Mwanza: Yaliyojiri kwenye Ziara ya Rais Samia Suluhu. Azindua Kiwanda cha Kusafisha dhahabu na Jengo la (BoT)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,788
11,930











Saa Nne Kamili Rais wa JMT Mhe. Samia Suluhu Hassan atawasili mkoani Mwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.

Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika Ziara hii anatarajiwa kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani Mwanza ukiwemo wa ujenzi wa daraja la Magufuli, kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa SGR eneo la fela na kuzindua mtambo wa kuchenjua dhahabu pamoja na kuzungumza na wananchi. Ziara hii inaanza leo Juni 13 hadi 15.

Pia atazungumza na vijana kuhusu fursa za ajira na uchumi.

Tutapeana yanayojiri kupitia Uzi huu.

Karibuni.

UPDATES
10:15
Rais Samia amewasili uwanja wa ndege kwa sasa anasubiriwa awasili katika uwanja vya kiwanda cha kusafisha Dhahabu.

10: 30 Rais Samia amewasili katika Uwanja wa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu kwa ajili ya kukata utepe.

10: 33 Rais Samia amekata utepe kama ishara ya kufunguliwa rasmi kwa kiwanda cha usafishaji wa dhahabu na sasa Rais anaingia ndani kwaajili ya kutazama kiwanda hicho.

10: 36 Rais Samia anapata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu na Watendaji wa kiwanda wakieleza namna gani kiwanda hicho kitakuwa kinafanya kazi.

10: 55 Rais Samia amemaliza kusikiliza maelezo kutoka kwa Wataalam wa kiwanda hicho kwa sasa ameelekea sehemu maalumu ambayo anatarajiwa kuzungumza.

11: 01 Viongozi wa dini wanakaribishwa kwa ajili ya kufungua shughuli kwa maombi. Wote wameombea nchi na wamemuombea kheri na salama Rais katika ziara yake mkoani Mwanza.

11: 10 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mwandisi Robert Gabriel amekaribishwa kwa ajili ya kufanya utambulisho ambaye ametumia nafasi hiyo kuwasimamisha Viongozi na Wageni wote waliohudhuria katika shughuli hii.

11: 52 Waziri wa Madini Dotto Biteko ametoa salamu na kumkaribisha rais kuzungumza na hadhara iliyohudhuria tukio hili.

Hotuba ya Rais Samia wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha kusafisha dhahabu
- Rais anatoa salaam na kutambua uwepo wa Viongozi na wote waliohudhuria akizingatia taratibu za kiitifaki. Sambamba na hilo, Rais Samia ametoa shukrani kwa kualikwa kuzindua kiwanda hicho.

Rais Samia: Ndugu zangu hivi punde nimezindua mtambo wa kusafishia dhahabu na nimeona mambo mazuri yaliyopo mule na mtambo huu pamoja na ujenzi wa kiwanda na ofisi mbili kama mlivyosikia zimegharimu dola za Kimarekani milioni 5.2 (Tsh bilioni 12.2). Aidha, tumeambiwa mtambo huu ni mkubwa na wakisasa ambapo uwezo wake ni kusafisha kilo 480 za dhahabu lakini zinaweza kuongezeka kufikia kilo 960 kwa siku kwa kiwango cha juu kabisa cha kimataifa, yaani dhahabu ya hapa itasafishwa kwa asilimia 99. 9 ambayo ni karibu 100%.

Nimeingia ndani nimeoneshwa kiwanda kinavyofanya kazi, kwa maneno mengine unaweza sema ni miujiza. Nimeoneshwa vigololi vya dhahabu. Vimeingizwa kwenye mitambo ni dakika 3 kama zilitimia, tayari imeshayeyushwa imetengenezwa bar. Kwahiyo ni mtambo ambao ni wa kisasa na purity yake ni ya hali ya juu. Wasiwasi wangu upo kwenye upatikanaji wa malighafi kama kwa siku ni kilo 480 ingawa kuna mashine ndogo ambazo zinasafisha kilo 80 kwa siku nadhani ni kuendana na upatikanaji wa malighafi lakini nina wasiwasi mkubwa kwenye upatikanaji wa malighafi.

