figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Mwanza. Watu 12 wakiwemo askari polisi wanane watapandishwa kizimbani muda wowote leo Ijumaa Januari 11, 2019 katika mahakama ya hakimu mkazi Mwanza.
Wamefikishwa mahakamani hapo leo na wanasubiri kupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Watu hao wanadaiwa kuhusika na tukio la kusafirisha shehena ya dhahabu kilo 323.6 na fedha taslimu Sh305 milioni kutoka mkoani Mwanza kuelekea Geita.
Wanashikiliwa na polisi tangu tukio hilo lilipotokea Januari 5, 2019.
Askari watakaopandishwa kizimbani leo walitajw ana Rais John Magufuli siku mbili zilizopita kuwa wanadaiwa kuhusika katika tukio hilo, kuwasaidia wahusika kufanikisha kusafirisha shehena hiyo.
Chanzo: Mwananchi
=====
WALIODAIWA KUTOROSHA DHAHABU WAFIKISHWA MAHAKAMANI: Watuhumiwa 12 wa utoroshaji wa Dhahabu waliokamatwa hivi karibuni wamefikishwa mahakamani alasiri hii wakiwemo askari wanane (8) waliokamata dhahabu hiyo.
Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakamani ya Hakimu mkazi wa Mkoa wa Mwanza huku wakikabiliwa na makosa Saba (7).