajuzi waje watusadie...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  races ni matokeo ya geneology, iko hivi genes ziko influenced geographically na hii ndo sababu kwenye kila eneo kuna aina ya watu wake. kama ilivyo wachaga ni weupe ukilinganisha na wanyakyusa, kadhalika wazungu ni tofauti na wahindi ama waarabu ama waafrika. na hata hivyo africa ukiangalia weusi wa wasomali ama warundi uko tofauti na watu wa east africa. hata iweje msomali akiish tanzania atazaa msomali tu mpaka tu na hata mzungu atazaa mzungu tu.

  geneticaly genes zinazocontrol color ziko tofauti na hata matching yake ili kutengenenza melanin ni tofauti. kuna namna ambavyo huwa zinafanya matching na hili ni somo refu sana and siwez kulielezea vizuri hapa kwani nahitaj kutumia biological terms na references ambazo ni michoro na siwez kuieka kiukweli. bado mwl ni kishoka wa kompyuta hahahaha!
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Mwl gfsonwin umeeleza vizuri lakini mimi kakaako sijui umri nao umeenda sana, kuna kitu sijaelewa hapo nilipounderline.
  Unamaanisha Mungu aliumba Nyani ndo wakabadilika kuwa binadamu kulingana na dhana ya evolution? Kama dhana ya evolution inafanya kazi, suala la Mungu kuhusika na uumbaji linakujaje? Msimamo wako Mwl ni kuwa kiumbe wa kwanza alikuwa nani, nyani na alitoka wapi? Au Mungu aliumba nini kwanza?

  Hatuwezi kuichambua hii theory bila kuchanganya Imani ya dini na theory za huyo mpagani Darwin? Nihisi tukichangaya uumbaji kwa misingi ya dini na theory za mpagani ndo tutachanganyikiwa zaidi kama alivyosema Mtambuzi, LOL!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280

  kaka mkubwa HP Mungu alimuumba adam wa kwanza akiwa ni binadamu wa kawaida. but take it from me ingawa alikuwa binadamu mwenye kila ktu kama waleo but alitofautiana asa ngozi yake ilijaa nywele sana for insulation kwani hawakua na nguo zakuwalinda na baridi, pia walikuwa na maumbo makubwa zaid kuliko haya tuliyo nayo na hata siku zao za kuish zilikuwa nyingi sana ias kwamba mtu wa miaka 70 ambaye sasa ni mzee miaka ile alikuwa ndo kwanza kijana wa miaka 10 ma 20.

  kwa concept hiyo evolution ya darwin natuonyesha kwamba binadamu aliyekuwa amefanana na sokwe kabisa aliendelea kuevolute hadi leo ii kuna binadamu mimi. huko tuendako utakuta mtu anazaliwa na kuzaa na kufa ndani ya miaka 20. yaani mtu wa miaka 18 tayari atakuwa mzee.
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Dada yangu gfsonwin, ninakusoma kwa makini sana jinsi unavyodadavua mjadala huu kwa makini kabisa, lakini hapo nilipopigia mstari ndipo ninapotaka kupata ufafanuzi zaidi... Je miaka hiyo walioyoishi hao watu wa zamani ilikuwa ikipimwam kwa kalenda gani? Kumbuka kalenda tunazotumia zimevumbuliwa miaka ya karibuni wakati huo binadamu alishakuwa mjanja. wasiwasi wangu isije ikawa kalenda inayozungumziwa ya miaka hiyo tunayoambiwa binadamu aliishi miaka 800, ilikuwa inapimwa kwa mwezi mmoja kuitwa mwaka...LOL

  karibu uendelee kutupa darasa dada
   
 8. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hapo sasa nimekupata, kuwa kumbe binadamu wa kwanza aliumbwa na MUNGU ila umbile lake lilikuwa kubwa! So evolution theory ya Darwin ikaja na kumshape mwanadamu mpaka ameonekana hivi alivyo leo! Kwa lugha rahisi, Darwin theory kuwa binadamu alianzia kuwa nyani (ingawa hatujui pia huyo nyani alitoka wapi) siyo ya kweli na hivyo watoto wetu wanafundishwa uongo darasani:A S embarassed:! naendelea kuchanganyikiwa. Mtazamo huu hapa umeuangalia kiimani zaidi, vipi kuhusu nje ya imani, huyu binadamu alitoka wapi? Au Mwl wewe unaamini ktk imani pekee?
   