Kwahiyo, kama serikali tuna kazi ya kufanya ya kisera, kisheria lakini pia kuwawezesha wachimbaji wachimbe zaidi malighafi ipatikane kwa wingi zaidi.

Manufaa ya mtambo huu pia tumeyasikia yapo mengi lakini nigusie machache. La kwanza, ni kuongeza mapato ya serikali kupitia Mrabaha au tozo za ukaguzi na ushuru wa huduma. Pili, utoaji wa ajira za moja kwa moja ambazo zinakisiwa ajira 120 zitakuwa za moja kwa moja na ajira 400 ambazo sio za moja kwa moja.

Tatu, mtambo huu utawezesha utunzani wa tofali za dhahabu kwa wazalishaji wa ndani na nje. Na nne, utawezesha madini mengine ambata by product kuainishwa na kuthaminiwa hapa nchini na nimeliona hilo. Nimeiona dhahabu ambayo imesafishwa lakini ndani yake kukawa na fedha ambayo pia imesafishwa upande wake na inatengenezwa michi ya fedha kwa upande wake.

Pia, mtambo huu utaiwezesha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanza kununua dhahabu kwa mujibu wa Sheria na hivyo kuwezesha nchi yetu kuwa na amana ya dhahabu. Sambamba na hilo, mradi utasaidia kuchochea shughuli za uchimbaji madini kwenye Ukanda wa Ziwa ambako takribani 90% ya dhahabu inazalishwa kwa sasa lakini kwenye Ukanda huu nimeambiwa kutakuwa kuna viwanda vitatu wasiwasi wangu tu ni kwenye upatianaji wa malighafi. Kwahiyo, tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha malighafi kwenye viwanda hivi zinapatikana.

Zaidi, Mradi huu utachochea shughuli za kiuchumi kwenye Jiji la Mwanza kama tulivyosikia mbali na kujenga mtambo hii Wawekezaji wametenga mtaji wa takribani dola za Kimarekani Milioni 154 sawa na Tsh. Bilioni 346.5 kwa ajili ya kununua dhahabu yote itakayochimbwa kwahiyo kutakuwa na ushindani mkubwa.

Wito wangu tutumie fursa hii WQWachimbaji, Wizara nasi Serikali kuendelea kuimarisha sekta hii ya madini ikiwemo kudhitibi wizi, utoroshaji na biashara ya magendo ya rasilimali zetu za madini, na moja wapo ya maeneo ambayo mnatakiwa kuimarisha ni mgodi wetu wa Tanzanite. Kama tunavyojua Mungu aliipendelea nchi yetu Tanzania peke yake dunia nzima. Ni madini yanayopatikana Tanzania peke yake dunia nzima lakini tunavyokwenda sasa ni kama madini yanayochimbwa dunia nzima. Ukienda kwa majirani zetu kuna Tanzanite nyingi tu.

Kama tulivyosema rasilimali hizi alizotupa Mwenyezi Mungu zinakwenda na kumalizika. Kuna haja ya kukaa kuirebrand Tanzanite yetu, kuna haja ya kuipa jina ambayo itaipa umuhimu na upekee Tnzanite yetu, lakini pia kuna haja ya kuwa na mfumo wa kuidhibiti. Kuwe na mashirika ambayo yataidhibiti Tanzanite yetu ili kuwe na mwamvuli mmoja wa kununua Tanzanite yetu. Kwahiyo, nakuomba Waziri kaa na Wawekezaji mtengeneze mfumo ambao utailinda Tanzanite yetu. Nasemea Tanzanite kwa sababu ndio zao pekee na madini pakee tuliyonayo ambayo tunaweza kuweka jina letu pale.

