Mwanzo wa Binadamu, maswali ni mengi kuliko majibu. Je, ukweli ni upi?

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,271
29,879
Kama nilivyosema wakati nafungua huu mjadala kuwa nadharia ya uwepo wa binadamu imejaa utata mtupu.
Katika dini tulifundishwa kwamba binadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa Adam na Eva, na nilipokuwa shule, napo nilifundishwa kuwa chanzo cha binadamu ni nyani, halafu akawa anabadilika hadi kufikia kuwa binadamu.

Lakini bado kuna Maswali najiuliza, hivi ni kwa nini, nyani wengine wamegoma kubadilika hadi leo? Yaani wamebaki kuwa nyani badala ya binadamu.
Je na sisi kwa nini tumesita kuendelea kubadilika?

Kama tulikuwa kama nyani, halafu tukabadilika na kuwa binadamu, inakuwaje tusiendelee kubadilika zaidi na zaidi? Au kulikuwa na mipaka ya kwamba tukifikia mabadiliko kama haya tuliyonayo iwe ndio basi?

Kama ingekuwa binadamu aliumbwa kama nyani na kubadilika kufuatana na mazingira labda na mambo mengine, mbona basi leo hii uhusiano wa kinasaba kati ya binadamu na nyani sio mkubwa kama ule uliopo kati ya binadamu na panya weupe?

Yaani wale panya wanotumika kufanyia utafiti masuala mengi yenye kumgusa binadamu, kwani kinasaba panya hawa wanakaribiana na binadamu.

Basi kuna haja ya kuamini kwamba binadamu wa kwanza alikuwa ni panya kisha akabadilika na kuwa kama alivyo leo.
Lakini bado najiuliza kwa nini huyu panya asiendelee kubadilika, amefungwa na kitu gani?


Hivi karibuni wakati naperuzi peruzi katika mtandao nimekutana na mijadala mikali kuhusu asili ya viumbe hai.
Kwa mfano nchini Marekani mjadala huu umeingia mashuleni ukiwa na nguvu mpya, kutokana na vijana wengi nchini humo kupambazukiwa na kukataa kukaririshwa elimu za wanasayansi wa kale zisizo na mashiko.

Vitabu vingi vya Baiolojia vilikuwa vikisema kwamba asili ya viumbe hai ni mwendelezo wa mabadiliko (Evolution)
Walimu wengi wa nchini Marekani na Ulaya ambako jambo hili limeshika nguvu wanapinga nadharia hii ya mabadiliko na wanaamini kwamba viumbe hai viliumbwa na kitu, jambo au nguvu yenye akili.
Wataalamu wa mabadiliko nao wanapinga na kusisitiza kwamba nadharia yao ni ya kisayansi na ya wale wanaopinga ni ya kidini.

Hivi sasa hata wale waumini wa nadharia ya mabadiliko iliyoasisiwa na Charles Darwin wameanza kuitilia mashaka nadharia hiyo kiasi cha kuitupilia mbali ili kutafuta nadharia mbadala.

Kwa mfano, Mwanabaiolojia mashuhuri kutoka nchini Sweden, Sren Lvtrup, ameweka wazi kwamba, anaamini siku moja nadharia hii ya Darwin ya mabadiliko itakuja kuwekwa wazi kwamba ni nadharia ya uongo kupita kiasi katika historia ya sayansi.

Lakini Nadharia hii ya mabadiliko inaendelea kufundishwa katika mashule yetu ambayo yanahudumiwa na kodi za walalahoi, huku nadharia hii ikiendelea kutiliwa mashaka kila uchao.

Kwa kuwa nadharia ya kidini ina msimamo wake tofauti na ule wa sayansi, sasa kwa nini wanafunzi wasifundishwe nadharia zote mbili, kila moja ikiwa na ushahidi wake ili waweze kupembua ubora na udhaifu wa kila nadharia na kuwawezesha kwa ridhaa yao wenyewe kuamua nadharia ipi kati ya hizo mbili ina ushahidi bora kuzidi nadharia nyingine?

Bado napata kizunguzungu katika kujadili hii mada, kwani kila ninavyozidi kutafuta ukweli nakutana na nadharia zinazopingana, ingawa kila moja haitoi ushahidi unaojitosheleza.

Je wenzangu mnayo maoni gani juu ya hili?

Nahisi mada hii inaelekea kunishinda, naomba msaada wenu.
 
hayo yote ni manadharia yanayotoka akilini mwetu lkn binafsi natumai the universe/ulimwengu unamajibu! dunia ni part ndogo sana iliyo kwenye ulimwengu sasa kuujua ukweli inatupasa tuufahamu ulimwengu vyema,bongo zetu zinauelewa hivyo tunaweza kufanya tafiti tukaelewa what is what... kama dunia ipo kwenye ulimwengu basi ulimwengu utakuwa na viashiria vyote vya kila kitu kilichopo duniani.
nashauri binadamu tuelekeze nguvu ktk kutafiti ulimwengu there we can get a lot of things!
 
Kwanza nikupongeze kwa kuwa mtafiti maana nimeona watanzania wengi ukionyesha njia ya kujaji kitu watakuambia unapingana Na wazungu ulimwengu wote wanaamini wewe nani hadi ukatae' Mimi nilishakutana Na maswali kama hayo kwa watanzania wengi nikaona wananivunja moyo nikaamua kufanya tafiti zangu kimya kimya.....
Come to your topic.
Hiyo nadharia ya kusema binadamu wa kwanza alikuwa nyani yaani nauona ni uongo ambao kama ningekuwa mwalimu wa history ningeona aibu kuufundisha lakini sijui kwanini walimu wetu huwa wanafundisha kitu ambacho wanajua kabisa ni uongo,nilishawahi kuhoji kama binadam wa kwanza alikuwa nyani ni nani aliyeandika historia yake au ni yeye mwenyewe alikuwa anaelewa kuandika historia kama tunavyoandika Sisi Na Sisi tumebadilika mbona wao hawabadiliki tu yani vitu vingine kuamini ni upuuzi kabisa
 
Back
Top Bottom