 9. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  nijuavyo mimi miaka ya karne 1 hadi hii ya 21 inahesabiwa kwa kalenda ya kawaida lakian pia hii imedesewa kutoka kwenye zile za BC ambazo zilikuwa hazina utofauti na hizi za kaileo ila tu miez ilihesabaiwa kiebrania na sio kilatin kama leo. ila hapa nasubiri kusahihishwa.

  fact kwangu kama christo alkufa na miaka 32 na alionekana kijana mtu mzima kiasi kile basi ni wazi kwamba alikuwa mtoto sana ukimlinganisha na baba yake yohana aliyekuwa na miaka 140.
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  theory ya darwin sio kama mnavyoielezea. yeye alilenga zaid kuonyesha jinsi kiumbe kinavyobadilika kila uchwao na hii ni kweli. na alichukua umbile la binadamu wa kwanza na kulisadifisha na lile la sokwe tofauti ikaja kwenye species kwamba huyu mu anauelewa ama big and well developed brain ukicompare na sokwe. na hapo ndipo aka deduce theory yake kwamba yawezekana kwamba alitokana na masokwe.

  kuna jinsi ambavyo nilijifunza mwanzo wa uhai dunian kupitia microbiology point of view hii ni kali sana but kuieka hapa nitashindwa kuielezea vyema.
   
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Dada yangu gfsonwin, bado kuna maswali mengi hayajapata majibu,Hebu soma hii, nimeidesa mahali:

  Kisha usome hapa:

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Mhhh kwa hiyo kuna theory za mwanzo wa uhai duniani kupitia microbiology point of view? Si uumbaji tena plus Darwin theory kama ulivyoeleza hapo juu?
   
 13. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hebu dadavua na hii mwalimu..lol
   
 14. Mbwiga88

  Mbwiga88 JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Soma kitabu kinaitwa "one heartbeat away" cha Mark Cahill kaelezea mambo yote haya kwa undani
   