Kuna changamoto mbalimbali zinazokwamishwa ustawi wa sekta ya madini nchini ikiwemo ongezeko la kodi ya thamani (VAT) kwa Wachimbaji Wakubwa. Pamoja na VAT na kodi ya forodha 25% wa dhahabu inayoingizwa kutoka nje. Haya ni mambo ya kisera na kisheria tutakwenda kuyatizama, lakini kwa vyovyote vile haiingii akilini mtu anatoka na kapu la dhahabu kwa ajili ya kuja kuiyeyusha Tanzania unamwambia atoe VAT na ushuru wa forodha. wakati sisi tuna uhaba wa malighafi.

Kwahiyo nadhani tukarekebishe. Rais Samia amesema VAT kwa madini yanayoletwa kutoka nje idaiwe baada ya kuchenjua, wanaoleta madini kutoka nchi jirani walete yasafishwe halafu kodi zitapatikana baada ya kusafisha malighafi za madini.

Rais Samia aelekea kuzindua Jengo la Benki Kuu ya Taifa (BoT)
- Rais Samia amekwishafika eneo la tukio kwa ajili ya kuzindua Jengo la (BoT) la Kanda ya Ziwa.

Nimefurahi kushiriki shughuli hii nilikuwa napita tu na kuona mabati yamezunguka na kuona majumba yamejitokeza juu lakini sikujua kwa undani kilichomo ndani ya mabati yale lakini leo nimejionea kazi iliyofanywa humo ndani na nimesikia thamani iliyotumika kujenga hapa. Nimeambiwa kwamba shilingi bilioni 23.37 ni kwaajili ya ujenzi na shilingi bilioni 18.73 zimetumika kuweka mitambo na mifumo mbalimbali. Niitumie fursa hii kuipokenza Benki kuu kwa jengo hili zuri na la kisasa.

Jumba hili mbali ya kuimarisha huduma za Benki kuu kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa pia litaboresha mandari ya jiji la Mwanza na hii inaendana kabisa na dhamira ya serikali ya kulifanya jiji la Mwanza kuwa kitovu cha biashara kwenye eneo la nchi za Maziwa Makuu.

Mheshimiwa pamoja na sifa hizo ujenzi gharama kidogo imesisimua mishipa ya damu lakini hili tutalitazama jinsi tunavyokwenda kwa leo ni sherehe ya uzinduzi wa jengo. Fedha zimetumikaje, zimeendaje tutashikana huko.

Pamoja na mafanikio ambayo Benki kuu imeyapata natamani kuona maeneo machache ambayo mnayapa mkazo zaidi. Moja, ni masharti na Riba kubwa ambazo zinatolewa na benki na taasisi za fedha. Watanzania wengi wanashindwa kukopa Benki na kwenye taasisi nyingi za fedha kutokana na Masharti ya kukopa kuwa magumu na viwango vya riba kuwa juu. Mathalani, viwango vya kukopa katika benki ni asilimia 12 hadi 19, viwango hivi ni vikubwa sana kwa mtu wa kawaida.

Hii ndio miongoni mwa sababu Mh. Waziri alisema kwamba Serikali imetunga sera, sheria na kanuni za taasisi ndogo za fedha ili kuhimarisha uratibu na usimamizi wa taasisi hizo. Lakini pamoja na kutunga sera, sheria na kanuni hizo zipo baadhi ya taasisi ndogo za kifedha ambazo zinaendelea kutoza kiwango kikubwa cha riba naomba sana benki zifanyieni kazi suala hilo kama unavyojua Tanzania Informal sector ni kubwa na hatutaki wabakie informal sector.

Benki Kuu jiwekeni tayari kwa sarafu za mtandao (crypto-currency). Ni vyema kujiandaa na maendeleo hayo ili yakija yakute nchi ipo tayari Serikali inaweza kuona haiko tayari lakini wananchi wakaitaka.
 
