Mwanza yatajwa kuwa na watoto wabwia ugoro wengi

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Mwanza yatajwa kuwa na watoto wabwia ugoro wengi

Mkoa wa Mwanza umetajwa kuwa ni miongoni mwa mikoa nchini yenye vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji, ulawiti na mimba za utotoni kitendo ambacho kinatajwa kuwa ni hatari kwa ukuaji wa uchumi na kukosa nguvu kazi ya Taifa.

Inaelezwa kuwa katika kipindi cha mwaka 2019, jumla ya kesi 404 zililipotiwa katika dawati la jinsia la jeshi la Polisi mkoani Mwanza "one stop centre".

Katika kesi hizo 404, kesi za ubakaji zilikuwa 174, ulawiti zikiwa kesi 36, ambapo mimba za utotoni zilikuwa 47.

Hayo yameelezwa na ofisa wa dawati la jinsia wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Fortunata Kanda mbele ya Kaimu katibu tawala mko wa Mwanza EMILY KASAGAAL wakati wa kikao kazi cha kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto kilichokutana kuweka mikakati ya pamoja ya kutokomeza mimba za utotoni na ndoa za utotoni.

Kanda alisema vitendo vya ubakaji kwa watoto bado ni tatizo kubwa mkoani humo na nchini kwa ujumla kwa kuwa vitendo hivyo bado vinazidi kuongezeka kila kukicha.

Kanda alisema, kando ya mwaka 2019, pia kuanzia januari hadi machi mwaka huu zimeripotiwa kesi za ukatili wa kijinsia 56 ambapo kati ya kesi hizo ubakaji zikiwa 22 na ulawiti zikiwa kesi 12.

"Katika kesi hizo 56 za mwaka huu, watu waliofika chini ya masaa 72 ni watu 26 na waliokuwa zaidi ya masaa hayo ni watu 28, ukiangalia wastani huo bado ni changamoto ya watu kuchelewa kufika katika vituo vya kutolea huduma," alisema Kanda.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana la Kivulini mkoani Mwanza, YASSIN ALLY amesema pamoja na matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto mkoani humo, kumeibuka wimbi la watoto wabwia ugoro.

Alisema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni mkoa wa Mwanza limeibuka wimbi la watoto wadogo kubwia ugoro na wengine kukihusisha katika michezo inayosababisha kujihusisha na matukio hatarishi.

Alisema kutokana na kutokuwa na mfumo wa udhibiti na malezi watoto wengi wanajihusisha na uvutaji wa ugoro na kucheza michezo maarufu mabonanza ya mchina.

"Watoto sasa wamegeuka kucheza kamali (mabonanza ya mchina) na hii imetushtua sana kuona wimbi hilo la watoto wadogo kucheza mabonanza na wabwia ugoro.

"Jukumu la kulea watoto linapaswa kuanzia katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa ambako huko kuna kamati za ulinzi na usalama ambazo zinapaswa kukaa na kuangalia ni namna gani wataweka mifumo na makatazo ya kusimamia sheria za kudhibiti watoto hao," alisema Yassin.

Yassin pia alisema kuna wimbi kubwa la baadhi ya watoto wanaocheza muziki kwenye sherehe za harusi na kuishauri Serikali kupiga marufuku watoto wadogo kucheza kwa kuwa wapo watoto wenye umri wa kucheza kwenye sherehe.

Kwa upande wake, Kaimu katibu tawala mkoa wa Mwanza EMILY KASAGALA amevitaka vyombo vya dola vinavyosimamia sheria, kuhakikisha uvurugaji kesi zinazohusu mimba za utotoni unakoma.

"Wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wadau wanaosimamia sheria na vyombo vyote ikiwemo mahakama vishirikiane katika kuhakikisha kuzuia uvurugaji wa kesi na kuhakikisha zinasimamiwa vizuri ili ziwe na mafanikio katika Jamii," alisema Kasagala.

Kasagala alisema kuwa, uvurugaji wa kesi unasababisha kukatisha tamaa raia wema wanajiotokeza kutoa taarifa mahakamani hivyo ni muda sasa wa vyombo hivyo kufanya kazi yao.

Mwisho
 
Mwanza yatajwa kuwa na watoto wabwia wengi ugoro

Kama bibi anabwia mjukuu anaachaje ? Af ugoro si madawa ya kulevya wala hakuna sheria ya kuzuia.
Bibi yangu waliwahi kumchanganyia cha arusha kwenye ugoro dar huko. Kichwa kilimzunguka hatari.
 
Back
Top Bottom