 15. G

  GAGL Senior Member

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Baada ya kusoma post yako kwanza nimegundua bado watanzania tumeendelea kuegemea katika njia moja ya kujifunza, yaani KUJIFUNZA KWA KUSIKIA, hii imetunyima personal initiatives za kujiridhisha na ulichokisikia angalau hata kwa kusoma kilichoandikwa. Naomba nikusahihishe, Binadamu hakuwa nyani na wala hakutokana na nyani au sokwe, vitabu vya historia vinavyoelezea matokeo ya binadamu, hata tulivyoma sisi yaani vya kiswahili vilivyoandikwa na wataalamu vinasema, "BINADAMU ALIISHI KAMA NYANI" Kwa maana hii utakuta mwisho wa siku matokeo ya binadamu wa leo kama ilivyoelezwa kidini na kisayansi, yanagongana. Inawezekana kabisa baada ya Mungu kumuumba Adam, ilibidi aishi kama sokwe ili aweze kuyamudu mazingira yake ikiwa pamoja na kuparamia miti na kula matunda na mizizi pamoja na nyama mbichi. Hii inadhihirishwa watanzania wanaoishi maisha ya kuwinda mwituni hhadi leo hii, ambao mbali na kuwinda, wanategemea sana matunda na mizizi. Pia kuna baadhi ya makabila huko asia wanaishi kama wanyama hadi leo hii (fuatilia discovery channel au nationa geographyy). Ukitafsiri vizuri maandiko ya kitabu cha mwanzo kuhusu uumbaji, unaweza kupata picha kama hii kuwa binadamu aliishi kama nyani mara tu baada ya kuumbwa. Kwa upande wa Charles Darwin, alichoshindwa kutuonesha ni kile chanzo cha huyo kiumbe alianza kubadilika hadi akatokea modern man lakini evolution anayozungumzia hapa inahusisha vitu vingi, ikiwemo mazingira yaliyomzunguka kiumbe huyo ambayo yaliathiri kwa kiasi kikubwa maumbile yake. (mfano angaliia waarabu wengi waliozaliwa huku na kuulia huku, hawaezi kuwa sawa na waarabu waliozaliwa uarabuni) Lakini kikubwa kinachodhirisha maelezo ya darwin ni mabadiliko katika ubongo wa kiumbe husika ambao huwa unakuwa au unabadilika kulingana na mazingira husika, hivyo basi ubongo wa adamu baada ya kuumbwa haukutofautiana sana na ule wa sokwe, ila kutokana na changamoto za kukidhi mahitaji yake kama binadamu, Adamu alianza ku-develop skills katka ubongo wake ikichangiwa sana pia na mabadiliko ya hali ya hewa, kuwepo kwa masika na kiangazi, ukame na mafuriko, baridi na joto nk. Vyote hivi vinaigia katika dhana nzima ya mabadiliko. MABADILIKO AU EVOLUTION SI LAZIMA IKAWA YA MTU KUONGEZEKA KIUNGO AU KUPUNGUA KIUNGO KIMOJA, HATA KUONGEZEKA UWEZO WA KUFIKIRI NI EVOLUTION PIA, STD ONE WA LEO, SI SAWA NA STD ONE WA MWAKA 1900. MSISITIZO: Alichoshindwa kutueleza Darwin, ni mwanzo wa hicho kiumbe pamoja na chanzo cha uhai,ambapo inatupelekea kuamini kuwa kuna MUUMBA.
   
 16. e

  emmanuel chris New Member

  #16
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kulingana na ujuzi nilio nawo, tupo na Bible theory of creation na evolution theory. Maoni yangu ni kwamba tunafaa kuamini kama vile tunavyoelezwa katika hizo theory mbili. Kwakumaanisha hatufai kuongelea mambo ya Adamu na Eva wakati tunafundishwa mambo ya evolution na pia hatufai kuongolea mambo ya evolution kama tukifundishwa creation stories
   
 17. A

  Audi q7 New Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na vip kuhusu cell
   
 18. G

  GAGL Senior Member

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuamini kila tunachoambiwa bila kuchukua hatua za kujiridhisha kama kina uhalisia, ndio tatizo kubwa na chanzo kikubwa cha kuwa na uelewa mfinyu. Kwa mtazamo wangu nadhani ni muhimu sana katika kujifunza theory za matokeo ya binadamu tuangalie tuangalie pande zote yaani theory of evolution na theory of creation. Hapa lengo sio kuiponda biblia na kutukuza sayansi au kuponda sayansi na kutukuza biblia, hapana, mwisho wa siku lazima tupate jibu sahihi kuhusu matokeo ya binadamu. Kama kweli wewe unataka kujua uhakika upo wapi lazima ujifunze sehemu zote mbili maana ukirudi nyuma unaona kwamba binadamu anayeelezwa kwenye biblia kuwa aliumbwa, ndio huyo huyo aliyeiandika hiyo biblia inayomsimulia yeye mwenyewe. Kilichoongezeka kwenye biblia ni source ya uhai, ambapo tumefundishwa kuwa ni Mungu.
   
 19. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  So hatujijui kumbe?
   
 20. fredymkanza

  fredymkanza JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2016
  Joined: Jun 19, 2016
  Messages: 284
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
  Sasa kama tumetokana na nyani
  Swali: Sasa mbona nyani siku hizi hawabadiliki tena?
  Au wameisha
   
Loading...