Acha kuwa nyumbu! Wewe Mungu wao yupi ? Kwamba watu wa Mwanza wao sio watanzania au! Kwa kua tu JPM alitoka huko? Mnaacha kujadili mambo ya msingi kutwa kucha kumuwaza Jpm ! Hawatoki akilini mwenu!
Mungu wa misukule Kama wewe, mkuu gwaji boy yupo kwenye Helcopter anaelekea kumfufua mungu wenu, ,,,,wenzio kina Wakudadavuwa washafika wanaendelea kudemka kabla gwaji boy ajatimba
 
mungu wa misukule Kama wewe, mkuu gwaji boy yupo kwenye Helcopter anaelekea kumfufua mungu wenu, ,,,,wenzio kina Wakudadavuwa washafika wanaendelea kudemka kabla gwaji boy ajatimba
Kifo ni cha kila mtu mkuu. Unaposhangilia kile cha JPM kumbuka kipo cha kwako ambacho wala hujui kitakufika lini na wapi.

Huyu unayemtukana akiwa keshakufa alifia hospitalini mikononi mwa madaktari, wewe unajua utafia wapi?, punguza kufuru za kipumbavu haya unayoandika yanaweza kukutia mkosi.

Chunga sana, punguza utoto unaoonekana kwenye maandiko yako.
 
Jiji la Mwanza likijiandaa kumpokea Mheshimiwa Rais Mama yetu SSH ndio uongozi umekurupuka tangu juzi kuzibua mitaro, kuondoa taka na mchanga, kichekesho zaidi ni Tanesco kufunga bulb za LED za matumizi ya kawaida kwenye nguzo za barabarani anakopitia Mheshimiwa Rais wetu kumhadaa jiji huwa lipo hivyo siku zote.

Kiuhalisia jiji huwa ni chafu na lisilo na mikakati ya kutunza taswira na hadhi ya jiji, mama akitaka kujua anafanyiwa sanaa ashtukize ziara za kushtukiza maeneo ambayo hakupangiwa ajionee mwenyewe. Ni vibaya kumhadaa kiongozi wa nchi.
 
Nyie wapuuzi mliekuwa mnamtukuza mtu Kama ni mungu, na kufikia wakati kutamka kuwa eti atatawala milele hakuna mbadala wake, nahisi hamkujua kuwa maisha na uhai miliki yake ipo kwa muumba tu,
Aya Leo kiko wapi, kufa kila mtu atakufa Chief, ila nyinyi mlihisi bwana mkubwa ye ataishi milele,
Usiweke wote kwenye kapu moja, jitahidi kuandika vitu sio kwa kauli za jumla jumla. Usifurahie kifo cha mtu na usidhani kuwa wote wanafurahia vifo vya watu.

Tuliokuzwa na mafunzo ya dini hatuwezi kufurahia kifo cha mtu na hatuwezi kutaka mtu atawale bila ya ukomo. Ni Mungu tu ndio asiye na ukomo.

Jishushe, punguza hayo maneno ya visasi kwani hujui hata dakika kumi kuanzia sasa utakuwa katika hali gani.
 
Nyie wapuuzi mliekuwa mnamtukuza mtu Kama ni mungu, na kufikia wakati kutamka kuwa eti atatawala milele hakuna mbadala wake, nahisi hamkujua kuwa maisha na uhai miliki yake ipo kwa muumba tu,
Aya Leo kiko wapi, kufa kila mtu atakufa Chief, ila nyinyi mlihisi bwana mkubwa ye ataishi milele,
dhihaka ile ndio maana Mungu alimuondosha, sasa wanaanza tena kumchuria Mama.
 
mungu wa misukule Kama wewe, mkuu gwaji boy yupo kwenye Helcopter anaelekea kumfufua mungu wenu, ,,,,wenzio kina Wakudadavuwa washafika wanaendelea kudemka kabla gwaji boy ajatimba

Nyie wapuuzi mliekuwa mnamtukuza mtu Kama ni mungu, na kufikia wakati kutamka kuwa eti atatawala milele hakuna mbadala wake, nahisi hamkujua kuwa maisha na uhai miliki yake ipo kwa muumba tu,
Aya Leo kiko wapi, kufa kila mtu atakufa Chief, ila nyinyi mlihisi bwana mkubwa ye ataishi milele,
Kumbe Chadema nao wanakufa.Naona Prof Baregu nae kafa
 
Back
Top Bottom