Mwanza yajiunga na ligi ya miji inayopata huduma ya usafiri kidijitali baada ya taxify kuingia rasmi jijini humo

Apr 16, 2018
19
7
DC-NYAMAGANA (b).jpg

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Ms. Mary Tesha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyozinduliwa hivi karibuni jijini humo. Jiji la Mwanza sasa limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Kampuni ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
SHIVACHI MULEJI(1).jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki, Shivachi Muleji (kushoto) akikabidhi fulana kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Ms. Mary Tesha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Jiji hilo sasa limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Kampuni ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
REMMY ESEKA.jpg

Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini Tanzania, Remmy Eseka akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify hivi karibuni jijini Mwanza. Jiji hilo limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Taxify, Kampuni inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
FID Q.jpg

Msanii wa muziki wa hiphop, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.
MILIMBILWA KIPIMO(b).jpg

Meneja wa Taxify Kanda ya Ziwa, Milumbilwa Kipimo akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hafla ya uzinduzi ya huduma ya Taxify hivi karibuni jijini Mwanza. Jiji hilo limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Taxify, Kampuni inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.

  • Mwanza, ‘The Rock City’ kama inavyofahamika kwa wengi nchini Tanzania, imeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa huduma ya usafiri kidijitali jijini humo.
Mwanza. Taxify, ambayo ni miongoni mwa Kampuni kubwa zinazotoa huduma ya usafiri kidijitali barani Ulaya na Afrika imezindua rasmi huduma zake jijini Mwanza huku mamia ya madereva wakiwa tayari wamesajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo yote ya jiji.

Katika kusherekea uzinduzi wa huduma hiyo, Taxify inatoa punguzo la asilimia 50 kwa abiria kuanzia tarehe 28 Mei, 2018 mpaka mwisho wa mwezi wa sita mwaka huu. Gharama za usafiri kwa kipindi hiki ni:- Kuanza safari ni TZS 700, Kwa kilometa ni TZS 460, Kwa dakika ni TZS 70 huku gharama ya chini kabisa ya safari ikiwa ni TZS 2,000.

“Mwanza ni jiji lenye watu zaidi ya milioni 3.5, barabara nzuri zenye ubora, Huduma bora ya mitandao inayopatikana kirahisi na maelfu ya magari. Tulifanikiwa kupokea maombi mengi kutoka kwa wakazi wa jiji hili waliokuwa na shauku ya kutumia huduma yetu lakini huduma yetu ilikuwa bado haijafika jijini hapa, jambo hili limetusukuma kuzindua rasmi huduma yetu leo jijini hapa. Mamia ya madereva wameshasajiliwa kwenye jukwaa letu na tayari tumeshaona mamia ya safari ambazo zimefanyika hata kabla ya uzinduzi rasmi. Mwanza ipo tayari kwa huduma ya usafiri kwa njia ya mtandao na tunaimani kuwa huduma hii itafanya vizuri katika jiji la ‘Rock City’ alisema Remmy Eseka, Mkuu wa Operesheni, Taxify Tanzania.

Mary Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wa uzinduzi wa Taxify Mwanza, alisema "Kama Serikali tumejenga miundombinu na kupitisha kanuni ambazo zinaunda mazingira wezeshi ya biashara na wawekezaji kuja kutoa fursa kwa Watanzania. Huduma hii ya usafiri kwa njia ya mtandao imeonekana kuboresha maisha katika miji/majiji kwa kutoa fursa za kuongeza kipato kwa madereva, usafiri wa uhakika, na nafuu kwa wakazi. Mwanza sasa ipo tayari kujiunga na ligi ya miji ya kisasa duniani na tunaanza kwa kusherekea na ujio wa Taxify”.

Furaha ya madereva humaanisha huduma nzuri na bora kwa abiria. Taxify inaamini katika maelewano mazuri na madereva wake, kuhakikisha kuwa wanapata kipato zaidi ya wanachopata kutoka kwa washindani huku ikiwapa aina mbalimbali za ulinzi na vipengele vinavyowasaidia kufanya kazi kwa njia inayofaa kwao. Pia Taxify inaamini katika utoaji wa huduma iliyotukuka kwa abiria wake, huku ikiwa na timu ya huduma kwa wateja ya hapa hapa nchini na chaguo la kulipa kwa fedha taslimu.

Taxify imekuwa ikifanya kazi katika jiji la Dar es Salaam tokea Desemba 2017 na tayari ina maelfu ya madereva wanaojipatia kipato kutokana na kutumia program yake. Programu hiyo inaruhusu madereva kutumia muda mwingi barabarani na muda mchache sana katika maegesho kusubiria wateja.
***​
Kuhusu Taxify
Taxify ni miongoni mwa kampuni barani Ulaya inayoongoza katika utoaji wa huduma ya usafiri kwa njia ya mtandao, ikiunganisha mamilioni ya watumiaji usafiri na madereva ulimwenguni katika kurahisisha huduma ya usafiri, kwa haraka na ufanisi zaidi. Ufanisi wa Taxify na teknolojia ya biashara yake inawanufaisha wote madereva ambao wanalipa kamisheni ndogo sambamba na abiria ambao wanalipa nauli ya gharama nafuu.

Taxify ambayo iliasisiwa na Markus Villig ilizunduliwa mwaka 2013. Ni kampuni ya utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao inayokuwa kwa kasi ulimwenguni ikijikita zaidi Ulaya na Afrika.

Nchini Tanzania, Taxify inafanya kazi jijini Dar es Salaam. Taxify ina wateja zaidi ya milioni 10 katika nchi 20 ulimwenguni. www.taxify.eu

Taxify ina wateja zaidi ya milioni 10 katika nchi zaidi ya 20 duniani kote. Programu ya Taxify inapatikana kwenye mifumo ya iOS na Android.

Kwa taarifa zaidi tembelea www.taxify.eu
 
Mwanza is overrated,
Mwanza City haina 3.5ml pple ukitaka jua hili angalia usafiri wao wa umma, vile vipanya havuwezi ferry all that ppl
 
Mwanza is overrated,
Mwanza City haina 3.5ml pple ukitaka jua hili angalia usafiri wao wa umma, vile vipanya havuwezi ferry all that ppl
Tatizo lako unaangalia nyamagama na ilemela tu, hujui hata kolomije, ngudu na magu vipo mwanza?
 
Tatizo lako unaangalia nyamagama na ilemela tu, hujui hata kolomije, ngudu na magu vipo mwanza?
Jiji la Mwanza linaundwa na Ilemela na Nyamagana tu, the rest ni halmashauri zingine tu. Tofautisha mamlaka za serikali za mitaa (Jiji, manispaa, miji) na mamlaka ya serikali kuu (Wilaya, Mkoa). Wewe unachanganya Mwanza mkoa na Mwanza jiji.
 
Back
Top Bottom