Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,797
- 11,959
Kutoka katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tayari viongozi wa kiserikali na Chama cha Mapinduzi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani wameshaanza kuingia kwenye uwanja huu tayari kumuaga mpendwa wetu Dk John Magufuli.
Mageti ya uwanja wa CCM Kirumba yamefunguliwa toka saa 12 alfajiri na wananchi ni wengi sana ambao wako nje ya uwanja wakiendelea kuingia kwenye uwanja huu.
Mikoa zaidi ya mitano ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Tabora na Mara yote wananchi wake kwa uwingi wao wanaendelea kuingia kwenye uwanja huu.
Mwili wa aliyekua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli aliyefariki Machi 17 mwaka huu utaagwa kwenye uwanja huu kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Chato, Geita kwa ajili ya mazishi.
=====
MWANZA: Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli umeshawasili Mwanza ambapo idadi kubwa ya Wananchi wameonekana wakiwa wamejipanga barabarani na wengine wakisindikiza mwili wakati ukipelekwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Dkt. Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 na anatarajiwa kuzikwa Machi 26 Chato Mkoani Geita.
Baada ya mwili wa Hayati Rais Magufuli kuwasili jijini Mwanza, utapelekwa nyumbani kwa mjane wake, Mama Janeth Magufuli, maeneo ya Busisi, kupitia katika daraja la Kigongo-Busisi.
Jeneza lenye mwili wa Hayati Rais Magufuli litasimamishwa Busisi kwa dakika 10, kwa ajili ya kutolewa heshima za mwisho.
Baada ya mwili huo kutolewa heshima za mwisho mjini Busisi, utapelekwa Wilayani Sengerema, Geita Mjini hadi Katoro wilayani Chato, Mkoa wa Geita.