Elections 2010 Mwanza: Watu watawanywa kwa mabomu wakimsubiri Dr. Slaa

Ilulu

Senior Member
Mar 22, 2008
161
31
Tafadhali walioko Mwanza watujuvye, kuna taarifa kuwa Polisi wanatawanya watu wanaokusanyika kusubiri Mapokezi na Mkutano wa Dr. SLAA
 
Chadema mkoa waliomba mkutano kufanyikia Uwanja wa Furahisha ama Magomeni Mwanza, na wakachelewa kupewa majibu, ikabidi watangaze kuwa mkutano wa Slaa ni leo, sasa Msimamizi wa Uchaguzi akatoa taarifa leo mkutano usifanyike Furahisha maana kuna majukwaa ya mahubiri ya dini lakini watu walishajaa toka asubuhi na FFU wakaenda kuwatimua kwa mabomu. Sasa mkutano unahamia Magomeni.....
 
Sio tetesi tena ni taarifa kamili... msimamizi wa uchaguzi anaitwa Ibrahim Lyimo
 
Kuweni wavumilivu mda ulo baki ni mdogo make siasa za maji taka tutaziondoa hv karibuni.
A%20S%20103.gif
 
yaani watu wamekusanyika toka asubuhi?duuh na hawa hawajafuatwa na malori kama chana fulani hivi..hahaaaaa presha inapanda presha inashuk..wapi Makamba.Vipi unamleta mgombea wako kwenye mdahalo au?
 
hata wafany nini hiyo haiepukiki.....labda wapande juu wakamshawishi Mungu.....Dr Slaa is the new Presdaaa
 
Tupeni mambo yanayojiri huko... nasikia upepo unavuma vibaya sana kwa CCM na kundi lao la mafisadi kanda ya ziwa... Ni kimbunga ambacho hawakukitarajia, walijua wasukuma ni akina "nduhu taabu" lakini baada ya huyu Mba'rbaige kuweka karata yake upepo umebadirika sana sana wataanza kutumia nguvu
 
Huyu msimamizi ni chama gani vile?

Ni yule aliyetaka kumnyima mgombea ubunge wa chadema haki yake ya kuchaguliwa kwa kisingizio cha pingamizi la kilaza masha.

Ni mwana CCM damu. kwa hali hii kwa nini asishiriki mbinu chafu ya kuiba kura ama kumpa ushindi masha
 
Wakati ulikubaliwa ndio sasa na hapatakuwa na wakati mwafaka tena zaidi ya wakati huu
chadema oyeeeeeeeeeeeeeeeeehhhhhhhhh
 
Niko Mwanza hali bado ni tete katika maeneo yote yanayozunguka uwanja wa FURAHISHA, ambapo tangia asubuhi Chadema alikuwa wanaandaa mkutano wao. Mabomu ya machozi bado kama kawa. MAnispaa ya Jiji imekataa kutoa uwanja huo kwa ajili ya mkutano huo. Tangia TArehe 17/10 wamekuwa wakiwazungusha ili Chadema wasitumie uwanja huo. Yasemekana wametakiwa sasa kutumia uwanja unaoitwa MAGOMENI ambao ni mdogo unaoweza weka watu sio zaidi ya 200. Uwanja huo umezungukwa na makazi ya watu. Mwenyekiti wa CCM amekuwa akihubiri amani kumbe moyoni anamaanisha vurugu.


CHAGUA CHADEMA!!!!!!
 
Chadema mkoa waliomba mkutano kufanyikia Uwanja wa Furahisha ama Magomeni Mwanza, na wakachelewa kupewa majibu, ikabidi watangaze kuwa mkutano wa Slaa ni leo, sasa Msimamizi wa Uchaguzi akatoa taarifa leo mkutano usifanyike Furahisha maana kuna majukwaa ya mahubiri ya dini lakini watu walishajaa toka asubuhi na FFU wakaenda kuwatimua kwa mabomu. Sasa mkutano unahamia Magomeni.....

Umeeleweka!!
 
ccm wanawewesekam kila kukicha walidhani watz ndiyo walewale wadanganyika kumbe kila siku wanaelimika pamoja na kuwa shule za kata ni za walala hoi na sio watoto wa kikwete wala makamba.............
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom