Mwanza: Wanaodaiwa kusafirisha dhahabu wapandishwa kizimbani, wasomewa makosa 7

Polisi wetu wamekuwa kero sana kwa kweli,huku mtaani kwetu wameua mtu katika mazingira ya kutatanisha,lakini mpata leo sioni kinachoendelea.N kama wanajiona wako untouchable hivii.Jeshi la polisi linahitaji complete overhawl kama ilivyofanyika 1974.Cosmetic changes zinazofanyika kwa sasa hazitatusaidia sana.

Mkuu hapo Congo tusubirie Felix Chisekedi atapokamata kupata total overhaul.
 
Mbona hata kupelekwa mahakamani ni kuheshimu utawala wa sheria..watu wamekutwa na dhahabu na hela cash..na hao waliowasindikiza ambao wametumia mali za serikali kujinufaisha..ningekua mm hata mahakamani wasingepita wangenyooka magereza tu tena baada ya kuwatemesha mzigo wote waliochukua
Wewe una huruma mimi maamuzi ya Rais Durtete yangetumika ili wengine wasijaribu milele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umefuatilia hili sakata toka mwanzo lakini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeyaona yote yaliyosemwa toka mwanzo, lakini mimi na wewe hatuna taarifa halisi itakavyotolewa mahakamani. Tuvute subira.
Yatakayosemwa huko na kutolewa uamzi, ndiyo yatakayotupa picha halisi kama kulikuwa na mchezaji wa ziada katika timu ya mashtaka. Sasa hivi hatujui chochote, ila yanayosemekana tu!
 
Mwanza. Watu 12 wakiwemo askari polisi wanane watapandishwa kizimbani muda wowote leo Ijumaa Januari 11, 2019 katika mahakama ya hakimu mkazi Mwanza.

Wamefikishwa mahakamani hapo leo na wanasubiri kupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Watu hao wanadaiwa kuhusika na tukio la kusafirisha shehena ya dhahabu kilo 323.6 na fedha taslimu Sh305 milioni kutoka mkoani Mwanza kuelekea Geita.

Wanashikiliwa na polisi tangu tukio hilo lilipotokea Januari 5, 2019.

Askari watakaopandishwa kizimbani leo walitajw ana Rais John Magufuli siku mbili zilizopita kuwa wanadaiwa kuhusika katika tukio hilo, kuwasaidia wahusika kufanikisha kusafirisha shehena hiyo.

Chanzo: Mwananchi

=====

WALIODAIWA KUTOROSHA DHAHABU WAFIKISHWA MAHAKAMANI: Watuhumiwa 12 wa utoroshaji wa Dhahabu waliokamatwa hivi karibuni wamefikishwa mahakamani alasiri hii wakiwemo askari wanane (8) waliokamata dhahabu hiyo.

Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakamani ya Hakimu mkazi wa Mkoa wa Mwanza huku wakikabiliwa na makosa Saba (7).
Kufia uwanja wa mapambano ni ushujaa

Jr
 
Safi sana mheshimiwa raisi wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,hakika ww ni raisi wa wanyonge!

rais wa wanyonge haina uhalisia

polisi wanane wanaenda kushikiliwa miaka 10 mahabusu, bila kesi, bila hukumu

kijana wa kihindi ataendeshewa kesi yake fasta, atapewa faini ya milioni 200, atalipa

rais wa wanyonge anatoka wapi hapo?
 
Mwaka jana mda kama saa tatu usiku napita zangu karibu na rock city mall sina hili wala lile nastuakia napigwa jeki,sitatulia vzr nipo kwenye tenga,askari kama wawili wana sachi mifuko eti sijui wanatafuta bangi,utadhani waliambiwa mm ndo muuzaji halafu watu kibao wana sachiwa lakn badala watafute bangi wanaondoka na vyote vilivyo kwenye mifuko ya suruali.


Noma sana ila niliongea na kujitambulisha kwa mkubwa wao ndo nikaachiwa ila sikupata vitu vyangu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Fake story katibu na rocky city mall upande upi wakati pande zote zi na majumba ya watu acha uongo wewe
 
Askari polisi wanane wanaotuhumiwa kushiriki mpango wa kutorosha dhahabu kilo 319.59 zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 27 pamoja na wamiliki wa madini hayo, wamefikishwa mahakamani.
1.jpg


Washtakiwa hao waliokamatwa Januari 4, mwaka huu, walifikishwa mahakamani kwa makosa 12 likiwemo la uhujumu uchumi.

Walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Gwae Sumaye, na mawakili wa serikali Castuse Ndamgoba, Robert Kidando na Jackline Nyantori.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Januari 4, watuhumiwa wanne ambao ni Sajid Abdallah, Kisabo Nkinda, Emmanuel Kija na Hassan Sadick walitenda kosa la kuwapatia rushwa ya Sh. milioni 700 watuhumiwa wanne ambao ni askari polisi ili kuwasaidia kutorosha madini hayo.

Askari ambao majina yao yalitajwa na mawakili wa serikali ni Koplo Dani Kasara, Koplo Matete Misana na makonstebo Japhet Kuliko, Maingu Sorry, Alex Mkali, Timoth Paul na David Ngelela na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Moris Okinda ambaye alikuwa kiongozi wa askari hao.

Miongoni mwa mashtaka 12 yanayowakabili askari hao ni pamoja na uhujumu uchumi, kuomba na kupokea rushwa ya Sh. milioni 700, kuisababishia hasara serikali na kutakatisha fedha kinyume cha sheria za nchi.

Hakimu Gwae alisema watuhumiwa hawaruhusiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, hivyo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 28, mwaka huu, itakapotajwa.

Askari hao wanane, kabla ya kufikishwa mahakamani, Jeshi la Polisi Tanzania liliwasimamisha kazi Januari jana kutokana na tuhuma za kutenda kosa kinyume cha mwenendo mwema wa jeshi hilo.

-4.bp
 
Kazi IPO. But natamani kupata story upande wa pili wa watuhumiwa walikuwa wanatosha dhahabu. Isije ikawa kama habari za mwadui diamondi yaani alimasi zinakamatwa airport huku wanavibali vyote vya kuafirisha vilivyotolewa na serikali. Awamu hii ni ya kuitilia mashaka kilajambo inalofanya. Maana haiaminiki kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom